Thursday, June 13, 2013

NYUMBA ANAYOISHI BILL GATES...HATARI,WEKA MBALI NA WATOTO


Wakati wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga na unawaza lini utaiba kazini au kujichanga kwa njia halali zisizotosha kuweza kuanza Ujenzi,hali ni tofauti kabisaaaaaa na ndugu anaitwa BILL GATES,ambaye ni tajiri namba 3 duniani akiwa nyuma ya Carlos Slim na Warren Buffet.

Yeye amehama kutoka kuishi nyumba za ardhini na ameamua kutengeneza nyumba baharini,katikati ya maji,Nyumba inayoelea....Hela iliyotumika kutengeneza HOME IN THE OCEAN inafikia Dola Bilioni 1.4 ambayo ni sawa na karibu trilioni 3 za Tanzania...trilioni 3 ni Bajeti ya Tanzani Kwa Mwaka mzima kwa Wizara zote za Serikali inayotoka mfukoni kwetu kabla ya Wahisani....Jamaa kaamua kutengeneza Yacht yenye Nyumba

Chukua Muda wako uangalie WATU WANAOISHI...Maana sisi wengine tupo tupo tu...

HAYA MZIGO HUU HAPA BOFYA http://www.youtube.com/watch?v=uBrCZs3_G9k

HISTORIA YA HUYU JAMAA KWA KIFUPI TU:

Amezaliwa mwaka 1955 huko Seattle,Marekani akiitwa William Henry Gates III,babake ni Attorney kwenye jiji la Seattle na Marehemu mama yake alikuwa Mwalimu tu wa kawaida wa shule

Alianza kupenda mambo ya Kompyuta na Programming akiwa na miaka 13 tu...

Mwaka 1973 alijiunga na chuo kikuu cha Havard na mwaka 1975 kabla tu ya kuhitimu Masomo aliacha chuo akaamua kuunda Microsoft Company akiwa na mshkaji wake Paul Allen.

KAZI NI KWAKO..UKIACHA CHUO KISA JAMAA ALIACHA INAKULA KWAKO

No comments:

Post a Comment