Sunday, February 3, 2013

UFANYE NINI UKIGUNDUA PENZI LAKO LIMEINGILIWA NA MTU NA BADO UNAMPENDA ANAYEKUCHEAT?

TUMA NENO SETH KWENDA 15678 NA UTAUNGANISHWA NA HUDUMA YANGU YA MOBILE AMBAYO ITAKUPA ZAIDI YA HAYA UNAYOYASOMA HUMU MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO KAMA SMS....

Leo naomba tudiscuss topic hii,maana naamini kama sio wewe yanakukuta haya basi ndugu yako wa karibu au rafiki yako analalamikia hili...

Imewahi kutokea unampenda mtu sana na mmekaa kwa muda flani mrefuuuu,halafu katikati ya safari unakuja kugundua kuna kidudu-mtu,whether ni Mwanaume au Ni Mwanamke ameingia kwenye Penzi lenu na umekuwa Shareholder kwenye Kampuni ya Mahaba Limited???

Huwa unafanyaje ukigundua Mahabuba wako anaibiwa namtu flani na wewe bado unampenda???

Je unasusa na kuamua kumuachia Kidudu-mtu ashinde Battle kiulaini???

Au unakomaa na Battle na kumfunza adabu kidudumtu hadi anaachia ngazi???

Unatumia ujanja gani kama ni Boy wako na unampenda,lakii mchizi amefall kwa kidudu-mtu na unakaribia kutoswa na Mchizi kisa kanogewa na Penzi jipya tam tam???

Maswali ni mengi lakini all in all,LEO nataka nikupe Mbinu tu ambazo zitakufanya upigane hiyo vita na USHINDE....Ukifuata haya,Probability ya wewe kushinda na kutunza Penzi lako ni 0.7%...

Mambo haya ni muhimu uyajue maana yanatokea kila siku,Kama bado hayajakukuta basi yatatokea,Kula Shule,siku yakikukumba basi unajua Mlango wa kupigia Bao...TWENDE KAZI:

1.INAWEZEKANA KOSA NI LAKO

Mara nyingi tukiwa kwenye Mapenzi tunajisahau sanaaaaaa,tunahisi tumemaliza,nishampata basi inatosha..Ubunifu sifuri,we mbuzi kagoma tu miezi mia 7,hujui kitu ingine..Chalii angu inakula kwako...Mwenzio akitoka anapigwa Jackie chan,Mission Impossible 6 na Kandahar....We upoupo tu unaegesha kama Parking ya Corner Bar.....INAKULA KWAKO

Jambo la kwanza,weka possibility kwamba moja ya sababu zilizomfanya jamaa/demu atoke ni WEWE...Usi-throw lawama kwake tu wakati kumbe na wewe si ajabu ulikuwa na mapungufu yaliyochangia...

2.KUWA MPOLE

Ukishaweka Possibility ya wewe kuwa moja ya sababu we kuwa mpole...Jipange kwa mbinu za Comeback kama Manchester...Ukifungwa huendi nyuma kuanza kulia,unajipanga na mashambulizi ya kusawazisha..hiyo ndo Battle....

Sasa wengine wanapanic,wanaanza kumtusi jamaa/demu,ooh we malaya sana,umekosa nini kwangu.....ipo siku atakujibu,nakosa nyamaaaa,we unanipikia maharage tu!Utafanyaje???

Kupanic hakusaidii,tena ukipanic ndo atahamia kule mazimaaaaaaa,utabakia unatokwa povu tu mwenzio anapewa mijiraha!Kuwa Mpole

3.TAFUTA TATIZO NI NINI ILI UJUE UNAINGIA NA SILAHA GANI

Huwezi kuua Nzi na AK 47...Jua adui ni nini uchague Zana ya kudeal nae...

Hii ni mtihani pia kwa sababu kwa Mwanaume anayecheat kufunguka kwamba ni nini haswa kilichomtoa ni ngumu sana.....Na tatizo lingine ni kwamba hata akisema utamchukuliaje??Wanawake hawapendagi kuambiwa ukweli na ukimwambia,hata kama ndo ukweli atanuna mbaya,ufudu haingii!Mnuno haswa!Anauliza halafu ananuna.....Hilo moja,Wanaume nao ni worse...Akiuliza nini kimekutoa ukamwambia,ah we unanipa goma dakika 5 wakati mwenzio anasimamaia Show ya Fally Ipupa saa nzima...duh,mtu mzima unahisi umekosewa heshima unamwagia makofi!HAISAIDII!
Ukiambiwa we Selfish dakika 5 chali,chukua kama Positive issue na ujifunze...Kama huwezi zaidi ya dakika 5 jifunze wenzio wanasimamiaje kucha...Mwanaume dakika 5 aibu jamani khaaa,Mchuchu anapandisha Kilima anapishana na wewe ndo unaserereka kwenye ganda la ndizi.....Aaaaaaa,sio kiivyo!

Ukipata Kiini cha tatizo BADILIKA!Akisema unalewa sana humpi haki yake BADILIKA...Akisema humpigii simu na Mwasiliano yamekuwa hafifu na huku kwa Bi Kidude anapigiwa mara 76 kwa siku,BADILIKA.....Hakuna jinsi,kama Blunder ushafanya,wajanja wamefill GAP,Pigana ili arudi kwako kwa kubadilika kwa kile alichosema.

Kasheshe ni pale unapoambiwa tatizo ukakasirika....Au kutojibiwa kiini cha tatizo,,,Kila Ukiuliza anasema ah niliamua tu...au imetokea tu..Hapo unalo,inabidi utafute mahali muafaka pa kumuuliza,na most probably muda mzuri ni akiwa anakanyaga kitonga,hapo utajibiwa yote maana hisia zinakuwa ziko juu...

4.FANYA ANAYOPEWA KULE NA ZAIDI

Hakuna kitu kizuri kama kumpa Mpenzi wako vyote ili akose vya kuomba nje!

Usiache hata tundu moja la kidudu kuingia na kusambaratisha.....Mpe Mawasiliano kwa Asilimia Zote.....Mpe Attention....Mpe hela ukiweza...Mpe Mahaba makali yenye Kungfu,Taekwondo na Kila kitu....

Hakuna Mwanaume atamuiba maana unapata vyote....Hakuna Mwanamke atampa lolote ambalo wewe hujui,Viuno vyote wavijua,Feni Mbovu Style,Feni nzima,Air Condition Moves,Mupeeee.....

Kama umegundua tatizo ni Mahaba uliyokuwa unampa badilika,kuwa mbunifu from NOW going forward...Si unampenda???Usijali kwamba kuna Competition,wewe fanya kwa nafasi yako....Mchoshe hadi akiwaza kuamka kwenda kule akute hana nguvu tena,atabaki kwako..Dozi Tu!

Baada ya muda utagundua amerejea,Kule alikoibwa hakuna Jipya tena,atabakia wako na utaishinda vita ILA,Jifanye bandidu,eti unamnunia kwanini kaenda kule....Au unamtafuta huyo Mwanaume Mpya au Mwanamke Mpya unaanza kumtukana,eti ooh ntakukomesha,unaiba vya watu,mara ooh ntakuloga uvae chupi usoni...ah wapi,unafeli....Dawa ya mwizi ni kumkimbiza kimyakimya,wala kelele hupigi,mwenyewe atahisi huyu niliyemuibia leo sio wa kawaida,ila makelele ya mwizi mara vile,wote mtaonekana wezi.....

KIMBIZA MWIZI KIMYAKIMYA....JIPANGE KIMYAKIMYA....SHAMBULIA KIMYAKIMYA
TUMA NENO SETH KWENDA 15678 NA UTAUNGANISHWA NA HUDUMA YANGU YA MOBILE AMBAYO ITAKUPA ZAIDI YA HAYA UNAYOYASOMA HUMU MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO KAMA SMS....