Thursday, July 26, 2012

MAKE YOUR BED ALIVE ILI UHUSIANO WAKO UDUMU

Nimelazimika kuandika hili japo sikupenda sana kuingia so deep kwenye issue za Bed lakini nimegundua watu wengi wanakosea hadi hapa pia...


Kuna siri kubwa sana kwenye Kitanda....Hapa ndio kila kitu kuhusu wapendanao wawili hutokea.Mtadanganyana mtaani,mtaenda Outing,Mtapeana maua,mtanunuliana zawadi,mtaenda Movie,Mtafuliana nguo na kupikiana,lakini mwisho wa siku lazima mfike NGOME KUU.....Ngome kuu iko kwenye Kitanda...


Na hapa ni wote wawili wala sio Mwanaume tu,au Mwanamke tu....Kila mmoja ana matatizo yake


Kuna wanaume wanakosea na wanawake wanaokosea pia..Shida kubwa ya kukosea mkifika ngome kongwe ni kupafanya ngomeni pawe sio exciting anymore na inakuwa utumwa....Nimewahi kuongea na watu kadhaa ambao kwao Love making sio issue tena,hawaifeel,hawana hamu,na ikitokea wamefanya basi ni kwa sababu ni wajibu tu jamaa anataka ila si kwa mapenzi yake...This is bad...Mi naamini hakuna mtu asiyependa kumake Love ila kuna watu wameharibu feeling za watu kiasi kwamba mtu anaona kumake Love ni kama adhabu,nothing is exciting in it wakati ni tendo la raha raha raha siku zote kama mkijua la kufanya.


MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UKIWA NGOME KONGWE


1.MAPENZI NI SANAA NA SAYANSI
Huwezi kukurupuka tu linapokuja suala hili...Sanaa inatakiwa.Kama wewe ni Mwanaume jua una kazi kubwa sana kwenye hili jambo....Sanaa inaanza kabla hata hamjaenda,unamuandaaje huyo mtu mkiwa mnakwenda,Ile sio Quiz kwamba unamshtua mtu tu kama Amri,Bebii Quiz now...Bebi tufanye,ah ah...Mtengeneze kisaikolojia Mwanamke kwanza kwa maneno,ili aanze kufeel,na kama hayuko interested atasema,ni mbaya kwenda ngome na mtu ambaye hana hamu siku hiyo.Inawezekana ana mambo yanamsonga,ana stress fulani,MSIKILIZE.Sio kisa we umebanwa basi unakimbilia tu chooni,hapana
Nimeongelea suala la kumuandaa mwanamke kisaikolojia maana wanaume Every time is tea Time...Mwanaume hata umshtue sa 10 usiku vitu utapata,wala hahitaji kupashwa moto kama kiporo,ukibonyeza tu swichi lazima taa iwake


2.UVIVU MWIKO
Linapokuja suala la Uvivu...Hapa wote mnaingia...Kuna wanawake ni wavivu,wakiwa ngome utadhani kuku aliyebanikwa,mpaka mpishi akugeuze...Inaboa sana.Kama hutaki sema,ila Wanawake shurti kushughulika,usimwachie Mwanaume kazi yoooteee utafikiri we umeenda pale kuchinjwa halafu yeye ndo mchinjani,kitandani sio Kibla....Kukuruka!Muonyeshe na wewe wamo.Wengine eti wanaogopa wataonekana malaya,aliyekwambia hivyo nani???Mapenzi ni umalaya tosha,kuwa malaya kitandani ni ruksa na sio nje ya kitanda.kuwa malaya kwa Mmeo ni ruksa,si mmeo sasa usipompa umalaya wote utampa nani???Habari ndo hiyo


3.HARAKA MWIKO:UNAWAHI WAPI???
Wanawake wenye haraka huwa sio wengi,wanawake wengi wanafaulu hapa,na hii ni kwa sababu wanawake ni receivers mara nyingi.Inawachukua muda kufika Kibo na ni mpaka upate mtu mwenye uwezo huo.Kasheshe hapa ni wanaume!
Wanaume wengi ni very selfish,hawajali.Wao wana hamu,wakimaliza hamu zao wanalala,tena na kukoroma.Hawajui mwenzake alishafika kitonga au lah,yeye hana habari.Hii ni hatari sana kwa uhusiano wako.Siku mkeo akikumbana na wazee wa kusimamia kucha ujue umempoteza.Kuna watu wako bize,wanasimamia kucha kama wameajiriwa Rasilimali kiuno.Sasa wewe akija kwako unajipimia mwenyewe halafu yeye unamuacha hewani,usimlaumu kamwe akicheat,maana wewe umepewa kazi imekushinda,kama kuna mtu anaifanya perfectly afanyeje??


Lakini je,na wewe mwanamke unamueleza huyo mmeo kama yeye ni selfish???Usikurupuke na kumwambia wewe ni selfish na hunifikishi,wanaume huwa hawajisikii vizuri,tafuta njia nzuri ya kumfikishia ujumbe huu in a good way maana wengine hii shule imewapitia kando.Muelekeze,usiogope,huyo ni wako kwahiyo muonyeshe ngoma inachezwaje,akimaster wote mtafurahi.Tatizo la wanawake hawasemi,wanauchuna halafu wanatafuta option za nje....Hii ni mbaya....Na wanaume wengi mkiambiwa mnanuna,sasa unanuna nini,kama humfikishi unataka amwambie nani zaidi yako wewe???Mkiambiwa muelewe na mtafute njia za kuweza kuwafikisha wake zenu lasivyo msilaumu mkisaidiwa!

Dakika 5 Mwanaume tayari ushaamsha Mashabiki,unawahi wapi???Unakimbilia wapi???Kwa Mwanaume Kama kushuka utashuka tu,msubiri mama ajipimie visoda vya kutosha,Dance with her na Shuka pale tu mama akikuruhusu kushuka lasivyo ni Mwiko kwa Mwanaume kushuka kama hujapewa Green Light kutoka kwenye Traffic Lights za mkeo ushuke,lasivyo utavuka mataa na Red lights na hiyo ni Traffic Offense...Unawahi wapi?????Utapata ajali bure kwa haraka haraka zako!

4.COMMUNICATION ON BED IS POWER
Kwakweli hili ndio tatizo kubwa.Mshafika ngome,mnacheza ngoma...cha ajabu eti kuna watu hawaongei kabisa...Sasa utajuaje mwenzio anataka nini na amefika wapi,na ufanye nini ili awasili??


Msiishi kama mabubu...ONGEENI! Na kama mlikuwa hamuongei anza leo itakusaidia sana sana...Kuongea kutawafanya mfike pale ambapo hamjawahi kufika....Kuongea kutamfanya Mwanamke akupe instructions kwamba uguse wapi ambako yeye anakunika....Kwenye Mapenzi,mwenye mtihani zaidi ni Mwanamke ambaye hadi afike kileleni ni ishu,msaidie yeye zaidi kwa kumpa nafasi ya kucommunicate nawe....TRUST ME,ukimruhusu Mwanamke acommunicate na wewe utaona changes...Atakwambia kila kitu,na utaenjoy.


Build a better relationship,Mfanye Mmeo/Mkeo ajisikie raha ukimuita Ngome,maana wengine Ngome Kongwe pamekuwa eneo la mateso,hawaoni raha ya Mapenzi maana ukifika wewe huna ushirikiano zaidi ya kujifikiria wewe na hamu zako au kwenda pale kumridhisha tu fulani ila sio wote kufaidi.


Raha ya Mapenzi ni wote kutoka pale mkiwa mnasema YESSSSS,This was the game,na sio mmoja anachekelea na mwingine anatoka kama alivyoingia,Huo ni Uonevu wa Kijinsia.


Kwa leo tuishie hapa!

Monday, July 23, 2012

DALILI 7 ZA MWANAMKE GOLD DIGGER...ANAENJOY HELA YAKO TU NA SIO PENZI LAKO


Thursday, July 19, 2012

UKITENDWA NA MTU ULIYEMPENDA FANYA HAYA

Karibu kila mmoja wetu ametendwa,kwa namna moja au nyingine..Ni wachache sana ambao waliingia kwenye Mapenzi na wakafanikiwa kuoana na hao wapenzi wao bila kuhama baada ya kuumizwa na First Lover wake...Ila wengi tushahama nyumba kama 8(kadirio la chini) ndo kufikia hapo tulipo sasa

Uhamaji huu ni kwa sababu wale tunaowapenda,aidha hawatupendi in a same way,au wanajikuta wao wanatuhama,na hivyo inabidi tutafute nyumba nyingine ya kutusitiri...This is an on-going process,kila siku ya Mungu ipitayo,kuna Break ups,watu wanalia na kulia,kisha wanarudia tena...Ama kwa hakika Mapenzi ni machungu lakini watu wanayapenda no matter what...We keep on playing the Love Game despite of pains we get in the game...ila tutafanyaje sasa...Homoni ziko bize!

Wengi tulioumizwa na wapenzi wetu,wengine hatujaweza kusahau machungu ya First Men wetu...Thats true...Umempenda,ukamkabidhi bikira yako tukufu,jamaa akalikoroga,ukaachwa mataa ya Buguruni unashangaa..Unaishia kuwachukia wanaume...Haisaidii

Wale wanaume waliojitoa Mhanga,unampenda Mwanamke,unamzimikia(ambacho ni nadra sana Mwanaume kufanya),unamsomesha,unaingia gharama ukijua huyu ndio mkeo mtarajiwa,GHAFLA,linatokea jamaa kwa ulaini kabisa,linamwaga sumu baharini,Samaki wooooteee wanakufa...Huamini,umetumia gharama zote,na mahaba yote uliyompa kwa kujiminya kwelikweli,Sacrifice,hata babako hujawahi kumnunulia Batiki ili Mpenzi wako awe Clasic,jamaa kampitia fasta...Na demu anasepa huku anamwaga shombo kwamba HUJUI MAPENZI!Tusi kubwa sana kumwambia Mwanaume hili,atakuchukia milele,anaweza kukata roho huku anatukana jina lako.Umechukia wanawake,umeamua kuwakomesha,umekuwa Player,unawachezea na kuwaumiza wanawake kwa sababu ya Mwanamke mmoja aliyetibua nyongo,HAISAIDII!Na wala haitamaliza ile hasira,Kiu ya kuumiza itabakia palepale,hata uchezee wanawake 1000,atabakia moyoni tu!

SASA UFANYE NINI PALE UMPENDAYE SANA ANAPOKUUMIZA????

1.SAMEHE

Ngumu!Kila mtu anaguna aaargh,mi siwezi kumsamehe huyu Mwanaume,nimetoa Mimba zake 3 na bado kaniacha hana Shukrani!Hata ukimchukia ameshaenda,na ukimchukia hakutabadili zile mimba 3 ulizotoa ziwe watoto.Kumchukia kwako kunaufanya moyo wako uwe na Kinyongo,na hata ukikutana na Mr Right Man bado utakuwa na particles za woga na hasira,UTASHINDWA KUPENDA kwa moyo,kwa hofu ya kuumia...Dawa ni kumuachilia na kumtoa moyoni kwanza,hii itakufungulia mlango wewe kurudi kwenye Neutral Zone,ili Moyo wako uwe at ease,na love iendelee kuflow,lasivyo,utapishana na Muujiza wako wa Mme kisa una hasira ya jitu ambalo liko huko linakula zake raha,wewe huku unaendelea kuwa mtumwa wa Past.KAMWE,usiwe mtumwa wa Past,its gone,and you should move on!Hilo lilipita ili ujifunze kwamba wapo wa dizaini hiyo!

2.KUWA MAKINI KWENYE SELECTION

Usirudie kosa lile lile.Fanya screening ya kutosha(sio kama ya Questionnaire though),kama nia yako ni kuwa na uhusiano imara,kuna mambo ya kufanya.know the person better,familia yake,jua nia yake thabiti kwenye uhusiano huo,do some little test za kuprove kwamba he/she worthy it...ila isiwe too much...kuna tests huwa zinapiss off,unaweza kumpa mtu test akasepa,japo alikwa na nia...Ifanye kwa busara,usikimbilie tu mahusiano,ila kama unapass time,ize tu...Strong Relationships are built by Strong people...Jua level yake ya wivu,how anasolve matatizo yakitokea,ili ujue how to deal with taht person...Maana matatizo yapo tu,na wivu upo...jua Jealous level,jua Problem Solving mechanism yake...Ili yakitokea uhue fate.Kama ni mtu wa kupiga,au Mnunanji,Je,Uko tayari kuface Mnuno wa mwezi???Kama uko fit poa,go for it.Kama hauko fit usiforce,hata awe handsome au Gorgeous namna gani.Ndoa ni kimeo cha Milele,kuna vitu they look simple but in long run,they are so complicated....Msimamo wake wa Kiimani pia ukoje????Hili watu wanali-overlook sana,ila ni CRITICAL....Wote ni dini moja???Au mmoja Musilamu wewe Mkristo??Can u make it????Msichukulie poa tu,Tofauti za kidini mnaweza msione madhara yake ila ni msala...Watoto wakizaliwa ndo mtaona kazi,Wakwe watakuja juu,aitwe Asha au Neema,ndo utaona kazi..mtoto asali Msikiti wa Bin Jumaa au Lutheran Mbagala???THINK TWICE!

3.FALL IN LOVE
Baada ya choice kufanyika kwa umakini na una uhakika na mtu,Please FALL! Usianze maswali,sijui huyu atakuwa kama yuleeeee???Ah ah...ukianza questions tu,moyo wako hautafunga completely.Maadam umefanya Screening kwa uhakika,na kwa muda wa kutosha,na umesema huyu ndiye,basi FALL!

Ni balaa kushindwa kufall eti kisa uliumizwa nyuma,si nzuri kabisa...utajikuta kosa kidogo unakimbilia Break Up maana BREAK UP kwako ndio SAFETY ZONE.Hii sio njema.Umemchagua mwenyewe,Give Him/Her your all,and allow Him/Her to give asilimia zote za mapenzi kwako

4.TALK ABOUT YOUR RELATIONSHIP SO OFTEN AND CARE FOR MEMORIES

Ni vizuri kuongelea wapi mmetoka na wapi mnakwenda....Mara kwa mara ongeleeni how mmekutana,ilikuwaje...ingekuwaje kama msingekutana pale..Share how you feel for having him/her...Muonyeshe kwamba yeye ni wa thamani na ameleta mabadiliko kwako///

Kumbukeni Anniversary ya uhusiano wenu hata kama hamjaoana....Kama mlikutana April 15 kwa mfano,.Mnaweza kuwa mnakumbushana Kila Tarehe 15 ya mwezi kwamba mmetimiza miezi 6,au miezi 7...It shows kwamba ur happy with the relation...Lakini Pili,it shows kwamba you are going somewhere and you cherish the journey....

Trust me,This works...Hakuna ujanja mwingine wa kuwa na Penzi imara zaidi ya kulipenda penzi lenu kwanza....Epukeni maneno ya watu...Wakiona mnapendana wataanza chokochoko,utasikia maneno kuhusu Mpenzi wako...Mara hivi mara vile....Msiwajali,as long as nyie wenyewe wawili mnajua nini mnafanya na mnaaminiana,TRUST IS EVERYTHING...Kamwe msipoteze TRUST....Mkipoteza tu,amini amini nawaambieni,Mahaba yenu yatazama hapo KISIWA CHA CHUMBE!

Kwa leo inatosha!

Friday, July 13, 2012

USICHUKUE USHAURI WA KIFEDHA KUTOKA WATU WALIOFULIA...DONT TAKE FINANCIAL ADVICE FROM BROKE PEOPLE

Tangu lini Matonya ombaomba atamshauri Manji ajenge ghorofa Samora Avenue??Sanasana atamwambia ghorofa litaanguka blaza bora ufuge ng'ombe hata akiumwa utachinja ule nyama...Narrow thinkers will always give you Narrow Ideas.

 Do not take Financial Advice from Broke people!We unadhani watakushauri nini???Mawazo yao yamefungwa kwenye umaskini,hawaoni opportunities hata zinazopita kwenye Kope za macho... yao,kamwe usiombe ushauri watu hawa,wamefulia kuanzia Mfukoni hadi mawazoni.Ni waoga,na usidhani mtu mwoga atakushauri kitu cha kijasiri.

 Ni sawa na mtu aliyeachika kwenye Ndoa awe ndo Kungwi wako wa kitchen Party,Jiandae kwa talaka tu ndugu yangu!Watu wengi wameshindwa kujikwamua kwenye umaskini kwa sababu tu wameomba ushauri kutoka kwa Wrong people........
Wahenga walisema Ukitaka kunukia waridi kaa na waridi,ukitaka Mafanikio ongea na watu waliofanikiwa,hao wanazo mbinu za kukufikisha mahali ambako wao wamefika.Division 0 akikufundisha wewe mbinu za kufaulu basi usitegemee utapata Division 1,jiandae kupata Division Negative,kama ipo!
 
Watu wengi wana mawazo yenye thamani ya GOLD,wanaenda kushea mawazo hayo kwa watu wenye thamani ya Madini ya Ulanga....There will be no added Value...Gold should stay with Gold because its more valuable....Labda Ulanga uje kwa Gold ili uongezewe thamani,and not vice versa.
 
Your finacial Breakthrough itategemea na aina ya watu unaowakaribisha katika maisha yako,hawa wana-kuaffect kwa namna moja au nyingine...Kama wewe hutawaaffect wao,basi watakuaffect tu....Wataua ndoto zako kubwa kwa sababu wao hawana ndoto kabisa au ndoto zao ni za kitoto.
 
Amua leo,Je,una ndoto kubwa ya ku-achieve???Look for the right people to nourish it....Sit down with them,watakuonyesha njia
 
Ukiendelea kukaa na hao wasio na msaada utabakia hapohapo na usipoangalia utaanguka kabisa.
 
UAMUZI NI WAKO!

Tuesday, July 10, 2012

NO LOVE WITHOUT TRUST...JINSI YA KURUDISHA IMANI ILIYOPOTEA KWA MPENZI WAKO

No Trust No Love...


Penzi bila Kuaminiana ni sawa na Kuku asiye na Firigisi,bei rahisi sana aisee...


And when the trust is lost,si rahisi kuirudisha...Relationship nyingi zilizoishiwa Trust hufa kibudu,chache sana zimeweza kuibuka tena baada ya kazi ngumu na shughuli pevu sana.


Kuna sababu nyingi sana huua Trust among Lovers...Wengine wamefumania Wapenzi wao red-handed kitandani au gheto anauza Share bila ruhusa ya Menejimenti...Wakakosa pozi,wakalia,wakadhani wamesamehe lakini inawauma sana,kila wakikumbuka kile kitendo wanahisi things will never come back to normal...


Wengine wamekuta Meseji kutoka kwa Wanaume/Wanawake wengine kwenye Simu za wapenzi wao,ikawaua nguvu....Hakuna Cheating rahisi,na Wameshindwa kuwaamini tena no matter how many months have passed....


Inataka moyo sana kujikakamua na kurudi Mwanzoooo...Kama hakuna kilichotokea,wengi hawawezagi kurudi pale....Inataka Moyo! Wengine wanajikuta wanalipiza kwa kutafuta kidumu,kama alifanya basi atafanya tena,aah ngoja na mimi nitafute cha kwangu ili twende sawa...KOSA! Akigundua,there will never be a relation, it will die completely

FANYA HAYA KURUDISHA TRUST ILIYOPOTEA

1.Admit

Ukikumbana na kimeo,hakuna kujifanya wewe mjuaji,ADMIT kosa..Kama akiamua kukusamehe,asamehe,akiamua kukuacha akuache....Ukijifanya kidume kukataa kosa kumbe mwenzio anajua kila kilichotokea,atakaa kimya na atakulipizia in a place hutaamini. Hakuna ujanja kwenye hili,if you are in love with that person,show that ur regreting and you need to change!

Ubishi unaonyesha kwamba ulichofanya ni kawaida,na kwako sio kosa na haikuumi,and thats bad

2.Be Open and Honest

Baada ya kimeo kutokea,umeshaadmit you were wrong...Kifuatacho ni kumuonyesha kwamba kweli umedhamiria kutokurudia kosa

Ule uwazi ambao mwanzo haukuwepo,hapa ndio mahala pake....Kuwa muwazi,usiwe na hidden issues,hidden agendas ambazo kwa namna moja au nyingine ita-trigger Mawazo kwamba kuna mambo bado unafanya kwa siri.

Ratiba zako ziwe wazi,wapi ulipo,unafanya nini...Na usisubiri kuulizwa ukipo,ifanye iwe daily habit,ukizoea utaona rahisi,ukisubiri uulizwe utahisi uko Misri utumwani

Mfanye akuone wa tofauti kwa kuwa muwazi...Itamsaidia kupona na kusahau lililotokea.Ukijifanya Hero kuendelea kuficha,kile kidonda hakitapona!

3.Act Differently to heal Him/Her

Kila kilichokuwa kikwazo mwanzo jaribu kukirekebisha.Haina ujanja,ndo ushaharibu,lazima ufanye kazi kubwa sana kurudisha upya....Na usihisi kama ni mzigo maana umejitafutia,umejenga na ukabomoa mwenyewe,so ni kazi yako kujenga tena.

Mtoe out kadri uwezavyo,Talk openly,Mshirikishe ratiba zako,Plan zako na kila kitu,ajihisi upya na kwamba sasa ur TOGETHER....Mfanye akuone mpya this time.

Ukifanya haya,ni kweli itachukua muda maana TRUST iliyopotea ni ngumu sana kurudi maana shetani ni yuleyule,kabadilika manyoya tu...Ni ngumu ila ukiinvest enough time and energy utaweza lasivyo be ready for a Bye Bye Kiss!

Friday, July 6, 2012

AUNT EZEKIEL AFUNGA NDOA KIMYAKIMYA DUBAI

Msanii Maarufu wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel ameripotiwa kufunga ndoa na Mchumba wake ajulikanaye kama Sunday Dimonte nchini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE)Ndoa hii inaripotiwa kufungwa June 17, wiki 2 tu zilizopita.

Habari zinadai kuwa, Aunt alifikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kumwambia hawezi kuvumilia umbali uliopo kati ya Tanzania na Dubai hali ambayo Aunt alihofia kupigwa chini.

Waandishi walimsaka Aunt kwa njia ya simu ya kiganjani akiwa Dubai, alipopatikana na kuulizwa kama kweli amepigwa pingu za maisha, alifunguka:
“Ni kweli nimefunga ndoa huku Dubai lakini nimesikiasikia kuna watu wanasema nilifanya siri. Siyo siri, ila huku ni mbali na huko nyumbani Tanzani, isingekuwa rahisi kuita watu wangu wa karibu.”
Paparazi: Kwa hiyo ndiyo imetoka hiyo?
Aunt: Hapana, nitakaporudi nyumbani nitafanya sherehe, nitaalika watu, hata wewe, tena itabidi unichangie jamani.

Ngoja tuone akirudi itakuwaje.Kama ni kweli, Aunt Ezekiel atakuwa amejiunga na wasanii wengine wa Bongo movie waliowahi kufunga ndoa kama Irene Uwoya na Wastara.


Tunaomba iwe hivyo!

HABARI KWA HISANI YA RAFIKI YANGU JOHN KIANDIKA

Thursday, July 5, 2012

SABABU 3 KUU KWANINI WANAUME HAWATAKI KUOA

Dunia imechange sana...Zamani Mwanaume kufika miaka 30 hajaoa ilikuwa hatari,mwiko kwanza maana wazazi na ukoo wote watakukalia kooni..Ila siku hizi,aaah,watu hawana habari,wanatafuta watoto tu kwa kuzalisha Wanawake wa watu halafu basi...Hawataki kabisa Commitment.

Inaonekana kama ni Lifestyle ambayo ilianza mdogo mdogo,ikapenetrate,na ni kama inaanza kukubalika maana ongezeko la Wanadafada kuzaa tu bila mpangilio,bila ndoa linakuwa kubwa sana,na kwao inakuwa Simple tu,yaani Freshhh...

Kwa kutambua hili,Wadada hawana habari...Wanasema kuolewa ni utumwa,heri wazae.....Na Wanaume nao wanasema kuoa mh mh,bora wapate mtoto walee,ila kuweka mtu ndani ah ah,kimeo.

Feeling zote 2 zimegongana,na zimeshabihiana halafu zikakubaliana,bila kuwa na majadiliano yoyote...Imetokea tu...

Kila jambo lina Origin...Kuna chanzo...Kwanini hali hii itokee siku hizi tu,ni utandawazi...Ni mabadiliko ya Tabia nchi...Ni nini haswa???

Lazima kuna jambo...

Source iliyosababisha inaonekana ni Wanaume....Wanaume wanaonekana hawapendi kuoa siku hizi,lakini kwanini wasioe...Why siku hizi na Sio zamani ambapo ilikuwa ni fahari kwa mwanaume kuoa...Miaka 20 mtu ameoa na Watoto juu...Ila siku hizi walaaaa...

Hata Wanaume hawakupenda,ila kuna sababu zimesababisha wasipende kuoa....Kuoa ni a very nice Feeling lakini kuna vitu Wanaume hawataki na ndo maana hawaoi....

Leo tuangalie SABABU 3 ambazo zinawafanya wanaume WAPOTEZE HAMU YA KUOA

1.1961 REASON...ITS ALL ABOUT UHURU
Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961!
Hamna kitu Wanaume wanapenda kama UHURU
If una boyfriend,na unafanya mambo ya kumnyima uhuru,asilimia za huyo jamaa kukuoa ni 0.01%,Trust me!

Kama the best u can give ur man is Harassment....Questions kibaooooooo....Kumpangia ratiba zako ili yeye afit aache mambo yake,na kila siku unataka priority,SAHAU NDOA!
Ukikutana nae tu umekimbilia simu,huyu nani kakutext,mara huyu si nlishakukataza kuchat nae..Khaa!!

Uliza walioolewa walifaulu vipi huu mtihani,huu ni kama Mtihani wa Hesabu kwa Mwanafunzi wa Form 4,ukifaulu huu,umejiwekea hazina,trust me! Mpe mwanaume uhuru kwanza then ndo uongee mambo mengine,hapo mtasikilizana na hata ratiba zako zitafit kwenye uhuru wake,Dont try to put urself as the Most Important,ul loose! Akisema anaenda kuwatch mpira we unamwambia arudi home mwangalie movie,what the heck?Why movie na sio Football anayopenda???Sawa kuwatch movie sio dhambi lakini kwanini ugonganishe ratiba na unajua anapenda mpira?Hapa unampa definition kwamba unakuwa dominant na hakuna kitu kibaya na sumu kama wewe kujaribu kuwa Dominant,unajifanya Transformer..Dont be this kind of a Girl,He will end up being a Boyfriend,and He will never move a step ahead,akimove ujue Kibuti!

2.WANAWAKE MIMI-TYPE
Aina ya wanawake wanaojifikiria wao tu...Baby naomba mtaji wa Maembe..Baby naomba mtaji wa Mabungo...Baby nataka kuanzisha biashara ya Nguo na Vipodozi....Why cant you say baby,kutegemea mshahara sio vizuri kwanini TUSIANZISHE BIASHARA ambayo ITATUINGIZIA KIPATO EXTRA....Unaona utofauti????Collective statements..onyesha kwamba na yeye ni Inclusive.Sio MIMI this MIMI that....Be the kind of a Woman who gives an idea...Make sure he understands it...And ensure he takes it further and Control its implementation

Tangu uanze uhusiano wako na huyo Mwanaume umewahi kumshauri kitu gani ambacho siku akitaka kukumwaga atasema dah This girl did this Let me be considerate,Kipo kweli,halafu unataka ndoa????Sio idea za kununua Soksi na Boxer,Idea constructive ambazo zilichange maisha yake...HAKUNA! Sasa nani akuoe??

3. MWANAMKE DIVIDER
Aina hii ya Wanawake ni wale ambao wanaingia kwenye Maisha ya Mwanaume fulani halafu wanataka wawe kama MD hivi...Wamemkuta jamaa ana Marafiki zake,Mabesti kweli,wametoka mbali na huyo Mwanaume hujui wamemtoa wapi,wamemsaidiaje hadi hapo alipo....anaanza kutoa Opinions kuhusu hao watu...Fulani achana nae namuona kama hana lolote....Hivi Fulani anakusaidia nn...Halafu flani simpendi anaongea kweli...Hapo jua ushachemka....

Hamna vita ngumu kama vita ya kumchagulia Boy wako Marafiki na kujifanya HR una-screen uliowakuta eti wewe huwapendi...Huwezi shinda hiyo Vita I guarantee you,na ukiona umeishinda jua kuna kimeo mbele

Ukishinda hiyo vita na uhusiano wako utakuwa chali,unless huyo Mwanaume awe Bushoke type ambaye hana msimamo lakini siku zote ukipigana na Mashemeji ambao ni Close friends wa Jamaa YOU WILL LOOSE

When it comes to Men,Marafiki are more than Parents.They know kila kitu hadi ambavyo wazazi wake hawajui,na si ajabu hata uwepo wako kwenye maisha yake walichangia mawazo na kukuscreen kabla,na kumshauri akuchukue,lazima aliask opinion...Sasa umeingia unajifanya HR,wanaku-Ulimboka fasta utashangaa.

Wednesday, July 4, 2012

KUNA STAA ANAMWAGA HELA KWENYE TWITTER...PLEASE FOLLOW HIM AND GET SOME CASH
Huyu jamaa amezaliwa akiitwa Michael Collins Ajere


Mwaka huu ametajwa kama Mmoja wa Celebrity mwenye Nguvu Africa akishika namba 36(The 36th Most Powerful Celebrity in Africa)


Amezaliwa November 26 mwaka 1982 na yuko kwenye Industry ya muziki.

Wengi wanamfahamu kwa jina la Don Jazzy


Ni producer maarufu sana nchini Nigeria na Duniani kote akiwa ameshiriki kumuweka mwanamuziki D'BANJ hapo unapomuona leo hadi kuchukuliwa na Kanye West.Actually D'BANJ  na DON JAZZY ni childhood friends,wamecheza na kukua pamoja hadi kufika kufanya kazi na kupata mafanikio waliyonayo leo!


Don Jazzy ndo ametengeneza Album 2 ziliyomtambulisha D'BANJ, Tongolo mwaka 2004 na No long Thing mwaka 2005 akiwa na lebo ya Mo Hits Records na swahiba wake D'BANJ.


Mwezi May, 2012 baada ya D'BANJ kujitoa Mo Hits records na kwenda kufanya kazi na Kanye west, Don Jazzy alianzisha Record Label inayoitwa MAVIN RECORDS.Don Jazzy ameshatengeneza kazi za watu wengi tu maarufu akiwemo NAETO C ambaye ana nyimbo kama TEN OVER TEN na 5&6, TIWA SAVAGE mwenye hit songs kama KELE KELE na LOVE ME LOVE ME,lakini kali kuliko ni kutengeneza wimbo wa JAY Z na KANYE WEST kwenye Album yao ya WATCH THE THRONE uitwao LIFT OFF Ft Beyonce.


Huyu sio Producer wa kawaida na naona hela zimeanza kumpelekesha,jamaa anamwaga hela kwenye Twitter


Follow him kwenye TWITTER @DONJAZZY,kama una shida ya hela atakwambia umtumie akaunti yako na anakutumia mkwanja on the spot.Its not a joke,cheki hapa chini baadhi ya watu aliokuwa akiwasiliana nao na wakimshukuru baada ya kupokea mkwanja from him.Hes definitely very generous.Wabongo kazi kwenu! CHEKI TWEET ZAKE ZA KUGAWA HELA WIKI HII NA WATU WAKISHUKURU BAADA YA KUPOKEA DON JAZZY MWENYEWE


Moja ya Kolabo za ukweli alizotengeneza ni hii hapa chini ambayo aliwaweka pamoja D'BANJ na mkongwe SNOOP DOGGY DOGG kwenye Wimbo unaoitwa MR ENDOWED


Tuesday, July 3, 2012

KUFELI SIO MWISHO WA MAISHA....THERE IS LIFE AFTER FAILURE,GOD HAS A MASTERPLAN OF UR LIFE

Kila kitu kinatokea duniani kwa sababu maalum,aidha kukufundisha au kukufanya uelewe zaidi jinsi ya kuishi vizuri ukiwa duniani.Failure ni kama kujikwaa,unapaswa unyanyuke na kujifuta vumbi na kuendelea na safari.Kulala chini baada ya kujikwaa na kuanza kulialia hakutakufanya ufike ulikoplan kwenda.

 Ukifeli mtihani sio mwisho wa maisha,nafahamu watu waliofeli ambao wako very successful kuliko mimi....There is life even after failure.
 
Kupigwa sana vibuti na watu unaowapenda haimaanishi hutaoa au kuolewa,Mungu anajua who is the right partner for you,hao walioondoka hawakuwa type yako na usiforce wawe type yako coz hawatakuwa.

 Usimlazimishe Mungu akupe mke au mume wa rangi nyekundu wakati anajua kwamba wewe unahitaji wa rangi ya kijani ili uwe Complete.

 Ulimwengu huu haujiendeshi,aliyeucreate ni Mungu,aliyekucreate wewe ni Mungu,na anajua who is the best partner for you.
 
Ukiachwa na umpendaye shukuru maana unajua yupo aliyeandikwa kwa ajili yako utampata na atakuwa perfect,ukienda kwa feeling ya unachopenda wewe utaibuka na mme na mke mdosho feki kutoka China.
 

UKITAKA KUUA PENZI LAKO FANYA HAYA HAPA,FASTA TU

Ukitaka kufa mwakani unatakiwa kufanya mambo flani ya hovyo hovyo mwaka huu,utakufa tu..

Ukimeza dawa ya sumu usitegemee itageuka kuwa ARV,itakuua tu

Kuna aina flani ya watu wanapenda sana kujitafutia matatizo,wakiwa In love huwa wanajaribu kuwa too much,kwa vitu ambavyo sio vya msingi hata na havimuongezei lolote zaidi ya matatizo.

Kuna vitu ukifanya unajua kabisa kwamba vitakusaidia kupalilia penzi lako,kuliwekea mbolea ili likue zaidi...Concentrate kufanya hivyo

Ila kuna watu huwa wana-opt kufanya mambo ambayo yanawaua wao wenyewe na mwisho wa siku huishia kujuta tu.

Baadhi ya Mambo ambayo yameua mahusiano mengi sana na yanaendela kuua hata leo,na hata kesho yataua ni haya yafuatayo,Chonde chonde usifanye haya maana huwezi jua Damage ambayo yanafanya kwenye uhusiano wako:

1.MISTRUST

Sifa moja ya Penzi imara ni lile ambalo mnaaminiana...Mtu anaweza kuaga kwenda home na ukajua anaenda home kweli bila kuwa na chembe ya shaka kwamba atachepuka na kufanya Call Diversion.Ukiona penzi ambalo halina Trust,hilo penzi liko ICU na litakata Roho muda wowote.Hamtafika popote. Mistrust huwa haiji hivihivi,huwa ni zao la mambo mengi yaliyotokea ambayo yamemfanya mmoja kati ya wapenzi kupunguza imani na mwingine.Dawa ni kuhakikisha mnamaintain highest level of Trust at all time.Na moja ya njia rahisi sana ya kurudisha trust iliyopotea ni kuwa wawazi...Wawazi kwenye ratiba zenu za kila siku..Thats through Communication..Hakikisheni mna communication  muda wote,ifanyeni kuwa ratiba na sio utumwa,itawasaidia kuwa in touch na kila mmoja atajua ratiba ya mwenzie na kuwa at peace

2.EPUKA U-SPY

Kwenye Mapenzi hakutakiwi kuwa na mtu yeyote aliyesomea CCP Moshi...Hiki ni chuo cha mapolisi na maspy wa usalama wa taifa....Mapenzi ni eneo huru ambalo kila mmoja anapaswa kuwa huru....Sio mpenzi kaacha simu tayari umekwapua...Kuna vitu haviko kwenye Katiba ya Muungano...Simu ya Mtu ni personal property yake..Dont sneek,dont Spy...Ukimuomba simu kuitumia kupiga au kutext usijifanye spy na kuchungulia Inbox..Akigundua atakumind na itakuwa big issue...uhuru wa mtu binafsi uheshimiwe,haikusaidii lolote sanasana utakumbana na vitu ambavyo hutapenda utaishia kununa na kumbe hujavielewa..We are so different,mahusiano yangu na watu wangu niliozoeana nao ni tofauti na wewe...U can see messages na ukadhani ni za cheating kumbe ni kawaida...Stay safe...Dont be a police...Dont Spy,hata uwe tempted namna gani..hii imewacost wengi sana,BEWARE

3.EPUKA UBIZE

Ubize ni msala.Ukikubali kuwa mpenzi wa mtu jua kuna uhuru unapoteza...Japo uhuru kidogo...Mpenzi wako anakuwa priority na ni jukumu lako kuhakikisha anapata Attention....

Ndio unasoma lakini una mpenzi,dont replace him/her with books

Ndio unafanya kazi,una vikao,na assignments,na presentations,na warsha,na kila kitu ILA,una Mpenzi...Dont replace him/her with ur job...Kama huwezi kumanage Shule na Mpenzi....Kazi na Mpenzi....Chonde nakusihi,BE SINGLE,lasivyo utazingua tu mtu wa watu,atafeel hapendwi...hajaliwi..Atacheat,...na wala usimlaumu maana wakati ukiwa bize na mshule wako na mkazi wako,kuna mtu alikuwa na kazi na alimjali...Swali kwake ni Je,kwann huyu ameweza and my Boy ameshindwa???USIMLAUMU LIKITOKEA HILO,kosa ni lako 100%

4.EPUKA EXPECTATIONS

Kuna watu hawana simile...Dakika 2 tu nyingi wamewaza Mbinguni...

Mapenzi yanataka Patience....Anzeni mapenzi vizuri...Know him/her.....Jadili mustakabali wenu pamoja,akupe views zake....Then kama kuna kitu cha kuwasongesha mbele kila mmoja aseme/....Kama kuna vikwazo vya kusonga mbele kwenye hatua kubwa zaidi kama Ndoa mathalani,viwekwe wazi

Ni jambo liko wazi,kuna watu ni wazuri kuwa wapenzi tu lakini sio waume....Kuna watu wanafit kuwa Girlfriends tu lakini sio Wife material....Thats the naked truth

Mtu huyu ukimforce awe mume au mke inakula kwako....

Ndoa ni Institution maalum kwa watu maalum kwa sababu maalum

Kama wewe sio Mtu Maalum usiingie kwenye hiyo Institution Maalum maana hutakuwa na sababu maalum

The point is,usiexpect makubwa katika muda mfupi...give yourselves time to see ile sababu maalum ya kuwaingiza kwenye jukumu maalum..mkiona maono yenu hayaoani kufika kule usiforce...
Hakuna sababu ya kuwa fancy wa Ndoa halafu mkae Mwaka 1 muachane,utakuwa umejichafulia CV bure wakati ungeweza kutulia ukapata the right guy or right woman

Dont be over-ambitious....Stay in ur lane and choose the best out of the rest

Monday, July 2, 2012

TABIA YA MTU NI KAMA SCREENSAVER

Habits are like Screensavers

Tabia ya mtu haijifichi.Atajitahidi kupretend tu kwa muda lakini ipo siku itajulikana tu rangi halisi.

Ni ujinga kuamini kinyonga ana rangi ya Kijani na ukaenda kusimulia watu halafu wamkute ana rangi ya Kijivu,mazingira ndio yanaset rangi yake.

Huwezi kutegemea kondakta wa Mwananyamala anyanyue kwapa lake kudai nauli halafu usubiri kama atanukia Perfume ya Isa Miyake,tegemea kikwapa kilichoenda Shule kitakachokupa Flu ya kukutosha wiki nzima.

 Ukitaka kujua tabia ya mtu,Mpe tu muda,hawezi kudanganya muda.Ni sawa na Msichana wa Kichaga,ataweka mikogo na Swaga zote lakini Mwisho wa siku lazima Tege lake la kufa mtu litaonekana tu,Miguu ya kichaga haiongopi,Mchaga asiye na tege labda amezaliwa Thailand

SIHITAJI MARAFIKI...ANAITWA FID Q...VINA VYA HATARI


Tangu ameanza hii game,ameimari!

Huwa napenda kumsikiliza,maana huongea PURE SENSE...Vitu ambavyo hujawahi waza kuviwaza..

Brand new song,akimshirikisha Yvonne Mwale...Yvonne umeitendea haki hii ngoma,umeimba kwa Feeling kinoma

Nimependa Colour...Mashairi...The Way Fid Q amekuwa active kwenye hii Video,ameifeel yaani

Click hiyo http://www.youtube.com/watch?v=iMRtYxpWhuo ule ngoma safiii

Mike Tee amehusika pale kati kwenye Video hii...Na kazi nzuri kutoka TONGWE RECORDS kwa J'Rhyder

Hip Hop haiwezi kufa bana!

FID Q NA COCCA ALIPOKUJA TZ


FID Q AKIWARUSHA MASHABIKI