Thursday, June 13, 2013

NYUMBA ANAYOISHI BILL GATES...HATARI,WEKA MBALI NA WATOTO


Wakati wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga na unawaza lini utaiba kazini au kujichanga kwa njia halali zisizotosha kuweza kuanza Ujenzi,hali ni tofauti kabisaaaaaa na ndugu anaitwa BILL GATES,ambaye ni tajiri namba 3 duniani akiwa nyuma ya Carlos Slim na Warren Buffet.

Yeye amehama kutoka kuishi nyumba za ardhini na ameamua kutengeneza nyumba baharini,katikati ya maji,Nyumba inayoelea....



Hela iliyotumika kutengeneza HOME IN THE OCEAN inafikia Dola Bilioni 1.4 ambayo ni sawa na karibu trilioni 3 za Tanzania...trilioni 3 ni Bajeti ya Tanzani Kwa Mwaka mzima kwa Wizara zote za Serikali inayotoka mfukoni kwetu kabla ya Wahisani....Jamaa kaamua kutengeneza Yacht yenye Nyumba

Chukua Muda wako uangalie WATU WANAOISHI...Maana sisi wengine tupo tupo tu...

HAYA MZIGO HUU HAPA BOFYA http://www.youtube.com/watch?v=uBrCZs3_G9k

HISTORIA YA HUYU JAMAA KWA KIFUPI TU:

Amezaliwa mwaka 1955 huko Seattle,Marekani akiitwa William Henry Gates III,babake ni Attorney kwenye jiji la Seattle na Marehemu mama yake alikuwa Mwalimu tu wa kawaida wa shule

Alianza kupenda mambo ya Kompyuta na Programming akiwa na miaka 13 tu...

Mwaka 1973 alijiunga na chuo kikuu cha Havard na mwaka 1975 kabla tu ya kuhitimu Masomo aliacha chuo akaamua kuunda Microsoft Company akiwa na mshkaji wake Paul Allen.

KAZI NI KWAKO..UKIACHA CHUO KISA JAMAA ALIACHA INAKULA KWAKO

ANGALIA VIDEO HII...SIKILIZA MAUDHUI YA WIMBO HUU,UTAKUBALI KWAMBA CHRISTIAN BELLA NI RAISI WA MASAUTI

Kwa Wale Wapenzi wa Muziki wa Bendi nchini Tanzania,Jina la Christian Bella sio jina geni kwenu...Yes,anafahamika kama RAISI WA MASAUTI na ni mmoja kati ya Waimbaji ninaowakubali mno..He is very Unique



Christian Bella aliifanya Bendi ambayo haikuwa na jina lolote kuwa ON TOP kwa miaka yote aliyokaa pale...AKUDO....Kila mtu aliifahamu AKUDO na ilipata Wapenzi wengi sana hata kufikia hatua ya kutaka kuwapoteza kabisa kwenye ramani wapinzani wao wakuu waliokuwa wakishikilia chati, FM ACADEMIA.

Shukrani zimuendee rafiki yangu,Mtaalamu wa kutafuta Vipaji,King Dodoo kwa kumleta Christian Bella nchini Tanzania na kuisaidia sana Bendi hii kuwa kwenye Chati iliyo mpaka sasa...

Kwa sasa Christian Bella amehamishia makazi yake nchini SWEDEN na tangu alipokwenda huko amekuwa kimya na watu wakahoji kwanini na wengine kwenda mbali kufikia kudhani amekufa kisanii..LA HASHA....Simba hata azeeke namna gani hawezi kuwa nyau...Raisi wa Masauti amewadhihirishia Watanzania na mashabiki wake kwamba yuko fit baada ya kuachia Bonge moja la VIDEO alilofanyia Shooting STockholm,Sweden,na ukisikiliza maudhui ya Wimbo huu pamoja na Quality ya Video hii utakubali kwamba Christian Bella hana mpinzani na ndiye RAISI WA MASAUTI....PAmoja na kwenda nje hajawasahau wadau wake,amewarusha washkaji zake na mara kwa mara utasikia akimtaja Ustaadh Juma na Musoma kwenye wimbo huu unaoitwa MSALITI

Bonyeza Link hii uangalie Video yake mpya kabisa na utakubali Bella ni mkali wa wakali kwenye nyimbo za mahadhi ya Lingala ...Twende Kazi ...

BOFYA
http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=GytZVSdluF8#!