Saturday, January 14, 2012

FACE BOOK HUSBAND AND WIFE!!!


Kuja Facebook kutafuta Mke au Mme ni sawa na kwenda stendi ya Mwananyamala na kumuomba mpiga debe Business Card yake,sanasana atakuchana na viwembe tu...Tangu nijiunge humu nimesikia,tena kusikia tu sijaona wala kuthibitisha,ndoa 1 tu.nadhani wale jamaa walijoin kwa nia hiyo ndo maana wakaoana..Kuna vimeo humu vimetangaza ndoa kama elfu 92 ss sijui ndugu zangu mna vidole vya ndoa vingi kama mikono ya Pweza!Kazi mnayo wadada mlio desperate na ndoa,Mnafall in love na Profile pictures,ukikutana na mtu amekomaa kama Nguzo za Tanesco za Kigogo Luhanga....

THE WORD "SORRY"
Hamna neno rahisi lakini gumu kwa Mwanaume kama neno Iam Sorry..Atakosea lakini atataka ajaladie weee msala umuangukie mamsap,madai huo ndo ukidume..Hii ni siri vijana wangu,Neno Sorry lina uwezo wa kuyeyusha barafu ya hasira iliyojaa kama mlima everest kwenye moyo wa mwanamke kwa spidi ya Light kuliko masentensi laki 2 na 70 unayojaribu kutetea kosa.Ukisema wala hupungukiwi nguvu za kiume hata lita 2 na wala size ya nanii haipungui.Learn to say Iam sorry when ur wrong,.Hapo vipi wanaume,na nyie mtaniblock kama ile jinsia nyingine?ngoja nisubiri nione!

WANAWAKE MSIDANGANYIKE NA WANAUME KULIA MACHOZI

MTU MZIMA AKILILIA PENZI


Wanawake msidanganyike na machozi,Mwanaume kulia machozi ili ajiongezee pointi za kukupata ni rahisi tu,anakuja amejikoki mwananhu,anavuta taswira ya shangazi yake aliyempenda amekufa mwaka jana kwa ajali,atatoa chozi hilo na kamasi juu kama mnyakyusa wa tukuyu.halafu ulivyo juha We unaenda kujisifia kwa mashosti yule mkaka ameliaaa kweli ananipenda,kumbe umelamba Joker.Watu tuna machozi yetu hapa usipime...msiniulize mtawatambuaje,kazi kwenu tembeeni na pima maji kama fundi mwashi!

RELATIONSHIP BILA COMMUNICATION NIKA GARI BILA ENGINE.......

GARI BILA ENGINE
 
Gari bila engine ni kama kasha la penseli tu tupa kule,Relationship bila Communication mtabaki jina tu kwamba mlikuwepo.Unapuuzia simple things kama Gudmorning msg/call,maneno kama Pole na kazi/shule,neno am sorry baby,neno i miss u.Kama una alergy na haya maneno nani kakuambia upite Love Street?huo mtaa unahitaji sanaa,care na muda.Kumjulia hali mpenzi imekuwa uasi kama Maandamano ya chadema.Simu unayo,how many seconds zinakuchukua kumwambia mpenzi i miss you au kujibu meseji zake?Unajifanya bize na kazi eeh basi Muoe Boss wako

ONGEZEKO LA WANAWAKE KUVUTA SIGARA NAKUNYWA POMBE

A GIRL DRINKING BEER
A GIRL SMOKING
Kuna ongezeko kubwa sana la wadada wanaokunywa Pombe na kusmoke kwa sasa..Najiuliza,wamependa au kuna force ya Wanaume wanaowa-date kuwa-influence kuwa kama wao? Msipende kuiga tu,mwili wa mwanamke ni kama ua,ukilipigisha mzigo juani kesho halipendezi tena,na haya machips mnayokula mnakuwa na shape hazieleweki,mnazeeka mnakuwa na matumbo kama Biringanya iliyoivishwa na jua...Nani aoe nyie?Mke chapombe na Mme chapombe??watoto si watakuwa wanauza Chang'aa...Hawa maboyfriends wanawaendesha kama punda,wanawaharibu halafu baada ya muda ur dumped,ushajiishia,mnaanza kudandia kutafuta waume wa kuoa?Be urself,hatuoi biringanya sisi JITUNZENI

Tuesday, January 10, 2012

KUMJALI MPENZI WAKO NI MUHIMU


Ukijaliwa mpenzi anayekupenda kwa dhati na kwa moyo wote usimfanyie vituko kum-dissapoint bila sababu akajuta kuwa na boya kama wewe,kama unashindwa kumjali waachie wenye uwezo na mahaba ya kisukuma wampe raha.Si vema kung'ang'ania udongo wenye rutuba kama huwezi kulima jamani,kama huwezi waachie wenye nguvu na majembe imara walime wewe nenda singida kwenye ukame ukasubirie type zako za ki-ukame ukame zitavumilia coz na zenyewe zina mishemishe kama sime ya mmasai.Kama umeelewa comment,kama hujaelewa uliza tu,kama umenuna nauza nyembe njoo ununue umeze-Seth School Of thought