Friday, May 18, 2012

MAPENZI HAYAHITAJI UCHAWI,MCHAWI NI WEWE MWENYEWE

Hakuna haja ya kukimbilia Mapenzi,kama yapo yapo tu..Na huna haja ya kuogopa kumpoteza huyo uliyenaye,kwa mawazo kwamba akiondoka hutapata kama yeye..hapana...kama anakupenda hataondoka,na akiondoka basi utapata better replacement...hivyo ndo mapenzi yalivyo

Huna haja ya kutumia mbinu kulinda penzi,wengine hadi limbwata kwa Dokta ma-Mbwa mbwa ili kumlinda mpenzi asiibiwe,mapenzi hayana uchawi,mchawi ni wewe mwenyewe jinsi gani unavyojua kutumia ungo kupepeta na unavyoweza kuutumia kupaa nao pia

Ukimpenda mtu lakini ikashinikana basi shukuru maana huwezi jua Mungu amekuepusha na Jini gani ili akupe Malaika wa kukufaa maishani...Utang'ang'ania kibwengo na kukataa Malaika bila kujua

No comments:

Post a Comment