Social Icons

Featured Posts

Thursday, June 13, 2013

NYUMBA ANAYOISHI BILL GATES...HATARI,WEKA MBALI NA WATOTO


Wakati wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga na unawaza lini utaiba kazini au kujichanga kwa njia halali zisizotosha kuweza kuanza Ujenzi,hali ni tofauti kabisaaaaaa na ndugu anaitwa BILL GATES,ambaye ni tajiri namba 3 duniani akiwa nyuma ya Carlos Slim na Warren Buffet.

Yeye amehama kutoka kuishi nyumba za ardhini na ameamua kutengeneza nyumba baharini,katikati ya maji,Nyumba inayoelea....Hela iliyotumika kutengeneza HOME IN THE OCEAN inafikia Dola Bilioni 1.4 ambayo ni sawa na karibu trilioni 3 za Tanzania...trilioni 3 ni Bajeti ya Tanzani Kwa Mwaka mzima kwa Wizara zote za Serikali inayotoka mfukoni kwetu kabla ya Wahisani....Jamaa kaamua kutengeneza Yacht yenye Nyumba

Chukua Muda wako uangalie WATU WANAOISHI...Maana sisi wengine tupo tupo tu...

HAYA MZIGO HUU HAPA BOFYA http://www.youtube.com/watch?v=uBrCZs3_G9k

HISTORIA YA HUYU JAMAA KWA KIFUPI TU:

Amezaliwa mwaka 1955 huko Seattle,Marekani akiitwa William Henry Gates III,babake ni Attorney kwenye jiji la Seattle na Marehemu mama yake alikuwa Mwalimu tu wa kawaida wa shule

Alianza kupenda mambo ya Kompyuta na Programming akiwa na miaka 13 tu...

Mwaka 1973 alijiunga na chuo kikuu cha Havard na mwaka 1975 kabla tu ya kuhitimu Masomo aliacha chuo akaamua kuunda Microsoft Company akiwa na mshkaji wake Paul Allen.

KAZI NI KWAKO..UKIACHA CHUO KISA JAMAA ALIACHA INAKULA KWAKO

ANGALIA VIDEO HII...SIKILIZA MAUDHUI YA WIMBO HUU,UTAKUBALI KWAMBA CHRISTIAN BELLA NI RAISI WA MASAUTI

Kwa Wale Wapenzi wa Muziki wa Bendi nchini Tanzania,Jina la Christian Bella sio jina geni kwenu...Yes,anafahamika kama RAISI WA MASAUTI na ni mmoja kati ya Waimbaji ninaowakubali mno..He is very UniqueChristian Bella aliifanya Bendi ambayo haikuwa na jina lolote kuwa ON TOP kwa miaka yote aliyokaa pale...AKUDO....Kila mtu aliifahamu AKUDO na ilipata Wapenzi wengi sana hata kufikia hatua ya kutaka kuwapoteza kabisa kwenye ramani wapinzani wao wakuu waliokuwa wakishikilia chati, FM ACADEMIA.

Shukrani zimuendee rafiki yangu,Mtaalamu wa kutafuta Vipaji,King Dodoo kwa kumleta Christian Bella nchini Tanzania na kuisaidia sana Bendi hii kuwa kwenye Chati iliyo mpaka sasa...

Kwa sasa Christian Bella amehamishia makazi yake nchini SWEDEN na tangu alipokwenda huko amekuwa kimya na watu wakahoji kwanini na wengine kwenda mbali kufikia kudhani amekufa kisanii..LA HASHA....Simba hata azeeke namna gani hawezi kuwa nyau...Raisi wa Masauti amewadhihirishia Watanzania na mashabiki wake kwamba yuko fit baada ya kuachia Bonge moja la VIDEO alilofanyia Shooting STockholm,Sweden,na ukisikiliza maudhui ya Wimbo huu pamoja na Quality ya Video hii utakubali kwamba Christian Bella hana mpinzani na ndiye RAISI WA MASAUTI....PAmoja na kwenda nje hajawasahau wadau wake,amewarusha washkaji zake na mara kwa mara utasikia akimtaja Ustaadh Juma na Musoma kwenye wimbo huu unaoitwa MSALITI

Bonyeza Link hii uangalie Video yake mpya kabisa na utakubali Bella ni mkali wa wakali kwenye nyimbo za mahadhi ya Lingala ...Twende Kazi ...

BOFYA
http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=GytZVSdluF8#!

Sunday, February 3, 2013

UFANYE NINI UKIGUNDUA PENZI LAKO LIMEINGILIWA NA MTU NA BADO UNAMPENDA ANAYEKUCHEAT?

TUMA NENO SETH KWENDA 15678 NA UTAUNGANISHWA NA HUDUMA YANGU YA MOBILE AMBAYO ITAKUPA ZAIDI YA HAYA UNAYOYASOMA HUMU MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO KAMA SMS....

Leo naomba tudiscuss topic hii,maana naamini kama sio wewe yanakukuta haya basi ndugu yako wa karibu au rafiki yako analalamikia hili...

Imewahi kutokea unampenda mtu sana na mmekaa kwa muda flani mrefuuuu,halafu katikati ya safari unakuja kugundua kuna kidudu-mtu,whether ni Mwanaume au Ni Mwanamke ameingia kwenye Penzi lenu na umekuwa Shareholder kwenye Kampuni ya Mahaba Limited???

Huwa unafanyaje ukigundua Mahabuba wako anaibiwa namtu flani na wewe bado unampenda???

Je unasusa na kuamua kumuachia Kidudu-mtu ashinde Battle kiulaini???

Au unakomaa na Battle na kumfunza adabu kidudumtu hadi anaachia ngazi???

Unatumia ujanja gani kama ni Boy wako na unampenda,lakii mchizi amefall kwa kidudu-mtu na unakaribia kutoswa na Mchizi kisa kanogewa na Penzi jipya tam tam???

Maswali ni mengi lakini all in all,LEO nataka nikupe Mbinu tu ambazo zitakufanya upigane hiyo vita na USHINDE....Ukifuata haya,Probability ya wewe kushinda na kutunza Penzi lako ni 0.7%...

Mambo haya ni muhimu uyajue maana yanatokea kila siku,Kama bado hayajakukuta basi yatatokea,Kula Shule,siku yakikukumba basi unajua Mlango wa kupigia Bao...TWENDE KAZI:

1.INAWEZEKANA KOSA NI LAKO

Mara nyingi tukiwa kwenye Mapenzi tunajisahau sanaaaaaa,tunahisi tumemaliza,nishampata basi inatosha..Ubunifu sifuri,we mbuzi kagoma tu miezi mia 7,hujui kitu ingine..Chalii angu inakula kwako...Mwenzio akitoka anapigwa Jackie chan,Mission Impossible 6 na Kandahar....We upoupo tu unaegesha kama Parking ya Corner Bar.....INAKULA KWAKO

Jambo la kwanza,weka possibility kwamba moja ya sababu zilizomfanya jamaa/demu atoke ni WEWE...Usi-throw lawama kwake tu wakati kumbe na wewe si ajabu ulikuwa na mapungufu yaliyochangia...

2.KUWA MPOLE

Ukishaweka Possibility ya wewe kuwa moja ya sababu we kuwa mpole...Jipange kwa mbinu za Comeback kama Manchester...Ukifungwa huendi nyuma kuanza kulia,unajipanga na mashambulizi ya kusawazisha..hiyo ndo Battle....

Sasa wengine wanapanic,wanaanza kumtusi jamaa/demu,ooh we malaya sana,umekosa nini kwangu.....ipo siku atakujibu,nakosa nyamaaaa,we unanipikia maharage tu!Utafanyaje???

Kupanic hakusaidii,tena ukipanic ndo atahamia kule mazimaaaaaaa,utabakia unatokwa povu tu mwenzio anapewa mijiraha!Kuwa Mpole

3.TAFUTA TATIZO NI NINI ILI UJUE UNAINGIA NA SILAHA GANI

Huwezi kuua Nzi na AK 47...Jua adui ni nini uchague Zana ya kudeal nae...

Hii ni mtihani pia kwa sababu kwa Mwanaume anayecheat kufunguka kwamba ni nini haswa kilichomtoa ni ngumu sana.....Na tatizo lingine ni kwamba hata akisema utamchukuliaje??Wanawake hawapendagi kuambiwa ukweli na ukimwambia,hata kama ndo ukweli atanuna mbaya,ufudu haingii!Mnuno haswa!Anauliza halafu ananuna.....Hilo moja,Wanaume nao ni worse...Akiuliza nini kimekutoa ukamwambia,ah we unanipa goma dakika 5 wakati mwenzio anasimamaia Show ya Fally Ipupa saa nzima...duh,mtu mzima unahisi umekosewa heshima unamwagia makofi!HAISAIDII!
Ukiambiwa we Selfish dakika 5 chali,chukua kama Positive issue na ujifunze...Kama huwezi zaidi ya dakika 5 jifunze wenzio wanasimamiaje kucha...Mwanaume dakika 5 aibu jamani khaaa,Mchuchu anapandisha Kilima anapishana na wewe ndo unaserereka kwenye ganda la ndizi.....Aaaaaaa,sio kiivyo!

Ukipata Kiini cha tatizo BADILIKA!Akisema unalewa sana humpi haki yake BADILIKA...Akisema humpigii simu na Mwasiliano yamekuwa hafifu na huku kwa Bi Kidude anapigiwa mara 76 kwa siku,BADILIKA.....Hakuna jinsi,kama Blunder ushafanya,wajanja wamefill GAP,Pigana ili arudi kwako kwa kubadilika kwa kile alichosema.

Kasheshe ni pale unapoambiwa tatizo ukakasirika....Au kutojibiwa kiini cha tatizo,,,Kila Ukiuliza anasema ah niliamua tu...au imetokea tu..Hapo unalo,inabidi utafute mahali muafaka pa kumuuliza,na most probably muda mzuri ni akiwa anakanyaga kitonga,hapo utajibiwa yote maana hisia zinakuwa ziko juu...

4.FANYA ANAYOPEWA KULE NA ZAIDI

Hakuna kitu kizuri kama kumpa Mpenzi wako vyote ili akose vya kuomba nje!

Usiache hata tundu moja la kidudu kuingia na kusambaratisha.....Mpe Mawasiliano kwa Asilimia Zote.....Mpe Attention....Mpe hela ukiweza...Mpe Mahaba makali yenye Kungfu,Taekwondo na Kila kitu....

Hakuna Mwanaume atamuiba maana unapata vyote....Hakuna Mwanamke atampa lolote ambalo wewe hujui,Viuno vyote wavijua,Feni Mbovu Style,Feni nzima,Air Condition Moves,Mupeeee.....

Kama umegundua tatizo ni Mahaba uliyokuwa unampa badilika,kuwa mbunifu from NOW going forward...Si unampenda???Usijali kwamba kuna Competition,wewe fanya kwa nafasi yako....Mchoshe hadi akiwaza kuamka kwenda kule akute hana nguvu tena,atabaki kwako..Dozi Tu!

Baada ya muda utagundua amerejea,Kule alikoibwa hakuna Jipya tena,atabakia wako na utaishinda vita ILA,Jifanye bandidu,eti unamnunia kwanini kaenda kule....Au unamtafuta huyo Mwanaume Mpya au Mwanamke Mpya unaanza kumtukana,eti ooh ntakukomesha,unaiba vya watu,mara ooh ntakuloga uvae chupi usoni...ah wapi,unafeli....Dawa ya mwizi ni kumkimbiza kimyakimya,wala kelele hupigi,mwenyewe atahisi huyu niliyemuibia leo sio wa kawaida,ila makelele ya mwizi mara vile,wote mtaonekana wezi.....

KIMBIZA MWIZI KIMYAKIMYA....JIPANGE KIMYAKIMYA....SHAMBULIA KIMYAKIMYA
TUMA NENO SETH KWENDA 15678 NA UTAUNGANISHWA NA HUDUMA YANGU YA MOBILE AMBAYO ITAKUPA ZAIDI YA HAYA UNAYOYASOMA HUMU MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO KAMA SMS....

Tuesday, January 22, 2013

MAKOSA 6 HUTAKIWI KUFANYA UKIBREAK UP NA MTU,KAMA KWELI UMEMAANISHA

Haya haya hayaaaaaaa(kwa sauti ya Gossip Cop Soudy Brown)....Niko nalalaaa..Hapana!

Ni Muda mwingine wa kutiririka...

Lakini kama ilivyo Maombi kabla ya Chakula,basi niwaombe wale ambao bado hawajajiunga na Huduma yangu ya Simu Ya Mkononi-Seth Straight To Your Phone,please mfanye hivyo..
Ni rahisi tu,Chukua simu yako kisha tuma neno SETH kwenda 15678...As Simple As That! Please support your Boy,Your fellow Tanzanian....
Ukijiunga humo,I guarantee you and Your Love Life will never be the same! KARIBU!

Leo tuangalie issue zinazohusu Break Ups...Hili ni jambo baya sana kwenye Relationship kukutokea kama ulimaanisha..kuna watu hawamaanishi so hata wakibreak haiwaumizi hata kidogo,siku 2 tu yuko freeshiiii,anamingo kitaa!

Ngoja niongee na wale ambao mko kwenye Relationship...Wengine mlikuwa kwenye Relationship,mkapitia Break Up,mnajua inavyouma,na wengine tangu mmebreak Up mmeshindwa Kumove on kabisaaa..yeah,kabisa,najua mpo...Ntawapa dawa leo,mtapona tu...
Wengine Mmebreak up halafu mmesusa..mmenuna,hamtaki kusikia kitu kinaitwa Love...Huwezi kususia Mapenzi...Mapenzi ni kama Maji...Usipokunywa basi utayaoga,ukisusa utakuwa mtu wa ajabu na utajikuta unapata tabia za ajabu maana unashindana na Nature...

Leo naomba tuangalie makosa 6 ambayo Lovers huwa wanafanya pale inapotokea Wanabreak Up,kinachosababisha Maisha yao yashindwe kuendelea au yaendelee kwa Shida.Jitahidi sana kuyaepuka makosa haya:

1.KUMFUATILIA EX WAKO ANAFANYA NINI,NA NANI

Kama umeamua kwamba Its Over,Go on with your life...Usiendekeze Jealousy ya kipuuzi...Umeachwa/Kuacha unaanza kufuatilia maisha ya Ex wako,yatakusaidia nini???He/She is gone,and gone for good..jipange kuishi bila yeye,jipange ku-heal maumivu as fast as you can,na tabia hii ni contrary na MOVING ON Strategy...Moving On Strategy hairuhusu ubongo wako kuanza kupanga Mbinu za kuwa Paparazzi wa Ex wako...

Kuna watu ni mabingwa kwenye hii...Atafungua akaunti mpya ya Facebook aanze kumwangalia jamaa yuko na nani...Au ex wake anaendeleaje....Akiona yuko poa ataanza visa...Wengine huenda mbali na kuanza kumtafuta New Man wa Ex GF wake au New Woman wa ex BF wake..Una matatizo makubwa...Atamtukana,oh we mwanamke malaya,we mwanamke hivi..Hizo ni dalili za FRUSTRATIONS! Dont expose your frustrations over a Past which is History...jenga Historia mpya..Acha huu upupu,simama,sema its enough,songa mbele...itakusaidia...ukistuck kwenye kumfuatilia utaanza kujipa hopes kwamba maybe atarudi..maybe,Muda unaenda,hupati Partner wa maana maana kila anayekuja unampiga kalenda ukihope mchizi/mdada atarejea...HAJI NG'OO!

2.KUTUNZA MEMORIES MLIZOSHARE

Kuna watu wanatunza meseji nyie,balaa..Hata Makumbusho ya taifa pale Posta haiko deep kama wao.....Anatunza meseji za tangu unamtongoza mpaka mmeachana...khaa!nimewavulia kofia..Especially wanawake,ur best at this...nooomaaa!

Sasa mmeachana,unatunza zile meseji,unalialia chumbani,unafungua Archive Folder..unasoma Malavidavi ya zile siku zenu mlizokuwa Paradiso ya Mahaba...unalia weeee kama kengele ya Ibada...FOR WHAT???

Kama umekubali aondoke moyoni mwako,ondoa vitu vyote ambavyo ni temptations za kukuremind kuhusu yeye ili usije ukarudisha kivuli cha mtu moyoni....Wanawake ur so weak katika hili,mioyo yenu hugeuka Piriton hapa,mnanyong'onyea weeee,yaani mnahisi kama dunia imekuangukia...I cant live without Felix...Nani kasema wewe,Pumzi unayo,Moyo unao,Macho unayo mawili yanaona,Tafuta Replacement acha uboya! Huyo Felix akigundua unamlilia,miezi 7 baada ya kuachana anajionaje Mfalme...Anajionaje King wako,anaona YESSSS,demu analia mpaka leo kwa ajili yangu...Atakutesa,atakuburuza-buruza hisia zako kama Guta la Soko la Buguruni....Umeumbwa na moyo mzuri lakini atauburuza It will look like Shit....

Destroy Picha zote zinazokupa Nightmares....Album zake za nini???Gallery kwenye Simu weka mbali kule choma ikibidi kama zinakupa matatizo....Hakikisha kila kinachomuhusu kipo kwenye Recycle Bin na delete completely kusiwe na room ya ku-retrieve data!

Ukifanya hivi utaona jinsi anavyopotea taratibu,na baada ya muda itakuwa Historia.....Sasa wewe kumbatia weeeeee mapicha yake...Soma weeee mameseji aliyokuwa anakutumia na kuchat naye...Halafu unajiuliza,Hivi why I cant forget him????Ni sawa na kula halafu unauliza mbona tumbo limejaa...Tumia akili,Ni Maamuzi magumu lakini kama unaujali moyo wako ni lazima uyafanye or else kuwa mtumwa wa mtu asiye-exist kwenye maisha yako!

Lingine,Epuka kwenda sehemu ambazo wewe na EX wako mlikuwa mnaenda sana...Kama mlipenda kwenda KIJIJI Beach kama ndugu yangu Jumanne Mbepo,ukienda pale mwenyewe unajitafutia shida...Utaanza kukumbuka mliogelea wapi...mlikaa kiti gani na kadhalika....Potea kutoka kwenye hizo Memory Zone kwa muda mpaka utakapokuwa Sure kwamba hazikusumbui anymore!

3.MASHEMEJI ZAKO WA ZAMANI BADO UNAHANG NAO

Hii ndo yenyewe...Amlipokuwa wote alikutambulisha kwa washkaji zake..mkazoeana!Mmeachana lakini bado wewe unahang nao!

Hapa kuna trick!Sisemi uwachukie,Sisemi kwa sababu urafiki na Mapenzi yenu yamekufa basi na hawa uwachinjie baharini LAKINI....Probability ya kumeet na EX wako ukiwa na hawa mashem zako ni kubwa...Wale ni rafiki zake...Unapohang nao,ipo siku mtakumbana,na ita-trigger memory upya...You all know what am talking about...meeting na EX uliyempenda sio kitu rahisi,utaharibu siku yako hiyo na pengine wiki nzima..hata kama ulikuwa umeshaanza kupona,tunakurudisha LOVE ICU upya!

Jitahidi kukaa mbali na Mashemeji wa zamani especially zile siku za Mwanzo mwanzo ukiwa mmebreak,angalau jipe miezi kadhaa ya kukaa nao mbali,ukishazoea kidogo unaweza kuanza

Kuna watu mnashindwa kumove on kwa sababu hii....Kama Mashemeji ni tatizo,wapotezee kidogo mpaka utakapoona kamoyo kako kamestabilize then unaweza kuchill nao tena

4.UNAKOSEA MESEJI ETI...AU UNAMPIGIA SIMU ETI UMEMMISS...JINGA!

It doesnt make sense ila watu wengi tu tunafanya haya....Kuna muda unabanwa,unasikia kawimbo flani ambako labda alikuwa anakapenda...KOSA! Unanyanyua simu,Nimesikia ule wimbo wa LONELINESS wa BABYFACE nikakumbuka kweli yaani...Hii Call itaanzisha mambo mengi sana maana mnaweza kujikuta mnaongea,mtakumbusha weeeee hadi mliusikia wapi mara ya kwanza na kadhalika...ukikata ile simu Moyo wako umeharibika upya,utammiss upyaaa,kidonda kinarudi upya...Please avoid that!

Wengine wazee wa tricks za Magumashi,anatuma meseji MAKUSUDI,Baby last nite u were so good,i like that style....Halafu anajifanya kakosea kamtumia EX wake..Madai yake amtie Wivu mchizi/demu aone kwamba Dah!Mwenzangu kumbe kashapona na anakolezwa huko alipo...kumbe hamna lolote! Una mijiwazo yako lukuki,hakuna cha Last Night wala nini....Mtaanza ku-conversate bila sababu yoyote ya maana na mtaishia pabaya utajikuta unaanza upya bin upya!

Wale wenye hizi mabo,acheni...Hii itakurudisha nyuma na usishangae 2 years huna Uhusiano wowote bado,na kama Unao unayumba kwa sababu bado unambeba mtu fulani moyoni wakati nafasi yake haikutakiwa kuwemo,unashindwa kujitoa kwa New Love uliyopata...mwisho wa siku unakosa vyote...kule kwa EX hakueleweki,na huyu Mpya anakuona huna msimamo kwa kumbeba jamaa bila sababu zozote za maana!

5. KUDUMBUKIA KWENYE ULEVI NA STAREHE NA UKICHECHE/UPLAYER ILI KUMKOMOA

Tit for Tat wanaita....kwamba ukimwaga Ugali yeye anamwaga mboga....Watu wengine wameanza Ulevi wa kupindukia eti kisa Break Up...mtu anaanza mapombe eti kuondoa mawazo....Let me be very Clear here....POMBE HAIONDOI MAWAZO.....Narudia!POMBE HAIONDOI MAWAZO NA HAISAHAULISHI CHOCHOTE!

Utakunywa,utalewa tilalila,Utaamka ukiwa yuleyule! Na ukipata Marafiki wapuuzi wasio na msaada wanakusapoti kwamba kula bata,this is ur time...Jamaa alikuwa anakubana sanaaaa,hata outing ulikuwa hutoki yeeaaahhhhh we are divaaasss let us show him...SHOW WHO STUPID???

Unamshow nani...Hela utamaliza za kwako...Mwili unaounywesha Mipombe ni wa kwako....Na Kidney Failure na Kisukari utaumwa WEWE...Dont show anyone..Use ur brain.Usiingie kwenye Ulevi na Umalaya kisa UMEACHIKA,huo ni ujinga uliotukuka!

Wewe sio wa kwanza,mamako mwenyewe alishapigwa vibti 88 kabla ya kuolewa na babako,muulize atakwambia....Break Up sio mwisho wa Maisha..Ni challenge ambazo unapaswa uzishinde na Ukiweza utajikuta umejifunza mengi sana in life.

Wale Ma-Player,sijui ni VCD Player au DVD,poleni sana...Eti unaamua kuwa Player kisa Diana amekuacha..oh nilimpenda sana,Maisha hayana maana ngoja niwe Player....SAWA! Kuwa Player na UKIMWI utakuwa Kocha wako!

6.KUKUMBUSHIA....NAOMBA NICHOVYE KIDOGO TU ASALI HAPO KATI MTUNGINI

Kuna haja ya kuongelea hili kweli eti??Mbona najua hii balidahhh!!

Wazee wa kukumbushia Mupoooooo???Wadada wa kumiss Lips za EX mpooooo????Na wale wataalamu wa kutuma Meseji mmemiss Mjeledi aka Mjarabati mpoooo????

Unaachana na mtu mmeshindwana sera....Halafu mnamove on...unadate na mtu wako na yeye wa kwako...mnamisiana..mnakutana kwa siri...Mnatupia vituuz...Na mlikuwa mnapendana kwelikweli,mnadhani Feelings zitaisha...mnabakia Friends With Benefits.....Ma-New BF wenu na Ma-GF wanaona wamepataaaaa,kumbe nyie huku nyuma mna makubaliano yasiyo rasmi kati ya CCM na CUF kushare madaraka Zanzibar....

Hutamove on kamwe,utaanzisha Relationship mpya lakini una kitanzi cha mshkaji,mpaka mtakapojifunza kusema enouugh is enough....Lakini kila wiki 2 mna mechi kwa Hisani ya watu wa Marekani...Ah Msahauliwe!

Monday, January 21, 2013

WASICHANA...EPUKA TABIA HIZI KAMA UNA MPANGO WA KUWA MKE WA MTU ONE DAY LASIVYO SAHAU

PLEASE I NEED YOUR SUPPORT...PLEASE!

Tuma neno SETH kwenda 15678 SASA HIVI kama bado hujajiunga na Huduma ya Seth Straight to Your Phone.Its next level:Ili kupokea Meseji hizi na zingine nyingi kwenye simu yako ya Mkononi popote ulipo kubadilisha mtazamo wako wa Kimahusiano na Kimapenzi na kufanya maamuzi sahihi ukiwa kwenye Mahusiano..Usisubiri ufunge ndoa ndio ugundue ulifanya makosa kuingia....Kujiunga ni BURE kabisa hutakatwa hela kwa kutuma Meseji hii.Wateja wa Mitandao yote ya simu Tanzania wanaweza kutuma SMS hii na HUTAKATWA hata thumni...

Narudia,Tuma neno SETH kwenda 15678...Please tuma SMS kabla hujascroll kwenda chini kwa somo la leo....NAWAPENDA1
....

.....


......


.....


.......

........

Naulizwa WHY GIRLS...Kwanini nawaandika sana...Jibu ni rahisi sana,Wanawake ndio vichwa vya nyumba kivuli....Baba ni kama Raisi lakini MAMA ni Waziri Mkuu...Mtendaji mkuu wa day to day activities za Home Government...Waziri mkuu feki ni hasara kwa nyumba..Lazima washibe neno haswa ili hiyo nyumba isimame.Baba bila Mama bora hakuna Familia....

I have a lot to share to girls,natamani Familia Bora sana kwenye Kizazi hiki cha Nyoka aisee,na sitoacha mpaka nione Ma-mama bora wakizaliwa huku mitaani....

Leo nna katopic tena kwa ajili yenu,Wanawake...Najua siku hizi mmepata Hobby Mpya....KUPENDA NDOA!

Hii Hobby inawacost sana maana hamu zimezidi uwezo....Mnatamani sana ndoa lakini uwezo na credits za kuipata HAMNA...Sasa miujiza hii ya Maji kugeuka Divai mara ya mwisho alifanya Yesu tu kule Kana ya Galilaya,sijasikia tena maji kugeuka Ndovu Tandale...You must work for it...Very hard...

Na jinsi gani unaweza kuwork...ni discpline tu...Manage ur attitude! Wengi wenu ni kama mshakata tamaa...Mnajiendesha tu kama Guta...Values za Mapenzi hamna tena...Miiko ya Mapenzi mnaivunja bila hofu...Mapenzi yamekuwa Useless,kwahiyo kwenu lolote ni sawa....SI SAWA!

Kuna tabia ambazo,kama wewe ni Mwanamke na unazo,SAHAU kwamba utakuwa mke wa mtu,labda huyo atakayekuoa awe Stevie Wonder...Namaanisha kipofu,poyoyo,hakujui amekurupuka tu..Maana Wanaume hao wapo pia wanadamka tu na kuzama dimbwini kisa Housing....Kaona una shape kajaa kimiani,kumbe angelijua.....Ange...ishakula kwake anajitia kitanzini!

Kati ya Tabia ambazo Wanawake wa Kizazi hiki wanazo,na hawajali,bila kujua zinawaharibia Pozi kinoma,na zinawapa kitu wao wanaita Gundu,kumbe Gundu wamelikumbatia wenyewe,na wanalisababisha wenyewe ni hizi hapa:

1.MWANAMKE SAJENTI WA JWTZ MAKUTUPORA

Tunawafahamu Wanajeshi..lugha yao nzuri na tamu ni AMRI....Lete...Kuja...Kwenda....Rudi...

Sasa Mwanamke tangu lini una Amri kama umekabidhiwa Kombania ya JKT???Mwanamke yake mapozi na politeness...Lugha tamu....Mwanaume hahitaji Amri maana nature yake ni amri tosha...Akumbane na Amri za Bosi wake,na wewe home umletee Amri.Sasa nani BABA??..KINANUKA FASTA!

Utawasikia,

We Papito Casto hivi huoni kwamba sina viatu??

We Kataza,si nimekwambia Sina Vocha???

Lugha nzuri zimejaa teleeee...Baby wangu sina vocha ai weweeeee,nitumie japo buku.Unamrembea mkaka Sauti,HACHOMOKI!....Mwanaume ukishamrembea sauti hivi hata kama hakuwa na mpango atanunua tena Buku 2 atatuma tu....Sasa wewe endekeza Amri uone,utabip weee,utaishia kuomba TIGO NIWEZESHE!

2.MWANAMKE USELESS

Role kuu ya Mwanamke ni USAIDIZI....HELPER....Hii ni Kibiblia kabisa,Mungu akaona si vema Adam awe peke yake,akamtafutia Msaidizi....Sasa wewe Mwanamke husaidii anything,badili tu jinsia yako!

Kama kuna jambo moja tu unaloweza kunyonga Hisia za Mwanaume na akakupenda maisha yake yote ni kama utatimiza hili jukumu vizuri....

Kuna watu mnakaa na Boyfriends wenu/Wachumba/Waume,hamjui anafanya nini...Ana wazo lolote la Kibiashara...Humsaidii kumpa Mawazo mfanye nini kuongeza Kipato....Sasa we wa nini kwenye Maisha yake????USELESS
Akitokea Shankupe anayejua hii Siri anamuiba fasta,utashangaa,Huyu Mwanaume kafuata nini pale kwa yule shosti hata Sura hana,NDIO,Sura hana,Shape Sony Wega ya Inchi 26 kama Mjapenga lakini ROLE KUU kapata 100% kwanini jamaa asikutose????Inakula kwako I guarantee.

Likikugusa badilika...Onyesha kwamba upo..Show ur presence...Mwanaume kila akikaa akihesabu Mafanikio anakuona upo behind this..Behind That..behind that and that one....Sasa kila kitu kafanya mwenyewe,hela hujachangia...Hata wazo???Come on Girls!!!You can do better than that.

3.MWANAMKE DEBIT AND CREDIT NEVER

Hawa ndo Kiboko yao! Hakuna wazo atakalokupa ambalo ni la kuingiza hela..yeye kila wazo lake ni la kupulusa kilichopo bila kujali kitarudije na zikiisha itakuwaje!Wanatumia ile 'Shauri yake Principle'

Baby twende Maisha Club Leo kuna Usiku wa Mabeste anazindua Album jamani,Nampenda kweli Ben Paul atapafomu....

''Baby uko Mlimani City??please nichukulie 'Tuna' Fish hapo njaa inauma kweli mpenzi..hata hujui ana hela au hana,kiruu!

''Baby,nimeona cheni nzuri kweli can i have 60 thou mpenzi wangu,mwaahh...Ulimpa hiyo 60 thou??Ilikuwa kwenye Plan???Is it necessary ununue leo????THINK!

''Honey,kuna Samsung Galaxy nzuriiiii nimeona dukani,kama ile ya BFF wangu Joanita''

''Mpenzi,hivi huwezi hata kuninunulia VITZ,kwakweli nimechoka Daladala''.....Umechoka daladala wakti mamako bado anapanda,tena za Tandika...acheni biashara kichaa,hailipi!

Sisemi usiombe hela au vitu lakini hakuna hata sentensi moja ambayo ni Income Generating inaweza kutoa kinywani mwako hata mara moja kwa mwaka ili huyu MKAKA akumbuke kwamba She did this last year????

Hata kusema mpenzi nimeona tangazo kiwanja kinauzwa can we go see it and buy tujenge when tukioana?? Au Mpenzi kuna this Business nimeona rafiki yangu amefanya inamlipa sana,can you think of doing it???

Wewe ni Debit Debit Mwanzo Mwisho,hakuna Positive hata moja???Halafu unataka huyu jamaa A-propose ndoa???Na unamkomalia kwamba mbona yuko kimya hasemi kitu mwaka wa 3 huu???Apropose kuoa DEBIT????Ah nani kasema,utasubiria Treni hapo Ferry,subiri hapohapo hadi usikie honi..Anakutafutia tu Timing ya kukumwaga,maana ur a Liability to him japo hakwambii!

4.MWANAMKE CHAUPEPO

Hawa kama ni graph basi inaongezeka huku ikiongezeka...Waingereza wanasema Increasing in Increasing Rate!VYAUPEPO!
Jumatatu yuko Samaki Samaki...
Jumanne yuko Club Rouge...
Jumatano yuko New Palm Bar kwenye Baikoko na Friends.....
Alhamisi yuko Ladies Free Billicanas...
Ijumaa yuko Elements....
Jumamosi yuko Runway.....
Jumapili yuko Skylite Band Thai Village.....
Ana Ratiba kama Mbunge wa Msovero!

Unajua kuna mambo Wanaume wanafanya,sawa,ila Wanawake mkiiga wala haifai...mtasema mbona Wanaume wanafanya,lakini ukweli unabakia palepale,Mwanamke Chaupepo wa usiku ana-raise lots of Question Marks...Lots.....

Mama wa nyumba ajaye,anapepea haifai,hata Bendera ya Mwenyekiti wa Kijiji haikufikii,Wiki nzima una mishe,hujali hela ngapi umetumia kama kweli ni za kwako unajitegemea,but it shows that HUNA FOCUS....

Na hili lina-apply hata kwa Wanaume,siku 4 kwa Wiki zote unatoka,hata kama unatumia 20thou kwa siku,still its too much...ukisave hiyo hela unanunua tofali za kutosha tu....Mtalalamika ujenzi shida lakini hela unazokula gambe ili bata ikuzoee ukiichange FOCUS yako kidogo utashangaa kibanda kinainuka taratibu...Siongei Rocket Science,inawezekana,Nimeona na ninazidi kuona....Change ur focus and things around you will change...MEN,HEAR THIS!

5.MWANAMKE ZEZETA/GOIGOI/KILAZA

Mwanamke lazima awe Sharp...Bed...Jikoni...Everywhere! Make your Man proud of YOU!!Ukiwa Sharp hata mmeo atakusifia kwa rafiki zake,hiyo kafanya mama flani bwana....Sasa mmeo hana hata kimoja cha kukusifia....Bed pia uko shallow na you dont bother kujifunza wala,unaona utaaaammmm...Mh mama,wataka ndoa ama ndoano???

Mkisoma Sifa za Mke mwema kwenye Biblia ndo mtajua....Mke sio Sura au Shape,hata Punda ana shape...Mke shurti uwe SHARP.....

Kuna nyumba ukiingia tu unajua Mke KILAZA...liko wazi....Mwanamke Sharp hata ukifika kwake utaona....iko clear na kilaza iko clear...
Kuna watu wanaoa vilaza wanajuta...Mke hajui kupika,kutwa alikuwa anashinda vibanda vya chips na kula burger...Kisa ana shape umeweka ndani,dadeki bonge la pancha,muda wote anatengeneza kucha...Mwanamke kufua hawezi/hataki eti ataharibu kucha....Mwanamke anajua Kuoga na Kuvaa tu....Mwanamke kupika hawezi anamuachia Housegirl kila kitu....mahausigeli siku hizi ukizubaa tu MESSI huyooooo kapita,unapinduliwa Uganda hivihivi na IDD AMIN upo hapohapo!

Mwanamke kitanda akutandikie Housegirl????Halafu unategemea nini???Kama Housegirl anashine in the eyes of your Man kwamba yeye ndo Masterplanner wa House,Mmeo atajuta kwanini alikuoa wewe ni afadhali angem-turn Housegirl into a Wife....

Tafadhali,Think Twice,Ndoa sio kama Vinyweleo kila mtu anavyo...Zile Zama zimepita....Utabakia kutegesha Mimba huolei Ng'o maana huoleki...

Kama una hizi Tabia BADILIKA lasivyo chagua,ama UJIOE au UOLEWE na Same type of Stupid Man as ur maana mtakutana wote level za Ngassa na TEgete...ASANTE!

Wednesday, January 16, 2013

DALILI 8 KWAMBA MWANAUME UNAYETAKA KUMDATE HAYUKO GOOD KWENYE UKANDA WA 6 KWA 6 HIZI HAPA..

Hizi ni dalili 10 ambazo Wanawake mnaotaka kuingia kwenye Mahusiano inabidi mziangalie kwa Umakini sana kabla hujasema YES...

Lakini kama ushakufa na ushaoza juu yake,na ana cheda/mpunga/mijihela na ndicho ulichofuata najua topic hii wala haitakugusa....

Na wale wenzangu na mie ambao huwa tunaamini unaweza kumbadilisha mtu wa dizaini hiyo,basi sawa......

Ila ni muhimu uzijue,Ukiamua kuingia kwenye uhusiano nae uwe prepared kupelekwa Shallow kwenye shallow water na uwe willing kuvumilia tu na kujaribu kumbadilisha ukiweza...ingawa wengine wabishi hao,anavyopump ye ndo anaamini ni ze best,humwambii kitu....

TWENDE KAZI...

1.ANAONGELEA SANA MAFAILI YA MA-EX WAKE WA ZAMANI WALIVYOKUWA BED

Katika hali ya kawaida,Mwanaume rijali na anayejiamini hawezi kukaa na kuwaongelea Ma-ex mbele yako,na kuwasifia kwamba walikuwa wakali kweli bed...Ukiona Mwanaume wa dizaini hii ujue anajaribu kukuonyesha kwamba 'He had his best' na wale kwahiyo inabidi uprove kwamba unaweza kuwafikia ingawa hakutakuwa na kipimo coz ur not even sure kama walikuwa wakali au yeye ndo alikuwa Shallow alikumbana na Shallow wenzake waliomzidi uwezo akawaona wakali...

Ukiona Mwanaume wa type hii,tembea na Question marks mkononi na uendelee kuangalia Dalili zinazofuatia kama zinaendelea ku-match au lah..Kama anazo 8 kwenye hizi 10,aaah chezo hamna hapo!

2.HAJUI KUCHEZA MUZIKI

Ukiacha Blues ambayo hata watoto wadogo wanacheza kwenye ubarikio,hajui kabisaaa kucheza,....Weka Shamukwale holaaaa...Mayaula Mayoni wapiii...Kiduku holaaaa....Alingo Holaaaa...Taarabu zirooo...Mduara nehi bambuchi....Sasa viuno ataviweza wapi???Labda kwaya....

Kama Muziki una Midundo na Beat hawezi,Mtanange wa Bed usio hata na mlio wa zumari ataweza kwenda na mapigo kweli???Weka viulizo,Muziki ni Kipimo kwamba hii njemba alfu ulela,hadithi tu!

3.ANAONGEA SANAAAAA

Hawa wapo wengi....Ahadi lukuki,mimi nomaaaaa...muulize flani,yule demu ananikumbuka mpaka leo....Ah yule nilimpa vitu akakimbia...oh vilee...Tuu machi perepepe! Mpe kinu,ulimi huu...
Mwanaume anayejisifu sana kwamba anajua vyenga kama Messi ukimpa Penati anapaisha kama Nsajigwa...Kuwa nao makini,weka viulizo,maneno mengi vitendo hamna!

4.HAWEZI KUKUANGALIA MACHONI HATA SEKUNDE

Connection ni kitu muhimu sana kwenye Mahaba...Aibu haina nafasi....Kama hamna connection kwenye Macho na huyo mtu,akikuangalia sekunde 2 anakwepesha macho jiulize anaogopa nini???
Hawa ndo waleeee wataalamu wa kupenda giza,mkifika chobingo anafall in Love na Swichi....Mapenzi ya aibu ya wapi haya???
Raha ya tunda liliwe mko Connected...Lazima Computer iwe na Internet connection na Modem ili uweze Kubrowse...Sasa Modem umezima unasurf vipi????
Hakuna raha kama kuwa na connection ya macho,macho yana siri kubwa sana....Kuna wanawake ni Mabingwa wa kufake Orgasm,unaweza ukadhani unatwanga kweli maana hizo kelele kama kaumwa na Nge kumbe wala....Ukitaka kujua Fake orgasm ANGALIA MACHO,Hayadanganyi kamweee,utajua tu hili Gubegube LINAFAKE MAMBO!Chukua Siri hiyo,itakusaidia

5.TOO MUCH DRINKING,PIGA SANA ULABU MPAKA MASANGA YANAOMBA RADHI

Mwanaume mlevi ni ngumu sana kum-satisfy Mwanamke! This is a fact.Wanaume wengi mnagongewa mademu zenu na Wake zenu kwa kuendekeza Pombe especially Bia...Vikao vya Bia haviishi,muda wa kukaa na demu wako au mkeo huna,unarudi umelewa unazima..hiyo moja,2 unapiga masanga unalewaaa,unakuja unaomba mechi,ukipewa  vitu dakika 5 nyingi unamwaga Povu halafu unazima kama Trekta la Massey Ferguson...Kweli huyu Mwanamke atavumilia A ONE MINUTE MAN???
Siku ampe mzee wa kazi anayejua  kokoto ni kokoto na jiwe ni kaka yake kokoto,unakuta kalima lami...Muda si muda,Wanawake feelings zao kuibiwa rahiiiiisi,atakusahau,na hata ukiendelea kuwa wake hisa asilimia 80 kashapewa msela..Wewe upige usipige ye kashapata wa kumshushia Vitu...Mupe Muruke...Mupe...WEWE UNABAKIA BOYFRIEND JINA!
Si ajabu hata wewe ni Boyfriend Jina tu,ila kuna mtu anaipiga hiyo kitu mpaka inabakia na rangi ya Royco...wewe lewa weeeee,yumba weeeee,mwenzio katulizwa tayari....NIMEMALIZA,Mwanaume hasifiwi chupa ngapi za Bia,anasifiwa 'KAZI'

6.CHUMBA CHAKE KIMEJAA UREMBO,PERFUME KIBAOOOO,PODA...JIULIZE

Huyu Mme au Mwanamitindo??
Hii ni subject to discussion...Wengine watasema usafi wa kawaida...Wengine watatetea sana ila too much of anything is harmful...Sisemi Wanaume tuwe wachafu,na tusinukie ila mmh...Pierre cardin,Prada,Gucci perfume...Mapoudah nini pale kati...Mwanaume dah,wengi wa dizaini hizi ni wachovu,YES,watavutia wadada kwa kung'aa lakini wadada mtakuwa mashahidi,hawa marioo wanaonukia nukia kila muda wanafuta viatu wanapiga kazi kweli????Mtanijibu kule kwa Wall...I DOUBT! Wengi Mjarabati hawawezi,wana mapenzi ya Mrabaha tu!Kipande hapa na pale ''Baby some water please,hoi!''

7.CHUMBA CHAKE KAMA CHA MFANYABIASHARA WA MBAO

Ingia chumba cha huyu jamaa,rafuuu mbaya...atasema ye msela...
Glasi chafu za juzi kwenye sinki full nzi....anasubiri umuoshee
Mabegi kuleeee..Nguo chaliiii....Vitu ovyo ovyo....Hana mpangilio kwenye lolote lililomo chumbani...
watu wa namna hii wana dalili za ugoigoi..wavivu....
Kama hawezi kupanga vitu room...vikapangika,ataweza kupangilia chochote kwenye Mahaba???Atajuaje aanze wapi..Kisha aguse wapi...Ashike wapi,na aingize wapi??Thubutu,utashangaa huyooooo kadandia...Baba mara hii????

8.SELFISH NA HAKUFIKIRII WEWE KWANZA

Kuna msemo wa Ladies First...Si lazima utumike lakini we expect Gentleman autumie..na sio kwa kupretend!

Mwanaume asiye selfish utamjua tu...He cares about his girl first..je,honey kashapata???kabla hajajifikiria...

Ukiona Mwanaume anatembea fasta MWanamke yuko nyuma bila kujali amevaa High Heels amsubiri...Yeye kuleee mbele kama  kuruta wa JKT demu wake yuko nyuma,as if hawako safari moja...Jiulize,why???

Ukiona Mwanaume mnaingia kwenye gari yeye wa kwanza kashajifungulia mlango kazama,maskini demu wake yuko nje...Jiulize

Ukiona Mwanaume muda wa kula,yeye kashajiwahi kanawa kaanza kula bila kujali mama yupo...Jiulize

Hii ni mifano midogo sana lakini it shows jinsi gani huyu jamaa hajali presence ya malkia around him....Wanawake tumeumbwa tuwahudumie,vitu vidogo vinawafanya wajisikie kama wanapaa hivi,sasa wewe hata hivyo vidogo navyo kero,humpi...Sasa huyo ni mpenzi wako au Bodyguard???

Aina hii ya Wanaume,hasara moja utakayopata wewe mdada ni kwamba mkifika Bed,hatajali wewe umefika Kileleni au Lah,Maadam yeye kashasuuza rungu na Wazungu wameshuka na ndege ya KLM,basi kwake kamaliza...Utajibeba mwenyewe,utajishushaje huko uliko is none of his business....Sasa we mwanaume ukiibiwa na washushaji wenye uzoefu utalalamika???BLAME UR OWN SELFISHNESS...

Kabla hujajifikiria wewe mfikirie yeye kwanza...Kabla hujafikiria kumaliza make sure naye kamaliza atleast Viwili flani ndo ushuke,sio unatua kama Ng'ombe bila kujali hali ya hewa..Uanaume sio hivyo baba!

NATUMAI TUNAENDELEA KUPONA,KAZI NI KWAKO!

Tuesday, January 15, 2013

KAMA WEWE NI AINA HII YA MWANAMKE,YOUR BOYFRIEND MUST CHEAT NA USIMLAUMU

Girls....You run this World right???Run it with your Brain!

Wanawake wamekuwa Mabingwa sana wa kulaumu Wanaume kwanini wanacheat sana..Na wanaamini kwamba Wanaume hawana Reason ya Kucheat maana wao wanadhani wamefanya yoteeee,sasa kwanini jamaa acheat??

Leo naleta kwenu Aina ya Wanawake ambao wao wenyewe kwa hiari,wanafanya mambo ambayo ni Greenlight kwa Mwanaume kucheat...

MASHARTI KIBAO KAMA FOMU YA MKOPO

Hawa wanawake wana misimamo yao ambayo sijui wamefundishwa na Ngariba wa Loliondo au lah...Inapokuja suala la Bed Business,UTACHOKA! Kungfu si Kungfu...Taekwondo Si Taekwondo...Sarakasi si Sarakasi,ilimradi kero....Hataki umguse hiki...ukimgusa kile hataki,ye anataka kipondo alale....Mapenzi ni sanaa...Mapenzi ni Sayansi...Mapenzi ni maelewano ya wewe na yeye,anapenda nini,unapenda nini,maadam haombi kubadili Channel kutoka BBC kwenda Deutche Welle(Kula Tigo) sioni kitu ambacho ni kibaya kitandani...

Sasa utaambiwa Mate ni Uchafu....Ukimshika nanihii ili umuandae awe Wet vizuri(na hii ni recommended kiafya kuepuka Unnecessary Friction wakati wa tendo), HATAKI,eti sijazoea kushikwa huko,,,Sasa ushikwe Pua au???

Hataki kunyonywa(japo raha ni ya kwake)...Hataki kunyonya(BJ) eti ni uzungu na uchafu....Sasa ndugu zangu,haya ni Mapenzi au wazimu???Yaani nikurupuke tu,bila Maandalizi,bila kujua you are wet enough or not,nakurukia kama nadandia Bajaj...kweli???

Sasa Mwanaume huyu akikamatwa na kitoto kinachojua umuhimu wa Maandalizi,kikampa makamuzi,Mmeo/Boyfriend anakalishwa chali kama anasubiri Oparesheni ya Appendix,anashughulikiwa,akija kupewa mzigo You think huyu Mwanaume atakuwa na time na wewe???Muwe mnawaza...

Mapenzi sio Biashara ya Usafi,kama unadhani Mahaba yana usafi umekosea njia,hakuna Biashara ya Uchafu kama Mapenzi,ila Uchafu wenye raha...

Ukiwa penzini huna tofauti na Chizi,akifika jalalani hachambui hiki nini na kile nini...Maadam kinalika basi ndo anaponea hapo...

Kama Mapenzi yako yana masharti kama Dokta Manyaunyau,tafadhali tafuta biashara nyingine ya kufanya,hii ushafeli...

WAZEE WA MUDA

Hawa ni mabingwa wa kuhesabu dakika....Utasikia humalizi tu....Jamani nusu saa bado upo tu huchoki....We mwanaume robo saa si tayari unanikomoa??Nani akukomoe wewe!!
We Mwanaume hiyo ndo style gani....
Nani kakufundisha hii mbona hatujawahi kufanya.....

Sasa haya Mapenzi au Interview???

Yaani muda wote mnapepeta ye anauliza maswali tu kama OCD wa Polisi Mabatini,sasa raha utasikia saa ngapi???Mwanaume anajipinda ili akufikishe wewe umekazana na Questionnaire yako....Mara kidogo filimbi hiyo.....utasikia Maliza bwana mi nimechoka..Yaani kauliza maswali weeeeeee,halafu anakwambia Maliza....Dah,ukute we ndo kwanza uko Chalinze,unaambiwa maliza,sasa sijui utafika Ubungo Stendi na Ungo....Kwakweli,kama uko hivi,sishangai Mmeo akicheat,kosa ni lako mwenyewe!

WANAWAKE MMENISIKIA????MASHARTI ZIACHIE FOMU ZA MKOPO WA BENKI

Monday, January 14, 2013

WAKATI MWINGINE SECOND CHANCE HAINA MAANA KWA BAADHI YA WATU,WANAITUMIA VIBAYA

Yes ,Lovers!Once again,naleta mzigo mwingine muuthaminishe wenyewe...

Wote tuna mioyo na hisia,wote tunafall in love kila siku maana tuko tunatafuta Penzi la kweli...Penzi la kweli sometimes ni ngumu sana kulipata,ni safari yenye milima na mabonde..the journey is hard...

Katika pitapita yako,bahati nzuri ukaokota kijamaa au kidada,ukakipa moyo wako mwenyewe,una-expect kitautendea haki...kitakupa mahaba..Kitakupa mambo adimu,sio kama wale wengine ealioudundisha kama Kitenesi...
.....Kiupe mdomo wako smile na sio mnuno kama ufudu...
....Kiupe moyo wako sababu ya kupump damu kwa raha na sio kuuchezesha kiduku..
....Lakini wapi...Kinafanya tofauti na ulivyotegemea...

Inafikia kipindi unaamua,bwana basi! Enough is enough wanasema Waingereza!Unanyosha mikono juu hata kama unaamini wewe ni shujaa wa Mahaba..

Umejaribu kila mbinu kufanya Love Life yako ikupe furaha imeshindikana....
....Umejaribu kujifanya mjinga imeshindikana...
....Umejaribu kujitoa,kumfanyia mpenzi mambo mazito ambayo hata mzazi wako humfanyii maskini,Ili tu,Penzi lako liende vizuri....

LAKINI,Mtu unayemfanyia hayo yote,Je,Yeye anachukulia mambo kwa uzito sawa na wewe???Au umejitwisha Injini ya Scania peke yako???
Mara nyingi watu tunaowapenda na kuwabeba mioyoni mwetu kwa uaminifu na Mapenzi na Huba,hawajali lolote...Wanakuona Kichaa tu,na pengine wanashangaa,kwanini huyu Mwanamke anahangaika hivi???Kwanini hili Lijanaume linanipenda hivi,halina kazi???

TATIZO LINAPOKUJA,Pale unapoamua its over,utashangaa!!

Mtu huyuhuyu aliyeonekana hajali lolote pamoja na Mapenzi yote uliyompa,anakuja kwa nguvu,Atapiga magoti,ataomba marafiki msaada wamuombee msamaha...
Anaweza kuita hata Matrafiki wamsaidie kukwamua gari lake limenasa...Unajiuliza,alikuwa wapi hadi amesubiri haya yote yatokee ndio aonyeshe umuhimu wako kwake kwa misamaha yenye ahadi kama nyingi kama Ilani ya CCM??

ANAOMBA UMSAMEHE,UMPE NAFASI TENA...

Unaona sio ishu,maadam kaomba unampa...Anajitahidi wiki ya kwanza,fresh...Ya pili poa....ANASAHAU...

Mnarudi kulekule,vichozi vyako vilivyojikusanya kwa Wiki 2 za Mapenzi ya Ampicillin vinamwagika tena mwaaaaaaaaaaaaa.....
Na aliyevimwaga ni MTU YULEYULE??

Swali ni Je,NINI UMUHIMU WA SECOND CHANCE kwa mtu asiyeweza kuitumia Second Chance kujirekebisha????

Upuuzi uleule.
...Makosa yaleyale..
...Ujinga Uleule.
...Mateso yaleyale,na maskini ya Mungu Moyo ni huohuo,unauongezea tu Ufa....Matundu....Vidonda.....

JIHURUMIE WEWE KABLA HUJAMHURUMIA YEYE....

Kama kuumia unaumia wewe...Kama yeye alivyo na Moyo,na wewe unao pia,tena wa nyama....

Hata ukimpa SECOND CHANCES ELFU 8,kama habadiliki HAKUFAI...

Maana halisi ya Second Chance huonekana pale MPEWA anapogundua Makosa na Udhaifu na Kuitumia Second Chance kuonyesha kwamba Mapungufu yale ilikuwa ni Bahati Mbaya tu na Kujisahau.....

Kumis-Use Second Chance kwa Kurudia yaleyale ni TUSI kwako kwamba ''Wewe ni Mjinga kwa kunipa Nafasi ya Kukuumiza kwa Mara nyingine tena''...

Think twice kabla hujampa Mtu Second Chance,ANAMAANISHA au Anaiomba kwa sababu ipo kwenye Kamusi????

TAFAKARI

Sunday, January 13, 2013

HALI HIZI ZIKITOKEA,PLEASE BREAK UP,HAKUNA ISHU TENA HAPO IMEBAKIA MAZOEA TU

Haya tena..Mwaka 2013 ndo huo...Heri ya mwaka mpya!
This is my first article of the year...Kwa wale walio In love na wako fresh hongera kwenu...Wale wenye Relationship Vichomi poleni sana na endeleeni kusali...

Leo naleta hoja tena mezani....Vitu gani ukiviona kwa Mpenzi wako basi anza kupaki begi la Nguo usepe...Natumaini baada ya somo hili,utaenda na kuanza kuchambua kitu kimoko kimoko,upime,Je,ni sahihi wewe kuendelea kuwepo na huyo mtu au lah...

1.KILA ANACHOFANYA SIKU HIZI KINAKUBOA
Hii ikitokea maana yake ni nini???Hakuna analofanya kwako jema,kila anachojaribu kufanya whether its good for u lakini wewe inaku-piss off...Kuna jambo..Siku zote,mtu akikutoka rohoni,hakuna jema atafanya utaona..Hiyo ni dalili kwamba amekutoka moyoni..the love is dead...Ukimpenda mtu,utapenda mambo anayofanya,sometimes ni mabaya lakini you live with them because YOU ARE N LOVE.If what happens is the opposite,sepa!

2.HUPENDI VILE ULIVYOMPENDEA
Kama ulimpendea alivyo,Nywele,Macho,anything...Ghafla Personality ile iliyokuvutia imepotea..Huoni uzuri wake anymore,unaona karaha tu,,,hata avaeje unaona hapendezi,nywele nzuri zinaonekana minywele au kipilipili...Mama,sepa tu...You have lost ur appetite in him,u wont eat him no more

3.PRIORITIES ZENU ZINADIFFER

Hapa ndo patamu..Umewahi kuona Relationship zenye argument kwenye kila kitu???Mama anataka wali baba ugali...Mama anataka kujenga Baba anataka gari...Mama anawaza kutoka Outing Baba ana hamu ya kulala...Moja haikai 2 ndo kabisa haisimami....Mtawezaje kukaa pamoja huku mnatofautiana mitazamo????Ikifikia hapa,bora ujichenge fasta,ukikazana utaumia

4.HAUM-MISS AKIWA HAYUPO
Zamani akiondoka tu unatamani arudi...Haipiti siku hujamuona....You miss texting na kumcall..

Siku hizi wala,unakata wiki asipotaka kukuona unakausha tu na unaona fresh....Asipokupigia na kukutext na ww unasahau kabisa kama anaexist...That Love is dead

5.UNAONEA WIVU SANA WENZIO
Ukiona unaona sana wivu kwa wenzako wenye relationship na kuhisi wanafaidi sana jua kwako kumezama..Kama kwako kungekuwa salama ungejisikia ur better off kuliko wenzio na hata kama wanafanya jambo romantic kwako si ajabu maana nawe unafanya...Dalili kwamba what they have kwako imekufa inakukoroga nafsi,unatamani zama zirudi ila ndo zimepita,ni kipimo tosha kwamba Penzi lako limekufa

6.UNAONA SANA NJE

Zamani hata pite mdada mcutie wala hukuwa na habari...Hata apite mkaka ananukia,unatembea kwa mguu unapewa Lifti wala huhangaiki...Ila siku hizi macho yamekutoka,Kikalio kidogo unakifuatilia kama taarifa ya habari ya BBC....Kila mkaka unaona Hes Cute,wow Hes cutee,,,Jua kwako kumeungua

7.MAGOMVI HAYAISHI
Kuna watu wanateteaga ugomvi..Kwamba bila ugomvi eti Relationship haigrow...Sawa!Lakini Kila saa??Kila Siku??Kugrow gani huko???Kila muda manundu,labda mnakuza ndonya!
Ukiona magomvi kila saa kwa vitu vya kiboya na kipuuzi,na haikuwa hivi zamani,Jiulize,KULIKONI???

8.UMECHEAT/UMEMKUTA ANACHEAT

Hii ndo funga kazi,huoni tabu kucheat...Hata akijua poa tu...Hiyo ni dalili kwamba Jumba Bovu limeegama upande....When ur in love, there must be some Guilty Conscious in You....Ikipotea hiyo  bhaaassssssssss..Ukiona manyoya ujue kaliwa!

NI HAYO TU...JE,UNAYAONA KWAKO???TAFAKARI!CHUKUA HATUA!HAKI ELIMU!

Tuesday, October 30, 2012

WHY DO MEN LIE???

Hahahahaaaa!!!!

Mniruhusu nicheke kwanza....Girls, you wanna know????

Sababu chache kwanini Wanaume ni waongo hizi hapa:

1. WANAJUA

Uongo wa Mwanaume ni kama muvi...Kabla hajadanganya anapanga angle zote na majibu,ana-anticipate ataongea nn,utamjibuje,utamuuliza nn,na atakujibu nini...Wanawake hamuwezi,huwa mnapanic,na siku zote ukipanic umefeli

2. HATA TUKISEMA KWELI MNADHANI TUNADANGANYA

Hii ndo ilivyo,na inaudhi...Kwa sababu tunadanganya sana,hata pale tunaposema kweli basi nyie mnatuona wezi...So hakuna maana kusema kweli,bora tuendelee na PHD ya uongo tu-graduate

3.  WANAWAKE WANAPENDA UONGO

Japo hawasemi lakini hili tumeliprove,Wanawake ukimwambia uongo ndo anapenda...whether kwa kujua au kwa kutokujua...Ukimwambia ukweli anakuona hamnazo...Ukimwambia Mwanamke kweli utajuta....Itakuwa ndo wimbo bora wa mwaka...Masimago na Rewind button...Mwaka mzima,ukikosea tu wanarewind ulichokiri..

Waulize Wanaume waliowahi kukiri kucheat wakusimulie,wanajuta kwanini walikuwa na mahaba kuliko Bwana yesu...

4. UONGO KWENYE MAPENZI  NI NDIMU KWENYE SUPU

Mapenzi ni sanaa na sayansi....Mapenzi sio engineering!

Kama ndimu kwa supu ndivyo Uongo kwenye mahaba...kuan vitu unajua umedanganywa lakini unatolewa macho makavu inabidi uwe mpole..inabaki kama drama,na inaleta ladha flani ambayo ni ngumu kuielezea,japo wanawake wanaweza kuielezea how they feel pale ambapo wanajua wamedanganywa lakini hawana proof kwamba ule ni uongo...Mwanaume anashinda kirahisi...inabakia kama assignment flani hivi kwa Mwanamke kwamba next time lazima awe wise kidogo kumkamata...Na hiyo ndo ladha yenyewe na vionjo vya mahaba

SISEMI MDANGANYE,ILA NDIMU KIDOGO TU SUPU IPATE KUKUPA HAMU

WANAWAKE WAKICHEAT,WANA SABABU 4 TU,SI ZAIDI YA HIZO..HIZI HAPA

Ni ukweli usiopingika kwamba CHEATING is now a National Anthem...Kila mtu anaongea...kila mtu analalamika...Mapenzi na relationships yamekuwa magumu kwa sababu watu wanaogopa kuhusu ukweli na uaminifu wa wenza wao waliojitoa kwao kuwa in love...

Watu wengi(ikiwemo mimi), wanaamini kwamba Wanaume ndio wanaongoza kwa kucheat...The reason behind is, Men cant get enough...Every time is tea time using any cup....Lakini pia,Mwanaume akicheat(in most times) hamaanishi kihisia tendo analolishiriki isipokuwa kujisatisfy hamu...Ndio maana,wanaume wanaweza kufanya mapenzi na mwanamke hata hamjui jina na wakaachana hawajuani majina....Thats not the motive..Jina la nini???

Leo sikuja kuongelea hilo.....Today, Lets talk about Reasons which make WOMEN(Ambao wao wanajinasibu kwa kuwa waaminifu kwenye mahusiano), japo ushahidi unaonyesha nao hawavumi lakini wamo.

Achana na Magumegume/Micharuko/Vicheche/Maharage ya Mbeya....Kwa wale wanawake ambao wako kwenye mahusiano na wanaya-value,ikitokea wakacheat,basi wanaongozwa na Reason zifuatazo:

1.MATATIZO YA MWANAUME ALIYENAYE.

Hii huwa ni Lomg-term.Wanawake wameumbwa na software ya ajabu sana,wana uwezo wa hali ya juu ya kuvumilia....Kiu ambacho Wanaume hatuwezi! Wanavumilia mpaka vile visivyovumilika kirahisi....Kama Mwanamke ni mwema na mwaminifu lakini akapata Mwanaume ambae hamridhishi kwa kiwango anachotaka,na akashawishiwa aidha na roho yake,au mashosti,kwamba She can get something better...after a period of time ya uvumilivu,ATACHEPUKA....Ingawa roho itauma maana hajazoea,hakupenda iwe,lakini aliyekabidhiwa jahazi anasinzia,basi atampa mwingine mwenye uwezo wa kusimamia kucha,na akiisimamia vema basi ujue huyo si wako tena

2.REVENGE KWA HISIA KWAMBA UMEMCHEAT

Hii nayo ni Long-term....Ukimcheat Mwanamke na akajua,itamuuma,lakini atasamehe(kama kawaida yao),itaendelea kumhunt ndani kwa ndani....Inawezekana kwa muda flani asipange kufanya lolote,lakini endapo litatokea jambo akabananishwa kwenye kona ambayo uwezekano wa kuchomoka ni mdogo,basi anaweza kutumia justification kwamba 'afterall mbona flani alinicheat',akajikuta anafanya ili kuweka mlinganyo sawa.Hii ni dhahiri....Wanaume,make sure you dont pin your girl in this corner,kwa sababu akianza na ikatokea jamaa amesimamia show vizuri inaweza kuwa mwanzo wa series ya yeye kucheat kwa kutumia justification ileile moja uliyomfanyia,na itakula kwako mazima...Itachukua muda kuanza lakini ikianza haisimami!

3. KAKUCHOKA-NO MORE SPARKS OF LOVE-NO EXCITEMENT

Kwenye mapenzi kuna kuchokana,hilo liko wazi...Kama imefikia hatua ile spark iliyokuwa between you imeanza kufifia na hakuna njia mnayotumia wote waili ku-ignite pendo lenu upya,Mwanamke huyu anaweza kuanza 'kuwaka' na wanaume wengine wa nje,na akajikuta anatumbukia kwa mmoja au wawili ili kuweza kusaka Spark mpya.Wanawake wanapenda content...Sparks na excitement kwao ni kama Pie 22/7...Ndio maana haijalishi Mwanamke umemfanyia Shopping mara ngapi au umemnunulia zawadi mara ngapi,kwake kila Shopping au zawadi ni NEW EXCITEMENT.
Akiikosa kwako,akaipata kwa mwingine,usimlaumu kwa kuchangamkia nje kwa sababu ni wewe uloiyeshindwa kusoma alama za nyakati na kushindwa kumpa sparks anazozihitaji....MEN.,play your part well.

4.KIPATO vs DHARAU NA WOGA

Hii hutokea pia,japo ni 50-50...Si wanawake wote wakipata hela wanabadilika na kuanza kuwadharau wanaume wao,ingawa in reality Mwanamke akikuzidi hela,wewe kama Mwanaume unaanza kufeel weak hata kabla hajasema...Utashindwa kuperform kwa inferiority uliyoijenga mwenyewe,na Mwanamke huyo akiiona inaweza kumchange na kujihisi more superior....
Akianza kupata feeling ya Superiority ataanza kumingle na Superior men ambao watampa new adventure ambayo wewe Mwanaume wake hauna....TROUBLE! Pamoja na hela zake,atajikuta anahudumiwa vitu ambavyo ww huwezi kumpa,atapelekwa trip za dinner Dubai bila wewe kujua na huwezi....Ataliwa hukohuko na hatasema...Slowly, ur love will die...Sio kwa sababu alipenda,ila Inferiority yako ilikumaliza mwenyewe.
MEN,Ikitokea mwanamke uliyenaye amekuzidi kipato,ONGEENI,mlijue hili linaweza kuwa tatizo na mjue how to go about it lisiwaletee shida,ili mwanaume na mwanamke muwe at peace na kila mmoja aheshimu nafasi ya mwenzie kama mlivyokuwa mwanzo

Wednesday, September 26, 2012

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU ATOA LISTI YA WANAUME 322 ALIOWAAMBUKIZA NGOMA

Kumekucha...

Huku vyuoni sijui wanafundisha nini siku hizi maskini,naona ni ngono tu ndo somo ambalo wanafunzi wanafaulu sana...Matokeo yake ni kuambukizwa magonjwa makubwa...INASIKITISHA

Mwanafunzi huyu wa kike ametoa listi ya wanaume 322 aliowaambukiza ngoma....Nia yake ilikuwa aambukize wanaume 2500 ila sio kazi ndogo..ameingiwa roho ya ubinadamu ameamua kustop sasa...Lakini Stop Watch yake imezima baada ya kuwa ametimiza listi ya Wanaume 322...Haya ni mafanikio ya asilimia 12.88 ya Target yake.

Kwanini ameamua hivi....Mara yake ya kwanza kabisa yeye kufanya ngono...Hapohapo akaambukizwa UKIMWI....Wanafunzi mkiambiwa muende kusoma msome,Mapenzi yapo tu,hayana haraka,mnakimbilia mambo yasiyo na tija kwenu...Someni..Yatawakuta kama huyu dada.

Chuo anachosoma ni Nairobi University...Picha yake hiyo hapo,mtoto mkaliiiiii,ukimtazama kwa macho lazima utupie mbichi maana kanona....Ila ndo ameshaungua sasa

Tuesday, September 25, 2012

SABABU KUU 3 KWANINI WANAWAKE WAMEAMUA KUKIMBILIA USAGAJI


Ni aibu sana kwake..Kwa familia...Kwa jamii,na ndio maana wanajificha...Haiko wazi coz its awkward...

Wanawake ni viumbe so complicated...They need perfection...Sometimes wamejikuta wakichukua hatua ngumu sana kwa sababu tu hawapati Perfection wanayoitaka katika kitu fulani..

Mathalani kwenye masuala ya mahusiano,Wanawake wamekuwa wakilalamika sana,sana sana especially siku hizi,na wameamua kutumia SHORTCUT...Wameamua kuwa Wasagaji ili waweze kukabiliana na presha za vitu kadhaa vinavyowanyima raha....

Usagaji ni kimeo...kibiblia ni DHAMBI NA CHUKIZO KWA MUNGU....Kibinadamu ndio kabisa,ni AIBU KUBWA....Kihisia ni Uongo mtupu....Kwa nguvu zote tuungane kuupinga usagaji...watoto wa kike wengine wazuri sana,warembo,ukiambiwa ni wasagaji hutaamini,lakini ndivyo!

Sababu kuu 3 kwanini Wanawake wanashift na kuamua kuwa Wasagaji ni hizi hapa:

1.WANAUME WANAZINGUA

Hii ndio Falsafa yao Mpya.Wanaume mizinguo! Wanawazinguaje...Hawana true Love...Wanawamixx na mademu kibao,wanaumia feelings...Kwahiyo kimbilio pekee ni kwa wanawake wenzao,maana they can control them...This is so fake...Mungu hakuwa mjinga kukuumba Mwanamke na akamuumba Mwanaume kuwa na Kiungo ambacho Mwanamke hana ili kikune pale,sasa huu mkuno wa Female kwa female,hata kama Wanaume ni mizinguo,si vema kuwa na Temporary Solution kwa Long term problem...Kwani zamani hakukuwa na Wanaume???why nyie tu mje na sababu hizi???

2.WANAUME WANASHINDWA KUKUNA IPASAVYO WAKIPEWA NAFASI

Hili naweza kuwaelewa.Wanaume siku hizi wamekuwa mariyoo mno...Swagger kibao zimejaa..Mapenzi hayana Swagger,Mapenzi ni kazi,ukipewa Kifusi shindilia,unaleta Swagger Bed???Swagger hazilipi bili....

Mtu asubuhi anakula Kababu...mchana chips yai..Usiku Soseji...Utaweza wapi kazi sasa???Wanawake wanataka mzigo,kuremba kwenu...Hili Wanaume mnabeba lawama zoteeeeeee,usipopiga kazi,aidha watapiga Wanaume wanaojua shughuli,au ndo hivi sasa wanaanza kushughulikiana wao kwa wao,maana wanajua wapi pa kugusa mwenzao aje...Wanaume acheni Swagger,ukipewa kazi kamua...

3.KUIGA

Kila kitu cha West nanyi mmo...Ukiomna Marekani wanapromote unatamani kujua nn utamu wake...Mtaiga kila kitu????Iga vya maana,huu upuuzi achaneni nao,wazungu maboya,wanawalisha kasa mnapotea...ukianz hii kitu kuacha ni shughuli pevu sana...Mnaharibu wenzenu,mnaharibu watoto wenu mtakaopata..na mnaharibu jamii

Chekini wenzenu hawa maboya hapa chini,sasa ndo nini hii??Raha ya utamu upewe na kidume,ILA kidume kijue kazi...

Wanawake ni kwa ajili ya Mwanaume...Hasi na Hasi sio mpango...Mpango mzima Chanya na Hasi...

WANAUME....Pigeni kazi,hawa Wanawake hawataki stori mingi...kazi tu,we kula kula michips hiyo uone kazi
Saturday, September 15, 2012

NINI KIMEFANYA WANAUME KUTOKUWA NA HURUMA NA WANAWAKE THESE DAYS

Iam back....Sorry kwa kuwa kimya kwa muda,hii ni kutokana na kubanwa na mmbo ya hapa na pale katika kujenga nchi...

Leo tujadili hili...Na sababu kubwa iliyonifanya nilete mada hii ni kutokana na mambo ninayoyaona,watu wengi wanazidi kulalamika,na baadhi ya watu wa karibu wamekuwa wakinieleza jinsi wanavyoumizwa...Na hawa wengi ni wadada

Wadada wengi siku hizi wanalalamika wanaume wamekuwa Mbwa...Na ninakubaliana nao kwa asilimia 100..Kweli Wanaume wamekuwa Mbwa haswa....Hawajali anymore...Lakini nini kimesababisha Wanaume kuwa Mbwa siku hizi...Twende pamoja

1.GENETIC REASON

Kwa jinsi wanaume walivyoumbwa,wameumbwa wawe watu wa control...Na hii ni Kibiblia kabisaaa..Na hata socially iko hivyo

Kutokana na hii sababu,ikitokea Mwanaume akakupenda kiukweli kutoka moyoni,ambayo ni nadra sana kutokea,anatamani awe na control,ambayo ni nature...Control over you in terms of Ownership...Akumiliki peke yake...Na kama amekupenda,akatamani akumiliki,halafu wewe ukashare milki yake,kitu kitakachotokea hapo ni hasira ya Usaliti uliotukuka sana ambao huwa hauponi kirahisi..Si kwa kupenda ila ni nature...Naturally,Mwanaume kugeuzwa fala ni Abomination kubwa sana..Hata ikitokea miaka 20 iliyopita,haiponi haraka.Msiwalaumu wanaume,haiponi haraka na kila siku,na kila saa ataingia in Love with the notion of what happened,hataamini tena katika kumpa Mwanamke moyo wake...Na hapo ndipo shida inapoanzia,hatajali...Ukiumia au Usiumie kwake yeye ni sawa coz Moyo wake hauko 100% invested so hes in his comfort zone.

2. HISTORICAL REASONS

Wanaume kihistoria huwa wanakuwa na mahusiano mengi kuliko wanawake..Wanawake huwa wana sense of shame kwenye idadi ya wanaume wanaolala nao(with exception to bitches who dont care)...So kwa Mwanaume kuwa na listi ya wanawake 15 ni kawaida,wakati Mwanamke akifikisha 6 nafsi inamsuta kwamba sasa anajaza kontena...

Hii imewafanya wanaume kuwa exposed na mambo mengi sana kuhusu Mapenzi kuliko wanawake....In 5 years,Mwanaume anaweza kuwa na mahusiano na Wanawake hata 10...KAtika hawa 10,kila mmoja alikuja na rangi yake...Huyu anamtenda kwa style hii...Huyu style ile...So in 10 girls,anakuwa amewajua Wanawake vizuri na all types...Akija kwako wewe Mwanamke wala anakuwa sio mgeni,ukifanya jambo anarecall nyuma kwamba kilipotokea hicho Something happened...Na kwa Mwanaume kama alitendwa kwa style hiyo 5 years back na mtu,halafu wewe unakuja kumfanyia remix leo,usitegemee huyo atakuwa na huruma na wewe...NEVER! Atajua whats next na hatojali kukupush hadi wewe unapotaka kufika,hata kwa fork-lift

In general,Mwanaume aliyeumizwa kamwe hatajali kwa sababu ataona wanawake wote ni sawa,which is not true,lakini Wanawake,epecially wa siku hizi mmekuwa Chronic,hamtabiriki kama Mvua za Dar,muda wowote zinanyesha bila Mamlaka ya Hali ya hewa kutrace your occurence,so wanaume wamejitune..Anytime wako Standby kama FFU na Maandamano ya Chadema,na hapa ndipo Wanawake wengi wanapoumizwa.Wengine ni wema tu lakini mmekumbana na Wanaume waliopokea visago ambavyo kupona kwake ni kwa neema ya Mungu,usipoweza kumtibu vizuri basi utaumia tu,na wengi wenu hamna muda wa kuwajua boyfriends zenu,mko bize kuomba hela za Mawigi tu....

3.MAMBO WANAYOYAONA

Wanaume wanashuhudia vituko kila kukicha kwa marafiki,na ndugu zao wa kiume wanavyofanyiwa na wanajiuliza maswali mengi sana...Wameona rafiki zao wa karibu walivyotendwa baada ya kutendwa na jinsi inavyopain,na wengine hata wamejiua au wamekuta wakiua bila kukusudia kwa uchungu uliowapata.

Hii inatoa alarm na Warning kwao kwamba kuwapenda Wanawake ni kitu hatari sana...Haya yanatokea kila siku na kila leo

USHAURI KWA WANAWAKE

Unapoingia in love,kama umeingia nae inlove for future,find time kumjua huyo Mwanaume yukoje...Ametoka wapi...nini kilimsibu...Na Je,utawezaje kumsaidia kuiondoa negative notion..Usiassume Mwanaume uliyempata ni bikira kwamba atafall in Love....Watu wamegongwa sana huko nyuma,wanaumwa Love Concussion...Ukimchukua tu uakanza nae mahaba na mizinga juu hutajua wapi moyo wake uliumizwa,ur future dreams will die,I guarantee you...Find time umjue Mwanaume wako,Wanaume wengi wameumizwa huko nyuma na vidonda vya Wanaume haviponi kirahisi kama vyenu...Wanawake ni rahisi kusahau vitu,Wanaume sio..inawezachukua zaidi ya Miaka 10 kupona na mpaka apate daktari sahihi.Je, Wewe ni mwanamke daktari sahihi kumtibu ili ujenge family??Kama sio my dear ur finished.

USHAURI KWA WANAUME

Sio kweli kwamba Wanawake wote ni sawa,ingawa percentage wise,wengi wanafanana...Nao wametendwa pia so siku hizi nao wamekaa standby...Find muda kumjua Mwanamke wako ni wa aina gani...Msaidie kama nae ana matatizo,if she is a visionary girl tafuteni where ur interests lie,mjenge familia...Sio vema kumjudge Mwanamke kwamba she is all the same kama wengine,wengine mioyo yao ni Mitakatifu kuliko Papa wa Vatican...

ASANTENI!