Thursday, June 13, 2013

ANGALIA VIDEO HII...SIKILIZA MAUDHUI YA WIMBO HUU,UTAKUBALI KWAMBA CHRISTIAN BELLA NI RAISI WA MASAUTI

Kwa Wale Wapenzi wa Muziki wa Bendi nchini Tanzania,Jina la Christian Bella sio jina geni kwenu...Yes,anafahamika kama RAISI WA MASAUTI na ni mmoja kati ya Waimbaji ninaowakubali mno..He is very UniqueChristian Bella aliifanya Bendi ambayo haikuwa na jina lolote kuwa ON TOP kwa miaka yote aliyokaa pale...AKUDO....Kila mtu aliifahamu AKUDO na ilipata Wapenzi wengi sana hata kufikia hatua ya kutaka kuwapoteza kabisa kwenye ramani wapinzani wao wakuu waliokuwa wakishikilia chati, FM ACADEMIA.

Shukrani zimuendee rafiki yangu,Mtaalamu wa kutafuta Vipaji,King Dodoo kwa kumleta Christian Bella nchini Tanzania na kuisaidia sana Bendi hii kuwa kwenye Chati iliyo mpaka sasa...

Kwa sasa Christian Bella amehamishia makazi yake nchini SWEDEN na tangu alipokwenda huko amekuwa kimya na watu wakahoji kwanini na wengine kwenda mbali kufikia kudhani amekufa kisanii..LA HASHA....Simba hata azeeke namna gani hawezi kuwa nyau...Raisi wa Masauti amewadhihirishia Watanzania na mashabiki wake kwamba yuko fit baada ya kuachia Bonge moja la VIDEO alilofanyia Shooting STockholm,Sweden,na ukisikiliza maudhui ya Wimbo huu pamoja na Quality ya Video hii utakubali kwamba Christian Bella hana mpinzani na ndiye RAISI WA MASAUTI....PAmoja na kwenda nje hajawasahau wadau wake,amewarusha washkaji zake na mara kwa mara utasikia akimtaja Ustaadh Juma na Musoma kwenye wimbo huu unaoitwa MSALITI

Bonyeza Link hii uangalie Video yake mpya kabisa na utakubali Bella ni mkali wa wakali kwenye nyimbo za mahadhi ya Lingala ...Twende Kazi ...

BOFYA
http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=GytZVSdluF8#!

No comments:

Post a Comment