Tuesday, May 22, 2012

MWANAMKE ALIYEUMIZWA NI KAMA WAYA WENYE SHOTI,UKIGUSA VIBAYA TU MAIN SWITCH INAZIMIKA

Kama wewe ni mwanaume na umepata mwanamke ambaye amewahi kuumizwa,ukakaa nae mwaka wa kwanza,na miaka mingine juu,na ukashindwa kufanya kazi yako sawasawa ili kumponya na kumsahaulisha kabisa kwamba alishawahi kupopolewa kama embe huko nyuma jua umefeli mtihani...

Kuwa Mwanaume kwenye uhusiano sio kitu kidogo,sio tu kuvaa suruali na tai...Sio tu kujisifia This is my Girlfriend...Kumfanya mwanamke ajisikie malkia,kusahau ya nyuma,sio kazi ndogo...fanya kazi...pepeta mchele sawaswa,tenganisha pumba....

Fanya vitu vitakavyomfanya Mwanamke ajihisi yuko Mbinguni kumbe yuko Tandale....

Mfanye Mwanamke ajisikie vibaya kwamba kwanini alichelewa kukutana na kidume wewe, asahau kwamba kuna Bwege mmoja alishawahi kukabidhiwa huo  moyo,na badala ya kuupaka Asali ili ung'ae yeye akaupaka Spirit ya kuoshea Vidonda

3 comments:

  1. Umetishaaaaa!!!! Darasa zuri sana aisee

    ReplyDelete
  2. Dah bonge la message i real like it.

    ReplyDelete