Wednesday, February 15, 2012

Hii ni kwa wale ambao wanadhani maisha ni rehearsalHii ni kwa wale ambao wanadhani maisha ni rehearsal...Maisha hayana rewind Button...mmekazana kutafuta kudate masistaduu,wanaojua kupiga kiatu njano,hereni njano,pochi njano na lipstick njano...Uko busy kudate na msanii wa filamu,jeans inaning'inia hadi kwenye mstari wa Ikweta,msanii katoa hit unajilengesha,unatokea kwenye wimbo hulipwi hata thumni unaona dili...Unapata watu wa maana unaona hawanajina,hawana hela za kukupeleka Savanna,utakula savanna all ur life?Watoto wako watasoma Savanna lounge au Maisha Club.Its high time u think,5years from now where will u be?utaendelea kumatch mabegi ya njano na kucha za njano?utaendelea kuvaa mlegezo na kudundika kama una mafindofindo kwenye ugoko?Maisha hayakusubiri,ukipishana nayo sasa hutakutana nayo Chalinze-Seth School Of Thought

Tuesday, February 14, 2012

Hujampenda mtu mwaka mzima leo ndo unajishaua na kadi na maua,wizi huo


Hii siku bwana imekaa kichokozi sana..haina dili lolote ila unalazimika tu kufanya dili ili uonekane nawe umo..hujampenda mtu mwaka mzima leo ndo unajishaua na kadi na maua,wizi tu!Leo watu watakopiwa meseji zinaitwa SEND TO MANY,itatumwa kwa watu kama 70 na wote wataitwa honey..na ulivyo boya wewe utaipoke utahisi ur special kumbe ni mtu wa 69 kuwa delivery report..nawashauri hii siku muikaushie tu lasivyo itawaumiza kichwa,na wengi mtagombana kisa jumanne ya tarehe 14..ni ushauri tu!

Mapenzi na Ujinga ni Bestfriends-Huwezi kuinjoi penzi la kweli kama wewe sio mjinga,huwezi kudumu kwenye relationship kama wewe sio mjinga

Mapenzi na Ujinga ni Bestfriends wanaopendana sana,huwezi kuwatenganisha,wanaenda kulala wote,wanaenda shopping pamoja,wanashara hadi mswaki..Huwezi kuinjoi penzi la kweli kama wewe sio mjinga,huwezi kudumu kwenye relationship kama wewe sio mjinga,wakati mwingine wapenzi wanafanya makosa makubwa ila unasamehe ili penzi liendelee japo usingependa kusamehe hilo kosa,ujinga umefanya kazi yake...Bila kuwa mjinga ndugu zangu mapenzi hayaendi,usipoletewa zawadi Valentine,usipotafutwa na mpenzi,kuwa tu mjinga yatapita,ikifika tarehe 15 penzi lako linarejea...Habari zenu wajinga wenzangu,hope mnaendelea vema leo,endeleeni hivyohivyo,msipokuwa wajinga kila siku mtakuwa Single asikwambie mtu kuwa single inataka uwe na moyo wa bati la south Africa.

Msichana akikwambia Leave me alone,you are not my type i love someone else usimlazimisheKuna wanaume huwa hamuelewi Kiswahili...Msichana akikwambia Leave me alone,you are not my type i love someone else usimlazimishe kamwe,ameongea la moyoni,hata kama unahisi una kila kitu,hela na uwezo,hutamuweza..moyo wake uko sehemu nyingine ambayo ni unstoppable.Hutaweza kamwe kumlinda,hata ukijifanya wewe John Cena kumpeleka kila mahali kumlinda asiibiwe,kazi bure.Utampeleka salon Masaki na Hammer atakwambia anaset nywele 1hour,ukimuacha salon ye anapanda bajaj anaenda kwa Yalaiti wake Kwa Mtogoleee anamwimbisha pambio weeee anarudi anakukol honey tayari,na ulivyo bumunda unaenda kumchukua unahisi umewini kumbe ushapigwa tobo na afande kipepe saa nyingi...Ukiambiwa wewe ni mkasi using'ang'anie kufanya kazi za Bisibisi,utapinda bure kwa nati usiyoweza kuifungua-Seth School Of thought

Uko bize unalalamika ooh mi sina bahati ya kupendwaUko bize unalalamika ooh mi sina bahati ya kupendwa..Wakati kuna mtu alikupenda very seriously we ukamchukulia poa ukajifanya selective,unatafuta hips madai yako...imekula kwako...Walikuja watu vere siriaz ukawatazama,ukawapandisha ukawashusha,hadi wakaishiwa pozi,maana wadada wanaweza wakakupa jicho hilo hadi ukajihisi uesahau kufunga zipu ya suruali...Madai yako unataka handsome,mwenye gari na nyumba..Mahandsome wamekata kamba,wanakuja wenye Vichogo virefu tu,huwataki,imekula kwako....Maamuzi yako ya leo yana athari kubwa sana in future,usifanye maamuzi feki sasa ukategemea future yako itakuwa Original,feki inazaa feki,na Original inazaa original,Mchina hauwezi kuzaa Blackberry