Saturday, June 30, 2012

AINA ZA WANAWAKE AMBAO WANAUME WANAPENDA

Sometimes Wanawake huwa wanajiuliza Maswali mengi,wafanyeje ili wapendwe,wanahisi wana bahati mbaya,kila wanapojitoa mioyo yao inaumizwa.Jamaa hawakai,wanatupia kitu,wanakula mzigo wanatembea na Bwana..Mioyo yao imejaa matundu na hawaamini kabisa kama Wanaume huwa wanapenda,imefikia point wanadhani Wanaume hutamani tu kumbe SI KWELI!


Wanaume nao wana taste zao,hawaendi tu kama Mbwa koko,jalala moja baada ya jingine,HAPANA...Know their taste and you will enjoy theirs.

Sifa za Mwanamke ambae Mwanaume atavutiwa na kukaa ni hizi zifuatazo,JITAZAME,kama huna any of these,you better try to learn to have them,its not too late:

1.MWANAMKE MWENYE MSIMAMO
Jambo moja muhimu,the number 1 thing ambacho Mwanaume anaangalia kwa Mwanamke ni Msimamo wako...Sio Mwanamke uko kama Feni,kila sehemu unapulizia upepo,Mashariki,Magharibi kote wewe...Hapo sahau,tena sahau sana.Mwanaume anahitaji kuwa na uhakika,Mwanamke aliyemkabidhi moyo hana mishemishe na hayumbishwi na lolote,na chochote na penzi lake liko safe

Unaweza kuwa na kila kitu,Mzuri wa Sura na kila kituuuu,na bado usimpate Mwanaume wa Maana kama huna sifa hii,hakuna muujiza kwenye hili,ndo wanaume walivyoumbwa,if you lack this hamna Mwanaume wa Maana utapata,utapata vimeo kama ulivyo!

2.MWANAMKE MUELEWA

Men are simple creatures,they love to live simple,and take them simple as they are...

Ukiwa aina ya Mwanamke unamind vitu...kitu kidogo ugomvi...Unaongea na nani...Uko wapi..Na nani,Kwanini,hee,jamani kama Mahaakama kuu??Hapa unapoteza Credits

Kuwa aina ya Mwanamke muelewa ambae utamfanya Mwanaume ajisikie vibaya kufanya kitu flani ambacho ulishamwambia asifanye before...Lakini sio kukaripia na kununa kwa sababu amerudia..let him realize that amefanya kitu cha kukuudhi na hujareact,and if hes a man enough,he will know and apologize

Ila kama ni gumegume basi tena,litakausha na ndo inakuwa issue hapo...Are u patient enough to handle it??kazi kwako,ila kuna wanawake wana uwezo huu,learn from them wamewezaje..No matter how complicated the man is,they know how to handle him

Jua Lugha ya kutumia ambayo utafikisha ujumbe and yet you dont show him kwamba umemind na unamkaripia...kumkaripia Mwanaume ni msala mpya,hata kama ana kosa atakumind na itakula kwako...Una ulimi mzuri kufikisha ujumbe??

3.MWANAMKE DIRECTOR

Baba ni kichwa cha nyumba....mimi huamini Mama ni macho yaliyo kwenye kichwa hicho

Women play a very vital role in DIRECTING THE HEAD TO THE RIGHT WAY

Kichwa bila macho si utajigonga tu????Mwanamke ni jicho...

Ukikalia kujiremba tu na kuwaza mambo mengine bila kujua kuna kichwa kinasubiri maelekezo yako,utaonekana bogus..kutwa uko kwenye Umbea,huna muda wa kujua ur man anafanya nini,ana plan gani mwaka huo,unamsaidiaje kuzifikia,sasa we faida yako nini kwenye maisha yake??

be the kind of a woman ambae Mwanaume aki-achieve jambo anasema I have a woman beside of me who engineered this...Kama hujawahi kufikia hatua ya kuwa appreciated na ur man kwa jambo hili jua kuna mahali umefeli...Na hili haliji hivihivi,linakuja pale kunapokuwa na proper communication between you and ur man...Bila good communication:
 1.Hutajua what ur man is up to
 2.Kwa sababu hujui what he is up to hutakuwa na msaada.
 3.Akifaulu,jua haupo kwenye picha ya mafanikio yake na ur simply useless
 4.Akifeli,ur part of his failure kwamba humsaidii lolote..ur simply useless and actually absent in his life kwa sababu uwepo wako haumsaidii its better he becomes alone!YOU HEARD???

Women have planning and control ability,USE IT...Usikae tu kama muuza genge unasubiri wateja,Do your job and Win him!

4.MWANAMKE MSAFI NA MZURI

Usafi huu sio wa nguo tu na kunukia,ni zaidi ya hilo...

Usafi unaanzia ndani..Msaidie Mwanaume awe msafi pia,rohoni hadi mwilini...Rohoni how???Jitu halisali,halikumbuki kuna Mungu,lipo tu,unadhani mtajenga Familia gani baadae???

Msaidie kum-remind kukumbuka hilo,Mafanikio ya nje huanzia ndani..Dirty inside,Dirty Outside...Mambo mengine anafanya nje na yanaku-affect kwa sababu umefeli ku-inspire change ya ndani...Ngumu hii lakini ndo hivyo..You can save a lot of energy kama atakuwa msafi wa ndani,everything outside will be set automatically...Whatever u see in physical started in Spiritual...Yeah right! Hata ulimwengu uliumbwa,na vyote unavyoviona baada ya Plan ya Spirit kumalizaika.Soma Kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia,uone Uumbaji ulifanyikaje...Same applies na hapa,Uumbaji wa vitu vya nje,Mahusiano imara,Familia bora,inajengwa ndani..

Sio kazi yako ni kuuliza Baby hatuendi Club,Baby this...Unamkumbusha kusali???Utatengeneza mme freemason bila kujua...Mtu hasali we upo tu unaona sawa...CHANGE!

Huu usafi mwingine wanawake mmejaliwa,biashara za kunuka kikwapa no,Kusafisha nyumba vema saafiii...mengine si kama kawa??Mpango mzima uko hapo.

Uzuri huwa ni subjective...Unaweza kuwa mzuri kwangu lakini ni wa kawaida kabisa kwa mwingine....Ukiwa msafi unaweza ukamfanya Man wako aone potential,hata kama wewe sio mzuri sana lakini anaona Kiongozi wa Familia inside you and he will definitely opt you.

Hamna limbwata wala nini,tupa kule mbali...

Kama huna hizi sifa 4,aisee waza upya...Unaweza bahatisha ndulute ukaolewa,lakini jusitegemee muujiza,goma litapata Pancha tu...Jamaa hataweza kukaa na nunda...Atajutia Mahari aliyolipa ila atasepa kimyakimya..

To avoid that,please make sure you do your Homework well ili Mtihani ukija unafaulu tu bila shida...

Jitathmini halafu KAA HUMO!

Thursday, June 28, 2012

ILI UPATE MME/MKE MWEMA,KWANZA WEWE UWE MWEMA LASIVYO HUPATI

Kamwe huwezi kuingia kuchat Twitter na Nokia ya Tochi,unahitaji smartphone ili uweze kufanya hivyo...

 Hakuna Mmachame anayezikwa Dar makaburi ya Kinondoni,labda hana ndugu Machame wote wanazikwa Moshi,huo ni utamaduni..Huhitaji kuwa genius kujua hilo.

 Unapokuwa busy kutafuta Husband material na kujishaua unataka kuolewa na kwamba huna bahati,jiulize kwanza unaoleka wewe,are you a wife material???
 
Kabla ya kutafuta mme jiulize kama una sifa za kuwa mke wa mtu,ndoa sio kama vinyweleo kila mtu anavyo.Kama huna sifa ya nunua tu midoli ujikumbatie tu maana hutapata. be that best person that someone will see the best qualities in you first...Huwezi kuwa mfinyanzi halafu unatafuta udongo wa kichanga ujenge

 Unapotafuta wife material na kujishebedua jiulize kwanza una hadhi ya kuwa mme wa mtu wewe,are u a husband material??Unayaweza majukumu au unadhani kuwa na misuli na ndevu ndo una-qualify kuwa mme?
Kama wewe huna sifa za mke/mme bora tafuta kwanza sifa hizo kabla hujatusumbua na kelele kwamba ur looking for hubby/wife material.be the material that you are looking to have na ndoa itakuwa automatic maana tabia zako zitaongea na si maneno na kelele kama debe tupu
 
Tumekuwa na tabia mbaya halafu tunatafuta watu wema tuwaweke ndani,nani anataka uwe kichaka chake cha kuficha uhuni wako??Everyone deserves a better wife and a better husband lasivyo utatesa au kuteseka tu.
 
Huwezi kwenda Mbinguni kwa kupanda basi la Kariakoo...Njia ya kwenda mbinguni ni kuokoka tu,FULL STOP,bila hivyo mbingu utaisikia kwenye hadithi za Sunday school

Wednesday, June 27, 2012

WEMA SEPETU ANAJIANDAA NA HARUSI

Wiki nzima iliyopita amehit kwenye Blogs,Magazeti,na kila mahali baada ya kumleta mwanadada Staa wa Nollywood, Omotola Jelade kwenye uzinduzi wa Movie yake mpya iitwayo SUPERSTAR pale Giraffe Hotel.Ilionekana kama haiwezekani ila ndo hivyo...Mdada akatua

Katika hali iliyowashtua wengi,Leo,Mwanadada ambae daima yuko kwenye Magazeti, Wema Isaac Sepetu ametoa taarifa kwamba anajiandaa na harusi.

Wema yuko bize akiwaza aina gani ya gauni litamfaa na ameshaomba ushauri kwa watu kadhaa kuhusu choice ya nguo hiyo muhimu

Kwenye page yake ya Twitter,ameandika hili ingawa watu wengi hawakuamini na walimuuliza maswali kadha wa kadha awahakikishie kama ni kweli au ni Movie naye bila hiyana akawaambia ITS FOR REAL

CHEKI TWEET YAKE HAPA CHINI-FOR YOUR INFORMATION,USIPOAMINI HAIYAH ILA NDO HIVYO SASA...DADA HUYOOOOOOO ANAOLEWA!ILA MAHARI BADO

HIVI NDIVYO DK ULIMBOKA ALIVYOTEKWA-KAMANDA KOVA

Akizungumza na waandishi wa Habari Mchana huu, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema Dk Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana akiwa Leaders Club akinywa pombe, pale Kinondoni


Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo.


Dokta Ulimboka aliokotwa katika msitu wa Mabwepande na msamaria mwema aliweza  kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo

WAANDISHI WA HABARI WAKIMSIKILIZA KAMANDA KOVA


KAMANDA KOVA AKIONGEA NA WAANDISHI MCHANA HUU


Hii ndio hali ya dokta Ulimboka alipofikishwa Muhimbili Hospital.Inatisha aisee kama Tanzania tumefikia hali hii,amani iko wapi!
HAPA AKIWA NA WAZIRI MKUU PINDA..NA MIKONO WAKASHIKANADokta Ulimboka akionekana pichani wakati wakiwa kwenye mgomo wao wa mara ya kwanza na madaktari wenzake

Tuesday, June 26, 2012

ABIRIA ALAZIMISHWA KUKAA NA MAITI KWENYE KENYA AIRWAYS


Africa kuna mambo sana aisee.hii imetokea juzi tu hapa,Mwanamke mmoja raia wa Sweden alikuwa akisafiri kuja Tanzania kwenye Likizo yake kwa ndege ya KENYA AIRWAYSAkielezea tukio hilo,mwanamke huyo anasema jamaa huyo aliyekaa nae alipandia ndege kwenye uwanja wa ndege wa Amsterdam.

Mshkaji alikuwa anaumwa na alionekana akitokwa na jasho jingi sana na kuchechemea,lakini alilazimisha kusafiri.

Muda mfupi tu baada ya Safari kuanza yule abiria alionekana kuzidiwa zaidi na wahudumu walijitahidi kuwa karibu nae muda wote lakini Izraili alionyesha Umafia wake wa ku-operate hadi angani,yule jamaa aliaga dunia wakiwa katikati ya Safari.

Mwanamke yule kuona vile ikabidi aombe kubadilishiwa Siti lakini kwa Mshangao akajibiwa kuwa ndege imejaa na hakuna popote wanaweza kumpeleka zaidi ya yeye kukaa palepale na ile maiti.

Masaa karibu 10 yule mwanamke alisafiri akiwa amepoze na ile maiti just next seat.

Mawanamke huyo,Lena Petterson,alipofika Dar es Salaam aliuandikia uongozi wa kenya Airways kulalamikia ishu hiyo na ndipo Uongozi ulipoamua kumrudishia Nusu ya Nauli yake kama part ya kumpoza moyo Mwanamama huyo.

Nauli aliyolipa Mwanamama Lena Petterson ilikuwa Dola 1400 na alirudishiwa Dola 700 kama Compensation kwa yeye kukalisha siti moja na Maiti na Mwanamama huyo alikubali Fidia hiyo na kuwa mpole.

Sasa kama hiyo ni Kenya Airways,ambao wako very smart kwenye operation zao,Usishangae Air Tanzania ukiambiwa ukae na Magunia ya Viazi uyapakate tena kwenye Siti,sitashangaa!

Monday, June 25, 2012

NAHISI NICKI MINAJ NI MPARE..HII SIO KAWAIDA

Ndio maana siku hizi wadada wa kibongo nao wanafanya hii mambo...Ulaya na Marekani haya mambo yamekuwa kawaida kabisa.

Huyu anaitwa Nicki Minaj ambae mimi nahisi ni Mpare...wanawake wa kipare wanafahamika kwa sifa ya kuwa na Good shapes...Kama kweli anavyoonekana sasa hajafanya mchanganuo wowote ule katika kuongeza maujuzi,ama kwa hakika tusibishane,Nicki ni MPARE!

Tumezoe wazungu ni wembamba na Sony Wega nyuma...sasa huyu inakuwaje??

Kila mwaka akipigwa picha anaonekana duh...

Watu wamekuwa wanasuspect kwamba maybe Nicki huwa anafanya Surgery ya body parts...Lakini yeye mwenyewe akihojiwa mara kadhaa amekanusha hilo na kusema hawezi kuwazuia watu kuongea,na anapenda kuwa centre of attention ila ule mzigo kapewa na mama.

Swali ni Je,mbona ngoma imekua ghafla yaani,kama Graph ya demand and Supply bana....

Hebu tuangalie halafu tukubaliane,ni Surgery au Nicki ni Mpare???

MCHEKI NIKI BEFORE,MWAKA 2010 TU HAPO

HATISHI KIIVYO,HII HATA WACHAGA WANAYO


CHEKI...KAWAIDA TU YAANI


ANGALAU INGEBAKIA HIVI,MASWALI SI SAAANAAA
 CHEKI SHUGHULI YAKE SASA HIVI..GHAFLA BIN VUU KAMA ALIVYODAKWA NA WADAKUDUUUUHHHH..IMAGINE

 ULALAH FUNDI KALALAH


SASA HII NDO CURRENT,YA JUZI TU AMBAYO WADAU WANASEMA AMEFANYA SURGERY YA 3....WHATS THIS FOR ANYWAYS???WADADA WANAJUA ZAIDI


SIRI YA PUMZI KATIKA KUENJOY MAPENZI

Sijui nianzie wapi! Topic tete...TUTAPONA TU MDOGO MDOGO


Kwanza, Kuna wanaume ambao Wanawake wao wanalalamika,jamaa wako fasta kuinua mashabiki..Dakika 10 nyingi watu Yangaaaa Yangaaaaa....Washafunga Mahesabu....Ndo kwanza mpenzi anapanda Kilima wewe huyoooo unatiririkaaaaa...Inaudhi na kukera sana,na sometimes,jamaa linajifanya linajuaaaaaaaaaa hadi huwezi hata kuliambia,maana ukiliambia ugomvi...ooh unaleta mambo ya ajabu utakuwa ushapata mtu mwingine...


Ah ah,kama unakosea utaambiwa tu...Jifunze tufaidi wote..Raha ya Mechi ya mpira wa miguu ni magoli,ila Raha ya Mechi hii huwa ni Raha kwa wote...Waingereza wanasema Pleasure for Both....Tiririka muda muafaka.


Upande wa Pili...Kuna Wanawake,Amini usiamini,wamezoeshwa aina flani ya Mapenzi ambayo hawatiririki ng'oo...Wameingia kwenye huu ulimwengu wakakutana na Wanaume flani ambao ni Selfish,hawajali mama katiririka au Lah,wenyewe wakimaliza ndo basi...Filimbi Pyeeeee!Kati!


Hili ni tatizo kubwa.Na likifika kwenye Ndoa ndo inakuwa balaa zaidi....Leo tujifunze Power of Breathing....Inhaling and Exhaling...


Mfumo wa Upumuaji husaidia pumzi kupita kwenye kila part ya Mwili....Pumzi ina-release tension kwenye maeneo yenye tension na kuhakikisha mtu yuko at ease...


This is the Secret behind breathing


Kwa wale wanaume wenye haraka haraka...wenye Kisebengo...Mnawaudhi sana Wanawake wenu na mtasaidiwa kwelikweli na jamaa wanaosimamia kucha..Tena usiombe akamatwe na wale wakongo wa Saluni ndo kabisaaaaa....Fally ipupa haoni ndani,Show ndefu Dar mpaka Kinshasa.


Tafuta muda,wewe na mpenzi...Sio mkionana unarukia tu kama Basi la Kawe limefika...hujui mchuchu ana stress au hana,we unakwea tu...Sio mnazi...Muandae awe tayari kwanza,ndo uendelee

Tumia dakika 5,kaa nae...Fanya mazoezi ya Breathing,,,In and Out mkiwa mmekaa pamoja,mnaangaliana..Inakuwa kama aina flani ya Mchezo but its very healthy.

Hata kama alikuwa na tension,atajisikia released maana Breathing inasaidia kuondoa tension kwenye Mwili.

Na mkianza ile shughuli kumbukeni kuwa na pose kwenye breathing,ili kuendelea kuwa na Oxygen  ya kutosha kwenye Mwili

Kwa wanawake ambao kwao Kilele wanakisoma kwenye Stori za Eric Shigongo please do this...

Before the match do it,hata 5 times hivi ili uwe at ease..na ukiingia kwenye mechi jitahidi kuwa unavuta pumzi ya kutosha and exhale kwa kutumia pua na sio mdomo.

Ruhusu hewa nyingi ndani na uiachie yote,fanya hivyo kama mara 3....

Kamwe usipige kipute huku una mawazo...Mara kazini hivi mara bosi vilee...CONCENTRATE.

Akili yako iwe kwenye Mechi.....Jitahidi kumuangalia jamaamachoni...eye contact helps katika kuelekea kitonga...Sasa nyie mnaopiga kipute Gizani mtajua la kufanya,eye contact mtaipata wapi gizani....

BREATHING CAN CHANGE YOUR SEXUAL EXPERIENCE,TRY IT AND SEEFriday, June 22, 2012

DUDE JIPYA,HALINA HATA MASAA 2 SOKONI---GODZILLA NA MARCO CHALLI


ANAITWA MARCO CHALLI


GODZILLA AKA KING ZILLA FROM SALASALA


Huu mwaka Marco Challi ameamua...Na bado kuna Good Musiq kutoka kwake mwaka huu...


Baada ya kutua na ngoma ya Party Zone akiwa na AY na Video ya Dolari 30,000 wiki iliyopita tu, LEO LEO amedondosha Ngoma mpyaaaaa,kaliiiiii, ameshirikishwa na King Zilla, Godzilla from Salasala...Wimbo unaitwa NATAKA


Club Banger ya uhakika...BAdo ya motooooooo,hata masaa mawili hewani haina,isikiliza..


CLICK http://www.hulkshare.com/wd9zk1ml9ukg halafu usikilize vinanda...Sikiliza Mashairi...Sikiliza mkono wa Dokta Challi


MARCO CHALI AKIWA MTAMBONI MJ RECORDS


Kama wewe mtoto wa Mbwa sisi watoto wa Paka....BALAA


Doctor Chali umetisha

Thursday, June 21, 2012

TIPS TO LADIES...UKIJIACHIA TU KOSA,WANAUME HAWAPENDI SURPRISED

Habari tena kwa mara nyingine Ladies....Nyie ndo mnaoongoza kuumia mioyo inabidi tu msaidiwe kujua how Men are...kuna vitu vingine mwanaume hawezi kusema lakini moyoni vimeshapigiwa mstari kitambo..

Kwa wale ambao bado hamjazaa na hata wale ambao sasa ni wajawazito...Na wewe mwenye watoto au mtoto tayari,THIS IS IT...

Kama kuna mambo yanafanya Baba wa mtoto wako,au Boyfriend kwa nyie ambao mmeamua kujihalalishia kuishi na wanaume bila kwenda Kanisani,Msikitini wala popote,mkaamua kuishi gheto kisela tu,Mungu atajibeba mwenyewe sikieni hili...

Men can not handle Surprises....Ukimuuliza Mwanaume wako amekupendea nini atataja vitu flani hivi...Oh napenda una moyo na Tabia nzuri...SAWA....Atasema yoteeee,unapenda Mungu...Huna hasira...Una roho nzuri,na kila kitu...

Kuna vitu alikupendea lakini ukimuuliza hawezi kuvisema....Wanaume wanapenda Physical parts pia...Kuna wanaopenda nywele...kucha...Maziwa...Miguu....Vinyweleo....Smile...Dental formula ya Meno.....Inye gwedegwede...Shingo...wengine wanapenda hata Sauti tu...

Wengi wanapenda Figure...Aidha Namba 8...Awe Miss...Au mwenye kitu ya kuua mutu!

Wanawake wengi wanapokuwa wana ujauzito/mimba...Na wanapozaa...Wanajisahau...Huu ndio ukweli...Tena wale waliooa ndo zaidi...Wanaona aah mwanaume kashaniweka ndani,sina haja ya kujicomplicate sanaaaa...KOSAAAA!

Mwanaume hazeeki jamani,Ng'ombe hazeeki maini kamwe...Alikupenda akiwa na miaka 22,leo ana miaka 40 lakini hajapoteza taste ya vile alivyokuona,akakuhusudu akakubali kushea maisha na wewe...kuna touches alikukuta nazo,ni vema uzitunze,japo hazitakuwa intact all ur life lakini try to maintain...Nawajua wanawake aged,wana miaka 50 lakini wako Super..Wanaita ile mbaya...Wana watoto zaidi ya wa4...Wamewezaje na wewe ushindwe una nini???

MAINTAIN YOUR SHAPE

Ni kweli kukaa na mtoto miezi 9 ni kazi...Ni kweli utapata Sleepless Nights kumtunza mtoto baada ya kuzaliwa...Ni kweli kuna hatari ya ku-gain weight sana baada ya kuzaa,but hiyo si sababu ya wewe kujiachia na kuwa kama Furushi la Bhangi...

Mtu amekuoa mwaka jana,ukiwa booonge la Demu,akawa very proud kutembea na wewe njiani,kukutambulisha kwa marafiki zake....Leo umezaa mtoto mmoja umejiachia,hujitengenezi,urnt smart,umeachia mwili huooo kama zigo la Bhangi...Eh...SAPRAIIIIZZZZZZZ....Hii wanaume hawataki...

Atapoteza mvuto na wewe...Utalalamika mmeo harudi nyumbani mapema.....Hajisikii tena tendo la ndoa na wewe coz UMEBADILIKA....Ataanza kutafuta watu wengine nje wenye mvuto kama uliokuwa nao wewe alipokuona first day....Utamlaumu???

Getting married is 1 thing....THEN...Linakuwa jukumu...Maintain your marriage....Mpe mume sababu za kuendelea kukupenda kama alivyokuona mara ya kwanza...kufunga ndoa ukadhani umemaliza kila kitu ni KOSA...tena sio tu kosa,ni SUMU! Do not kill yourself...Dont murder your own Marriage wakati unaweza kuifanya i-work...

Get pregnant...Keep yourself Fit....Go gym...if not just do some exercise,make sure ur healthy na you maintain your shape....

NO SURPRISES PLEASE!

Wednesday, June 20, 2012

NO MATTER THE CIRCUMSTANCES...DONT LOOSE FAITH...UKIKATA TAMAA HAYA YATAKUKUTA

Something different kidogo....lakini kitakusaidia

Wote tunaishi kwenye ulimwengu huu na umejaa kila aina ya Shida...Sometimes mambo hayaendi vile tunavyopenda....Kwa style mbalimbali kabisa kila mmoja kwenye angle yake...

Wengine tunapata shida kwenye Kazi...Aidha hatuna kazi au tuna kazi tusizozipenda...Sio choice yako kuwa hapo ulipo lakini ndo kazi uliyonayo na huna jinsi ila kuvumilia ili usile nyasi...

Wengine ni familia...Majukumu yametukuta mapema tunasema..Aidha wazazi wamefariki na tumebaki na mizigo ya kutunza familia..Kutunza ndugu..wadogo...Kaka au Dada zetu kuhakikisha maisha yanasonga...inakuwa ngumu coz hukujiandaa,inafikia point unahisi its too much...

wengine maisha ya kimapenzi ndo mzozo...ur in love lakini mwenzako walaaaaa,hana hata habari..kila siku unapiga kelele zilezile na habadiliki...Kweli unampenda lakini unahisi ni too much...

There are lots of things,they keep on happening...Na inafikia point unakata tamaa..

Just one thing...kumbuka Mungu hana upendeleo....Mungu wa Matajiri ndio Mungu wa Maskini...Nanyesha mvua kwa wema na waovu....Wote anawapa masaa 24 kwa siku kufanya shughuli....Kila kitu ni sawa...Ni jinsi tu wewe unavyoamua kumchukulia Mungu na kufanyia kazi kile alichokubariki nacho...

Kumbuka,kwenye shida yoyote,kuna vitu viwili....Ni aidha unashikilia FAITH kwa Mungu....Au upokee FEAR kutoka kwa Ibilisi...

FAITH itakusogeza karibu na Mungu na utasali na kuamini kwamba haya yote yanayokusonga yatakwisha tu....Kila jaribu lina Mlango wa kutokea,kukata tamaa ni Mwiko...Ni dhambi,haipaswi kufika mahali ukasema IMESHINDIKANA...As long as Mungu yupo,hakuna linaloshindikana

Wakati mwingine tunahisi tumesali vya kutosha...Why Mungu hajibu???Why Mungu amekaa kimya???Hajakaa kimya...Siku zote Timing ya Mungu huwa ni PERFECT...I wish to share some examples for this...Mungu hachelewi kamwe...Wala hawahi kamwe...He is always on time.

Usithubutu kamwe kuruhusu FEAR...Fear ni product ya Ibilisi...kukukatisha tamaa,kukukwamisha na kukupa feeling kwamba Mungu is unfair...Mungu doesnt exist na kama ange-exist basi asingeruhusu yakupate hayo yanayokupata....Shetani akifanikiwa kuua FAITH yako,utajikuta unakubali kila kitu...Ni point hii ndio watu huwaza SHORTCUTS...Watawaza kwenda kuloga....Kwenda kwa Mganga kupiga ramli afanikiwe....Hii ni dalili ya mtu aliyepoteza FAITH na sasa anaendeshwa kwenye vitu vya kishetani na visivyo na muono wa Kimungu...

FAITH will take you through...mungu alikuumba kwa makusudi na as long as ameruhusu uwe hai ana makusudi na wewe...

Shida yote,ongea nae mwambie God i need you here....hata ukihisi anachelewa omba akupe uvumilivu wa kustahimili bila kukata tamaa..

Siku zote FAITH inalipa..Na ikikulipa utasahau shida zote za kusubiria...

Nina m mifano ya watu waliokaa nyumbani miaka mi5 bila kazi..Inafika mahali wanasema basi..maybe sikuandikiwa kuajiriwa na kufanya kazi....Lakini with Faith,leo wako mbali sana pengine hata kuliko wale walioanza kazi miaka mingi nyuma..

God is always able...lolote lile mwambie....Life haina Shortcut......the only way is God..The Masterplanner of your LIFE...

Kumbuka, FAITH ni product ya Mungu na FEAR ni product ya Shetani....Choose FAITH ili ufanikiwe na upate kuishi...Choose FEAR and all devil will do is to KILL...ndio kazi pekee ya Shetani,Kuua na Kuharibu!

BLESS YOU!

SUPERSTAR WA MUZIKI..WA UKWELI..CHEKI UTAJIRI WAKE...SIO UNA VITZ UNASEMA WEWE STARHuyu jamaa anafanya Muziki...Sio bongofleva,ni Hip Hop...

Ni CEO wa kampuni ya Muziki inayoitwa Cash Money Records ambayo ina wasanii wakubwa kama Drake,Lil wayne na Nicky Minaj

Amezaliwa miaka 43 iliyopita na wazazi wakampa jina la Bryan Williams

Fans wake dunia nzima wanamfahamu kwa jina la Birdman...Ana watoto wawili Bria,na Brian JR.

Mpaka kufikia Mwezi April mwaka huu, Birdman alikuwa na utajiri unaofikia Dola Milioni 125 ambazo ni zaidi ya Bilioni 200 za madafu..

Mwaka huu alimpa zawadi mwanae wa kufikia,Lil wayne gari aina ya Bentley Mulsanne na yeye akajinunulia 1 la kufanana nae...Hakuishia hapo,akampa na zawadi, Rasi wa Young Money Records, Mack Maine Rolls-Royce mpya...Mack Maine hakuamini macho yake na akakiri hiyo ni ndoto ambayo hakuwahi kuota kama Birdman anamthamini kiasi hicho..

Kwenye Listi ya marapa wenye mkwanja mrefu duniani, Birdman amezidiwa na P.Diddy mwenye utajiri wa dola milioni 550 ambaye amekaa kwenye number 1 slot kwa mwaka wa 2 mfululizo. Listi ya marapa matajiri inafuatiwa na Sean Carter au Jay Z kama anavyofahamika akiwa na utajiri wa Dola milioni 460,halafu Andre Young au Dr Dre mwenye dola Milioni 260 kisha anafuata yeye,na anayefunga Top 5 ya mkwanja ni Curtis Jackson aka 50 Cent mwenye wallet ya Dola Milioni 110.

VITU USIVYOJUA KUHUSU YEYE

Birdman anaishi kwenye nyumba ya Dola Milioni 30 huko New Orleans,Louisiana...CHEKI HOUSE HIYO

Mwaka jana alinunua gari aina ya Bugatti Veyron kwa Dola milioni 2.5 ambazo ni bilioni 3 na ushee za madafu...Wiki iliyofuata akanunua Pete ya thamani ya Bilioni 3.Wiki moja akaspend Bilioni 6...Hapo vipi??Ni moja kati ya magari ya Bei mbaya zaidi duniani na ni wachache sana wameweza kununua akiwemo yeye,Christiano Ronaldo na Kanye West..HILO HAPO CHINI LICHEKI...
BUGATTI KWA NDANI


MUZIKI UNALIPA BWANA..UKIFANYA KWA MOYO,KWA KUJITUMA NA KWA HESHIMA

Ni baba wa kufikia wa Lil Wayne

Wakati Katrina Hurricane ilipopiga nchini Marekani, Birdman alipoteza Nyumba 20 na magari 50 kwenye Kimbunga hicho...Hakumind,akanunua mapyaaaa!

Ofisi ya Label yake ilibidi ihamishwe kwenda Miami baada ya Katrina kupiga almost kila kitu

Birdman ni Fan mkubwa wa Justin Bieber na amekiri hilo mara kadhaa

Hununua magari 100 kila baada ya Miezi 6..Na yale ya Zamani anagawa kama Zawadi


Mwaka huu,2012,amenunua gari kwa Special Order,aina yaLamborghini Aventador lenye thamani ya Dola 800,000 ambazo ni Bilioni 1.3 kwa madafu..HILO HAPO CHINI....Kama haitoshi Birdman alikaririwa akisema ameweka Oda ya gari litakalotoka December mwaka huu aina ya Maybach Exelerro lenye thamani ya Dola Milioni 8 ambazo ni Bilioni 15 za madafu na ni lazima awe nalo ....LAZIMA UCHOKE...HILO HAPO CHINI
Halafu wewe ununue VITZ useme wewe Star???Hebu mtupishe
RAISI HOSNI MUBARAK AFARIKI JANA USIKU AKIWA JELA

Muhammad Hosni Said Mubarak: MAISHA YAKE HADI KIFO CHAKE
Wakati akihukumiwa kifungo cha Maisha wiki 3 zilizopita,niliwaambia rafiki zangu fulani tukiwa pale mlimani city kwamba huyu jamaa hatamaliza Mwaka....kumbe hata Mwaka it was too much...Hajamaliza hata Mwezi tu....Alizoea maisha ya Starehe mno,ya kitajiri mno,kuishi jela ni zaidi ya kitu alichotegemea in his life...Alitegemea kuishi kifahari maana ana kila kitu Binadamu anataka humu duniani...

Hosni Mubarak alizaliwa kama mtoto wa wakulima katika kijiji cha Kafr-El-Meselha kwenye mkoa wa Monufia uliopo Misri ya kaskazini. Baada ya shule alijiunga na jeshi la anga la Misri akawa rubani akasomeshwa kwenye vyuo vya kijeshi huko Umoja wa Kisovieti Baada ya vita ya siku 6 akawa mkuu wa jeshi la anga la Misri.

Mwaka 1975 aliteuliwa na rais wa Misri Anwar Al Saadat kuwa Makamu wa rais. Sadat aliuwa mwaka 1981 na Waislamu wakali hivyo Mubarak akawa rais mpya. Kuanzia 14 Oktoba 1981 alishika vyeo vya rais wa taifa hadi mwaka 2011. Kuanzia 25 Januari 2011 wananchi wa Misri alianza kuandamana dhidi ya utawala wake na tarehe 11 Februari Mubarak alijiuzulu na kumkabidhi makamu wake madaraka yote.

Mubaraka na familia yake walikaa kwenye rasi ya Sinai lakini tar 24 Mei 2011 serikali ilimshtaki Mubarak pamoja na wanawe Gamal na Alaa na aliyekuwa mkuu wa polisi ya kisiri Hussein Kamal al-Din Ibrahim Salem kuwa waliwajibika kwenye mauaji ya waandamaji 800 wakati wa maandamano wa 2011, pia ufisadi na wizi wa mali ya dola. Kesi ilifunguliwa tar 3 Agosti na Mubaral alipelekwa kotini katika kitanda ya hospitali.

KUONDOKA MADARAKANI

Mubarak alikuwa mmoja wa watawala wenye mamlaka na nguvu zaidi kwenye eneo la Mashariki ya kati. Alifuata siasa ya rais mtangulizi Sadat aliyepatana amani na Israel. Utawala wake ulikuwa wa kidikteta.

Wananchi wake walipomchoka waliingia mtaani na kulazimisha aondoke,baada ya kuiendesha misri kwa Miaka 30.Alikiwa mmoja kati ya Maraisi walioongoza kwa muda mrefu zaidi duniani ukiacha Mugabe na Omari Bongo wa Gabon.

Hatimaye nguvu ya Umma ilipozidi akaamua kuachia madaraka na machafuko hayo yalisababisha afunguliwe mashtaka ambayo yamempeleka gerezani Wiki 3 zilizopita baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha na Mahakama ya Kijeshi nchini Misri.


HAPA AKIWA JELA KAMA ALIVYOPIGWA PICHA JANA ASUBUHI KABLA HAJAFA


UTAJIRI WAKE

Mnamo mwaka jana, ilikadiriwa kuwa Raisi Hosni Mubarak alikuwa mmoja ya Watu wenye hela nyingi sana na pengine mtu tajiri aliye hai kwenye bara la Afrika.

HAPA AKIWA NA MKEWE,WATOTO NA MKWE WAKEUtajiri wake ambao alitajwa kuumiliki kwenye Benki za Kigeni  ulikadiriwa kufika Dola Bilioni 70 ambazo ni zaidi ya Trilioni  120! USIPIME!

Utajiri huu ni zaidi ya bajeti ya Tanzania kwa Miaka 20 mfululizo...Mtu anamiliki yeye mwenyewe na Familia yake....Ila Mungu atabakia mungu tu,hela zote hizi na amekufa ameziacha,tena kwa aibu,akiwa gerezani anatumikia kifungo cha Maisha alichohukumiwa Wiki 3 tu zilizopita

FUNDISHO

Hela sio kila kitu...He was a president....He was powerful....He is stinky rich....Lakini amekufa akiwa gerezani.....Learn and be wise!

Tuesday, June 19, 2012

STORI KAMILI YA MWANAFUNZI WA SAUT ALIYEPOTEA BAADA YA RAFIKI YAKE WANAYEKAA ROOM 1 KUNITAFUTA LEO KUHADITHIA TUKIO ZIMA MWANZO MWISHO

Nimepata Fresh update mchana huu baada ya rafiki wa karibu wa Msichana huyu aliyepotea kunizamia hewani na kunipa mchapo mzima wa issue hii inayosisimua...


Stori ya jana iliishia kwa jamaa kumuita Msichana Hotelini ili waonane kwa mara ya kwanza na kucheza mechi matata....TUENDELEE


Alipo fika hotelini mshkaji alimuelekeza chumba alichopo akaenda akamkuta kalala, jamaa hakuamka kumkaribisha ,hamna cha waooooooo wala Hug... akasema njoo kitandani tu mimi nimechoka na uchovu wa safari

Basi Shosti akasema basi na mimi ngoja nioge ndo nije hapo kitandani si unajua kujiandaa na mechi tenaAkavua nguo akaingia bafuni kupiga ma-shower...Wakati anatoka bafuni akamkuta jamaa kasimama,hayuko tena Kitandani...Halafu yuko uchi...Sehemu ya chini ya kitovu kuja kwenye eneo la tukio kuna kama Funza hivi wanatembea lakini hawaanguki chini...Akataka kukimbia akamwambia ukikimbia tu unakufa, unataka kwenda wapi zile hela ulizokuwa unakula unadhani zilikuwa zinatoka wapi...Stori ni kwamba jamaa alikuwa anatuma mkwanja zaidi ya Laki3 kila mwezi kwa mtoto wa kike...Muda wa kuzilipia sasaaaaAkamwambia haya panda kitandani unipe mambo mie...Demu kusikia kufa akawa hana jinsi akapanda kitandani jamaa alivyosimika tu mzizi demu kama aka-pass out anakuja kushtuka kumekucha, haelewi nini kimetokea baada ya lile tendo...Asubuhi ameamka anamuona jamaa kalala.....akikumbuka alicho kiona na wale funza  na anavyo ona asubuhi hii ni tofauti... Mwanaume akawa wa kawaida kama anavyomuona Facebook,Handsome fresh tuu akaamka,akaoga freshi akamuaga mie naenda chuo basi ntakuja badae, akasepa


Basi kufika chuo hakutaka kuwaambia wenzie ukweli kwamba kapelekewa mjeledi na jamaa ameoza...Akauchuna akawaambia wenzie ameonana nae mshkaji...Ghafla akabanwa mkojo,kwenda chooni kukojoa anaona wale Funza kama jamaa kuleeeee....


Ikawa soo,ikabidi tu sasa aseme ukweli ili asaidiwe...Wenzie wakampeleka Dispensari ili asaidiwe...Kule akachomwa sindano lakini hali ikazidi kuwa mbaya ikabidi wale manesi wamshauri tu apelekwe Bugando Hospital wacheki zaidi tatizo.


Njiani kuelekea Bugando ndipo mazingaombwe yakatokea na demu akapotea ghafla...


Wale mashosti kwa kuwa walikuwa na namba za yule SHEMEJI JINI wakampigia simu ili kumuuliza kulikoni....Jamaa akasema WALA SIO YEYE NA HUYO ALIYEKUJA MWANZA HAMJUI....


MPAKA HABARI HII INAPOANDIKWA DADA HUYO HAJAPATIKANAANAITWA DIAMOND PLATINUMZ...KUTOKA OPA MPAKA LANDCRUISER PRADO....HAKI YAKE TUMPE,HEKO MWANABONGO FLEVA
Sikuwahi kudhani nitakuja kumuandika DIAMOND...Kwakweli ila imebidi...

Wanasema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,nami nampa heko zake...

Baada ya ku-release Hit baada ya Hit...Mbagala...Kamwambie...Nitarejea....Mawazo...Nimpende Nani...Lala Salama...na mpya alioshirikishwa na Diva,Piga simu...Pamoja na nyingine nyingi tu alizoshirikiswa na wasanii wenzie kama Shetta na Ommy Dimpoz....ANASTAHILI MAFANIKIO HAYA NA ANAJITENDEA HAKI

Baada ya ku-expose mjengo wake wa thamani ya Milioni 69 wiki chache tu nyuma,Diamond Platinumz alipata nafasi adhimu na adimu kwenda Bondeni kwa Madiba,South Africa kwenye Jumba la Big Brother kutumbuiza....Wiki chache tu baada ya Headlines hizo,another headline zimesambaa na kuthibitishwa naye mwenyewe kupitia Blog yake ya This is Diamond,baada ya kununua mkoko mpya aina ya Land Cruiser, Prado...
Nyota ya Jaha imemuangukia,na Mungu anabariki kazi za mikono yake baada ya kujituma na kufanya kazi bora kabisa tangu aingie kwenye Tasnia hii ya Bongo Fleva...Mwenzetu kahama kwenye ile Toyota Opa nw he gat the new ride...

Monday, June 18, 2012

TETESI:WOLPER ANYANG'ANYWA GARI ALILOSEMA NI LAKE AINA YA BMW X6

GARI ALIYOPEWA WOLPER,AINA YA BMW X6Mwigizaji wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa gari lake la kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Bongo.

Habari zenye ukweli 100% ambazo Blog hii imezipata kutoka Mtandao namba 1 wa burudani Tanzania,Teentz.com, zinasema kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya  Milioni 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.Aidha chanzo hicho, kimeieleza Teentz.com kuwa hivi sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa aliyokuwa anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake wa karibu washitukie mchongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana Teentz.com iliamua kumsaka na baada ya kupatikana Wolper aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.
Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tene kwa siku tatu Wolper alisema hivi: “Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaaNGOJA TUSUBIRI TUONE UTETEZI WAKE MUDA SI MREFU MTASIKIA

Saturday, June 16, 2012

50 CENT ATANGAZWA KUFA AJALINI USIKU WA KUAMKIA LEO

Habari zilizotangazwa na Mtandao wa Local Team News umetangaza kifo cha Rapa 50 CENT ambaye alikuwa akiendesha gari ya rafiki yake.

Watu wa karibu walitia shaka labda 5o alikuwa amelewa lakini hakuna Pombe wala Bangi iliyokutwa kwenye gari hilo baada ya polisi kufika eneo la tukio.

Ajali hiyo imetokea kwenye mji mdogo wa Morristown na taarifa kuhusu mazishi yake bado hazijatolewa rasmi.

Kama habari hizi ni za kweli itakuwa ni habari mbaya sana kwa wapenzi wa 50 ambaye ametoka kutoa Album mpya mwezi uliopita tu.

50 CENT anafahamika ulimwenguni kote kwa nyimbo kali zikiwemo In Da club uliomtambulisha kwenye Ulimwengu duniani kote, 21 Questions, Baby by me na Neyo na nyingine nyingi na aliwahi kuja Tanzania kupiga Show iliyofunika sana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee

Toxicology(Uchunguzi wa Kidaktari kuhusu Kifo) utafanyika leo kujua kama alikuwa Under influence ya Kilevi chochote japokuwa taarifa zinaonyesha Ajali hii kwa kiasi kikubwa imesababishwa na hali mbaya ya hewa kwenye Mji huu kwa sababu 50 alikuwa akiendesha Spidi ya Maili 95 kwa Saa mpaka alipo-loose control ya gari na kupinduka.

Stay tuned maana mi mwenyewe siamini bado...Yasije kuwa yaleyale ya David Guetta na will Smith,Mastaa wanajua sana kufoji Vifo.

Lets wait and See!

WIMBO MPYA WA AY AKIWA NA MARCO CHALI-PARTY ZONE...VIDEO YA BEI MBAYA,KALI MNOOO


Bonyeza link http://t.co/U7Bb9uUO cheki mzigo ulivyokaa poa pale kati.

Video hii imetengenezwa nchini South Africa,na estimates za utengenezwaji wa Video hii ni Dolari za Kimarekani 30,000 kutoka kwa the well-known Video Producers in Africa,GODFATHER...Mkono wa MARCO CHALI aka DOCTOR CHALI wa MJ Records...Maneno hayatakiwi kuwa mengi sana.

Ingia mwenyewe uwatch Video hii na utakubali kwamba AY anafanya Muziki wa Kimataifa na ndio maana akaingia gharama na kutoa mkwanja mrefu ambao kwa madafu ni zaidi ya Milioni 45 za Kitanzania.HATARI!

AY AKIWA NA PREZZOBig up AY...Big Up MArco Chali...Big Up Godfather kwa kazi nzuri sana!

Friday, June 15, 2012

CMB PREZZO AAMUA KUJITOA BIG BROTHER AFRICA

Vijimambo vinaendelea kurindima kwenye jumba la Big Brother huko Afrika Kusini!

Baada ya washiriki kutoka Tanzania kutia fora baada ya kutimuliwa mapema,na baadae mshiriki DKB kutolewa baada ya kumdunda mshiriki mwenzie makofi akimaindi kuchunguliwa bafuni,sasa imekuwa zamu ya msanii nguli wa kenya, CMB PREZZO!

Prezzo ameamua kujitoa kwenye jumba hilo baada ya sheria ya Mitungi kutoruhusiwa kwenye jumba na amesema yeye sio mfungwa hivyo ana uhuru wa kutoka muda wowote anaotaka!Msanii prezzo ambaye anapewa nafasi kubwa kuondoka na kitita cha dola 300,000 mwaka huu amemshangaza kila mtu pale alipomwambia mshiriki mwenzake Keitta kwamba ni heri afunguliwe mlango aondoke zake kwenda home kuliko kukaa kwenye Mjumba usio na Pombe kama Mfungwa.

Sijui kama Big Brother atamruhusu kusepa,ingawa kama itatokea itakuwa ni pigo kubwa kwa waafrika wengi ambao wanaonekana kumpa sapoti kubwa sana tangu aingie kwenye Jumba hilo kutokana na kuchangamsha sana kwenye mchezo huo!

Thursday, June 14, 2012

SABABU 7 KWANINI HUTAKIWI KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA JAPO NAJUA UNA MIHAMU GUNIA ZIMA NA UNAHISI HUWEZI KUACHA UTAMU HUO

Najua hii topic ni msala mtupu! Hilo nalitambua lakini inabidi tu hata hili lisemwe,usiponielewa leo utanielewa tu siku za usoni lakini usiseme sikukwambia


Mimi na wewe wote ni wahanga wa Pre-mature Sex...Kwa wale mliooa(nna uhakika wengi wenu kama sio wote) Mligonga kitu kabla ya muda,au sio?


Sasa mzigo ndo huu hapa...Kuna sababu 7 kwanini tunashauriwa tusifanye Mapenzi kabla ya ndoa....Vitabu vya Dini vimeandika hili na Kukataza lakini amri inavunjwa kama kawa utadhani Kitabu cha Kutoka 20:14 kimefutika kwenye Biblia....Kile kilichokatazwa ndo kinapendwaaaaa,kitamuuuuu,na watu hawataki kukubali kwamba inabidi kiachwe!


Ubishi huu kuhusu kula tunda ndio uliotucost Binadamu kufika hapa tulipo leo...Kosa lileeee la Adamu kupewa Tunda na Eva,baada ya Ibilisi kumdanganya Eva kwamba Tunda lina Mzuka ile mbaya na hata Mungu anajua ndo maana kawabania...uongo ulikuwa mtamu Eva akajaa kimiani..Matokeo yake ndo haya...Adam kafukuzwa Edeni,tumerithi Dhambi na kero chungu nzima...kifo hakikuwa kwenye Plan ya Mungu ila ni adhabu ya uleee uongo wa mwanzo,lakini HATUKOMI wazeee tuko bize kufanya REMIX ya mambo yaleyale aliyofanya ADAM na EVA kule EDENI halafu tunatetea eti haiwezekani,Mungu anajua alichoumba usimfundishe kazi!


SABABU YA 1:IMEKATAZWA NA MUNGU


Sababu ya Kwanza kwanini hatutakiwi kufanya Mapenzi kabla ya ndoa ni kwa sababu MUNGU HAPENDI....Amekataa...Na amekataa sio kwamba hajui Sex ni Tamu,....Anajua utamu woteee unaousikia ukifanya mapenzi...anajua raha unayopata ukiwa unacheza kile kiduku pale bed kwa mbwembwe...Anajua zile hisia unazofeel na nini kinatokea ukifanya,ANAJUA...yeye ndo ameziumba zile hisia,USIMFUNDISHE MUNGU KAZI YA KUUMBA! Alikuumba akijua una Hormone ambazo zitakusumbua lakini vilevile amekupa uwezo wa kuzishinda...Mungu hawezi kuweka jaribu ambalo halina Mlango,kama alisema usifanye basi anajua uwezo wa kutofanya upo!
Tutabisha weeee,ooh haiwezekani,kuna watu hawafanyi na wapo,wanapumua kama wewe,wanamtii Mungu na wanaishi..hawafi,na wanakuja wanaoa na mambo wanakula kama kawa...Zile stori usipofanya sijui ufutio unapotea,mara hivi,ni Plan za shetani tu kama alivyomdanganya Eva akajaa kimiani,anakujaza na wewe uamini ili upotee.USIKUBALI


SABABU YA 2:UTAMU WA HONEYMOON KWISHNEY


Utakapooa, utaenda Honeymoon...Nia ya honeymoon ni wewe kupewa fursa ya kutoa gundi kwa mara ya kwanza...Kumbe gundi umeacha Machimachi Guest House miaka mia8 nyuma


UNAENDA HONEYMOON KUFANYA NINI??KUMDANGANYA NANI??


Hizo hela za Kamati ya Maandalizi watu wanakuandalia kwenda Honeymoon wakati Ramani nzima ya huyo mkeo na mmeo USED unaijua hata ukifumba macho.KATAA HIYO!


SABABU YA 3: UTAKUWA NA AFYA KIROHO


Tunaishi kwa ajili ya Mungu...tuko hai kwa sababu Mungu ametuacha na kutupa nafasi ya kurekebisha maisha...Ukifa leo utakwenda wapi?Umewahi kujiuliza??
Hauko hai kwa sababu wewe ni mwema sana mbele za Mungu...As long as uko hai inabidi uishi vile ambavyo Mungu anataka uishi...MAISHA SAFI MBELE ZAKE!
Na ni ukweli usiopingika kwamba dhambi hii ya NGONO/UTAMU/UZINZI ndio namba 1 katika kuharibu maisha ya kiroho ya Watu...Hii dhambi ndo Weapon namba 1 ambayo Ibilisi anaitumia kumaliza watu.Laiti hii isingekuwa dhambi basi watu wengi sana wangeingia Mbinguni,Wengi sana...Lakini hali ni mbaya sana...
Naweza kuthubutu kusema Afya yako ya Kiroho inategemeana na ushiriki wako kwenye Ngono au La.ukishinda hii,siamini kuna dhambi itakuwa ngumu kwako kushinda,Jaribu uone!
Unaikosa Mbingu hivihivi kisa pale katikati....WAZA UPYA!Tangu uanze kuifanya hiyo kiu imeisha???Mbona unafanya na unafanya na kufanya haiishi,uskiacha utakufa??Its not late to start over,na uzuri wa Mungu ukitubu,anafuta zoteeee za nyuma unakuwa mpya.You can start afresh LEO!


SABABU YA 4:NI NZURI KWA AFYA YA KIMWILI


Hapa napo imekuwa mgogoro.mwanzoni watu walisema aaaah ntakaaje na Sweetie wangu bila kufanya,wakahalalisha...wamefanya weeeee wamechokana...wakaanza kuiba nje,na wapenzi wengine,na kwa sababu umekuwa sugu huoni tabu kuongeza listi...Ishu inakuja Je, hiyo listi yako iko salama???


Watu wengi wamepata pancha hapo katikati,wamefikia muda wanataka kutulia na kufunga ndoa kuanzisha familia...LOH!AFYA MGOGORO!Siku hizi magonjwa ni mengi sana,acha tu Ngoma inayozingua kila kona,kuna magonjwa ya Zinaa ambayo unaweza ukaletewa na bila kuyatibu vizuri ukaharibu vizazi ile mbaya.....Kuna ishu za mimba,maana mechi siku hizi pekupeku tu...ETI MNAAMINIANA,peku pekua mara kitu kimejaa...wote ndo mnagundua hamko tayari kwa mtoto!Upuuzi mwingine huo...Mko tayari kukata kiuno ila result za kiuno hutaki...Utafanyaje mtihani halafu useme hutaki majibu??utajuaje umefaulu au kufeli??Mapenzi bwana!Mwanamke wa watu analazimika kutoa mimba maskini,mwisho wa siku mkibahatika kuoana hampati mtoto,HALFU UTASEMA WHY ME LORD???KWELI???Au mtoto wa kike anaolewa na mtu mwingine,tayari ushamsababishia kimeo kwenye ndoa yake,na haya yako kila kona wala sio mapya.WAZA UPYA!


SABABU YA 5:LINDA HISIA ZAKO


Unampenda mtu unafanya nae Mapenzi...mnaachana,unapanga misururu watu wengi kama msururu wa wateja wa NMB kwenye ATM...Wote hawa unatumia moyo huohuo,hisia hiyohiyo,wote umewaonja,wamekupa different tastes,kama mia7 hivi....wote wamekutenda,Hisia zako zinakuwa na rangi kibaooooo,hata hukumbuki moja kati ya hizo ipi sahihi....
Nakutana na watu wanasema hawawezi kupenda tena,kia wametendwa....Sio hivyo...Sehemu ya hisia ishatiwa shoti,kila mtu kaja na bisibisi yake anachomeka tu,size 17 twendeeee size 44 twendeeee,haueleweki hisia zako zimefikia size ngapi,maana kuna waliozi-under size,na wengine wameku-oversize...Umeshakuwa emotionally unhealthy....


Kwanini usitulie uje utumie hisia zako kiusahihi na mtu sahihi???kwanza hawa unaosex nao wengi hata wazo la kuao hamna,wanakutumia tu bureee bureeee,ukimwambia tu twende home nikutambulishe anajitetea  na maneno lukuki kama konda wa Mazese-Mburahati,ndo utajua utatumiwa tu kama condom,kisha kitanda chako jalalani!


SABABU YA 6: UVUMILIVU NI TESTI NZURI YA UPENDO WA KWELI


Hapa hata sina haja ya maelezo mengi...Mtu mvumilivu huonyesha nia ya dhati na upendo wa kweli..Ila mtu anayekurupuka tu huyooo ndani ya Shuka,utajua tu penzi lake ni la ki-shuka shuka zaidi.


SABABU YA 7: BARAKA ZA MUNGU MLIYEMTII NA UTULIVU WA NDOA


Ukimtii Mungu huwa anatoa baraka zake...Na kinyume chake ni dhahiri...


Wle wanaomuamini Mungu na kufanikiwa kufikia hapa,maisha yao yanakuwaga tofauti kabisa na wale walioishi maisha ya kibiriti-Ngoma Style.


Watu mmetoka tangu urafiki mnaibatua amri ya 6 bila huruma....Sasa mnafika kwenye ndoa mmechokana,Ladha yote imakwisha,,Mke hana jipya la kukupa...Hakuna machejo ya Mme usiyoyajua....NO EXCITEMENT.


Sishangai kuona Mwanaume ameoa anacheat...Hamna jipya,Mke anabakia tu kuwa Kiwanda cha kufyatua Watoto lakini INTIMACY YA NDOA HAKUNA. Anaamua kujaribu ladha zingine!


Na effect za Mwanaume asiye na Intimacy na mkewe zitaonekana hata kwa Mkewe in due time...Hatampa haki yake kadri inavyopaswa,na mwishowe mkewe atachoka kulishwa Makombo,anayoyajua kwa Nusu Karne huko nyuma...


Kifuatacho hapo ni wote kugeuka CHEATERS...Mke anapiga show za nje kwa wizi...Mme nae anakamua mechi za Mchangani nje kwa kujiiba...Wote hawa wanajaribu kupasha misuli nje maana ndani Gym imeishiwa vifaa...Wanajifanya wanapasha moto Kiporo kilichochacha...Kamwe hiyo ndoa itakuwa ngumu sana kusimama tests of Time!
ARGUMENTS
Wengi wata-argue kwamba Maadili yanachangia.NAKUBALI,Siku hizi ni ngumu sana kumuamini Mpenzi kwamba atavumilia,ndio maana Wanawake wameamua kujitoa Sadaka kutoa tunda kama njia ya kuwin penzi la wanaume...UONGO!Penzi la Mwanaume halishikwi kwa kumpa Tunda...Kama anakupenda WEWE atakaa,kama alipenda TUNDA atakwenda...Simple Rule....Mwanaume anapaswa akupende WEWE kwanza na Sio ulichonacho Wewe...Afterall kama ana ana nia na hicho kitu,si atakimilikisha kuwa chake Milele na milele??sasa anakiwahi cha nini??kuku wa Kwako ya nini Manati??


Na wanaume pia,wanalalamika wanawake hawaaminiki,wana roho ndogo...Wewe unamtunza hupigi show unadhani kwamba anakutunzia unashangaa anakuja bwege flani anakula mali yako kiulaini,Roho inauma,so bora upige show ili hata ukiporwa,ah fresh mlinganyo umekaa poa.


Maadili yanachangia lakini na Ibilisi kwa kulitambua hilo,ameinvest hapohapo kwenye LOST FAITH ya Maadili,na anawachapa watu bila huruma.


Mimi nimemaliza hapa..Ukiamua kunisikiliza na kuamini Mungu na akubariki,ila nikiwa kama Jogoo anawahi kuamka lakini hafungui mlango haya..


             NATUMAINI MJUMBE SITAUAWA!


MUME WA ANGELA CHIBALONZA AOA MKE MPYAAAAA!!

Angela Chibalonza sio jina geni kwenye masikio yetu,amekuja mara kadhaa nchini Tanzania kufanya huduma na anapendwa sana kwa nyimbo zake ambazo miaka na miaka zitaendelea kutamba kwenye chati za Muziki wa injili.Nyimbo zake kama EBENEZER, Ni maarufu si tu Kabnisani,ila kwenye midomo hata ya watu wasio Wakristo.Ama kwa hakika alikuwa muimbaji mahiri sana sana!

ikiwa imepita miaka michache tangu Angela Chibalonza afariki kwa ajali ya Gari akiwa ametoka kwenye huduma huko Kenya, mme wake, Apostle Elisha Muliri ameoa mke mwingine ili kupunguza upweke na ili huduma isonge mbele.

Ni ngumu sana kufanya huduma ukiwa huna mke,vishawishi ni vingi sana na imebidi hata yeye aoe tu ili huduma isonge.

ANGALIA PICHA SIKU AKIFUNGA NDOA(Mwenye Kofia) NA MKEWE MPYA, MAGRETH
Apostle Muliri ni Kiongozi wa huduma ya Shekinah international ambayo mkewe wa Zamani, Angela alikuwa akihudumu pamoja

KITANDA CHENYE UWEZO WA KUJITANDIKA CHENYEWE KWA WALE WAVIVU TUSIOPENDA KUTANDIKA VITANDA ASUBUHI

Najua hii inawagusa watu wengi tu...Na hata mimi inanigusa kwa namna moja au nyingine!

wengi wetu tukikurupuka asubuhi huwa tumechelewa na tunaona kama kutandika Kitanda tunazidi kuchelewa tunaacha kiko shaghalabaghala,bila kutandika!

Kama kawaida yao Wazungu,wanajua tu kutengeneza pesa kwa kutumia madhaifu ya watu

Wametengeneza kitanda chenye mashine maalum ambayo ina uwezo wa kusense kwamba sasa mtu ameamka na inaanza kutengeneza Kitanda automatic.

Na jamaa wameweka Mechanism,Mashine hiyo haiwezi kufanya kazi kukiwa na mtu amelala,ila sekunde 5 tu baada ya wewe kuamka, Ile Mashine itasense kwamba sasa mtu ameamka,inatengeneza Kitanda.USIPIME KABISA,mzungu noma!

CHEKI MZIGO WENYEWE HUO:HAPA NI PALE UMEKURUPUKAHALAFU CHEKI HAPA MASHINE ISHAKUFANYIA KAZI AFTER 5 MINUTESJAMAA AMGEUZA DEMU WAKE BUCHA KWA KUMCHEAT..AACHA UJUMBE

Inatisha sana...Jamaa mmoja mwenye Wivu huko Bahamas amemuua mchumba wake kwa kumkata kiungo kimoja baada ya kingine baada ya kugundua amemcheat na Mwanaume mwingine!

Baada ya kumaliza tukio hilo aliandika ujumbe kwenye Panga alilotumia kumkata ''THIS IS WHAT CHEATERS GET''

Jamaa huyo kwa sasa amekamatwa na Polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuua kwa kukusudia!

Inaonekana huyu jamaa yeye alikuwa hajawahi kabisa kucheat maana mpaka imemuuma hivi sio bure

WATCH OUT ALL CHEATERS! Kuna watu hawana dogo,utageuzwa bucha fasta! INATISHA

Wednesday, June 13, 2012

KANYE WEST APOST PICHA ZA UCHI ZA MCHUMBA WAKE KIM KARDASHIAN KWENYE TWITTERSijui ni wazimu au la ila Kanye West, siku ya jana alituma picha ya mchumba wake Kim Kardashian kwenye mtandao wa TWITTER,picha ambayo ilimuonyesha Kim akiwa uchi wa mnyama akijipaka lipshine kwenye chumba huku amekaa kitandani.

Muda mfupi tu baada ya tukio hilo, Kanye West aliitoa picha hiyo haraka lakini wadaku walikuwa wameshainyaka na kuisave na kuisambaza all over the World.

Kanye West alijitetea kwamba sio picha ya Kim Kardashian na hata Kim alikataa kuwa sio yeye.

Kasheshe ni pale ambapo ilikuja kusemwa kwamba picha hiyo ambayo Kanye West aliiweka ni picha ya Mcheza Ngono mashuhuri,Amia Miley.

Swali ni Je, Kanye West alimtoa wapi mcheza ngono huyo hadi kumposti akiwa vile??

Je,Kim Kardashian atareact vipi baada ya tukio hili la mchumba wake mpya??

Mcheza ngono huyo ameonekana kuongeza moto kwa kusema picha hiyo ni yake na sio Kim Kardshian...Anasema Kim Kardashian hana Dimples kama picha inavyoonesha japokuwa ukiicheki mmmmh,ni kama Kim hivi...

Hebu jionee mwenyewe,Je huyu ni Kim Kardashian au sio yeye???BALAA!Social Media hizi zina mambo

PICHA HIYO ALIYOWEKA KANYE...


RAISI BEN ALI WA TUNISIA AFUNGWA MVUA 20

Lile wimbi la Maraisi wa Zamani waliotumia vibaya madaraka kufungwa limeonekana kuendelea baada ya jana,Mahakama ya Kijeshi nchini Tunisia kuamuru Raisi wa Zamani wa nchi hiyo,ZINE EL ABIDINE BEN ALI kuamriwa kwenda jela kutumikia miaka 20 baada ya kukutwa na Makosa ya uhalifu wa kivita uliosababisha machafuko nchini Tunisia ambayo yalimlazimisha kukimbia nchi na kusalimu amri.

Kwa sasa Raisi Ben Ali anaishi uhamishoni nchini Saudi Arabia na itabidi arudishwe kuja kutumikia kifungo hicho. Raisi huyo aliamuru waandamanaji waliokuwa wakimpinga kupigwa risasi katikati ya January, 2011 kwenye mji wa Ouardanine nchini tunisia,lakini vurugu hizo hazikuweza kuzimwa na Polisi na hatimaye ikabidi akimbie nchi.Wasaidizi wake kadhaa nao pia wamehukumiwa kifungo cha kati ya miaka mi5 hadi 10 kila mmoja

Huu ni mwendelezo wa kichapo kwa Maraisi wa Africa waliotumia madaraka yao na kujiona wako Above Law,baada ya Charles Taylor kuhukumiwa miaka 5o wiki 2 zilizopita na Mahakama ya Uhalifu ya The Hague,akifuatiwa na Raisi wa Misri, Hosni Mubarak aliyehukumiwa kifungo cha Maisha jela japo yuko hoi hata Mwaka sijui kama atamaliza.

Hili ni fundisho kwa viongozi wa Africa kwamba Madaraka sio dhamana ya kutesa wengine, What Goes Around comes Around like a Hoola Hoo..

RAISI BEN ALI

HOW TO WIN MOYO WA MWANAMKE-RISASI 8 MUHIMU KWA WANAUME

Mara nyingi nimesikia watu wakisema Wanaume hupenda kwa akili, na Mwanamke hupenda kwa Moyo....Huenda ni kweli,lakini mimi naamini kuna wanaume hupenda kwa moyo pia na kuna wananwake hupenda kwa akili...Hawa ni wale waliochoka kufall in Love na kuumia,wameamua kutumia ubongo kudeal na wanaume,na usiombe ukutane na hiyo type utajuta,...

Leo tuongelee mambo kadhaa jinsi ya kuwin moyo wa Mwanamke,,na Somo hili ni kwa Serious people ambao wanataka kuwa in serious relationships with commitments...

Mwanaume ni kichwa wa familia,theoretically,ila Mwanamke ni kiongozi wa Familia practically...Ukitaka bisha na upasuke, Wanawake ndio wanaoongoza familia kwa asilimia 90..wana vision na familia,wana planning ability...Wana budgeting ability,ya hali ya juu,na Leadership na hata ukuzaji wa watoto unamhitaji MAMA...tafuta mtoto aliyekuzwa na BABA uone kazi...Shughuli pevu

Ukitaka kuwin moyo wa Mwanamke fanya yafuatayo:

1. Tambua mwanamke uliyenaye ana tabia gani,anapenda nini na anachukia nini.Mpe anachopenda na usifanye asichopenda.Ni ngumu,kwa sababu wanaume huwa wanataka kuonekana vidume na hawataki kuishi kwenye amri za mtoto wa kike lakini kama una nia ya dhati ya kuwa na Strong and Solid relationship na Bond iliyotakata na Mwanamke,Make her win in whatever she wants...Ukimpa hili,wala huna haja ya kufanya muujiza mwingine

2. Mpe attention maana wanapenda,na ni wote,ukiona Mwanamke hataki attention yako jua kuna jamb nyuma ya pazia au wewe ni 2nd choice. Attention hii ni mkusanyiko wa vitu vingi...Kumjali hisia zake,kuzielewa wakati yupo down na kujua nini cha kufanya kumrudishia Smile yake,na wakati akiwa happy kujua jinsi ya kushare happiness yake.Haichukui dakika nyingi kumjulia hali asubuhi,Mchana,na Jioni...Ni ngumu kwa Mwanamke kuona wenzie wakijuliwa hali halafu wewe umeuchuna eti uko busy,Busy my Foot!

3.Surprise her! Hakuna Mwanamke hapendi surprise,bado sijaona,na anayejifanya hapendi anazuga tu...Na wala surprise yenyewe wala haitakiwi na sio lazima iwe expensive ndo iwe surprise...Ile feeling kwamba My boy amenikumbuka out of nowhere wins a lot....Ukienda mahali ukakuta kitu kizuri,buy for her...buy her a gown,buy her shoes..buy her earings...buy her a nice watch...wala haicost milioni....Mpelekee...Hakutegemea,ila umemkumbuka....Uchawi mnooo!Wanawake wanapenda vitu vinavyoonekana,ili waringishie...akiambiwa saa yako nzuriiiii...its from my boy...See that! Buy her a good card ya Love...Sio mpaka Valentine ndo unajifanya una mahabaaaaaaaa,be different,be unique.....hata teddybear si mbaya,si unajua wanapenda kuweka room kwao...atakumbatia usiku,na atakuwa anakuwaza wewe,maana ndo umenunua!

4.Be proud of her ukiwa around marafiki zako.Atajisikia vibaya kama humtambulishi,ataanza kuhisi yupo uliyemtambulisha ndo maana yeye unampotezea...Mara moja moja ukiwa unahang na friends,be with her,ili pia kuweka Safety deposits,ukisema uko na Juma awe anamjua na kujua my man is safe...Sio niko na Juma,hamjui,anamsikia tu kama mmakonde anavyomsikia Santa Claus..Imaginations fulu.

5.Mtambulishe kwa ndugu zako,hata kama hujampeleka kwa wazazi...Atafeel vizuri kujiona amekuwa part ya familia yenu...Anaanza kuifeel ile bond ya upande wa pili,ajue mawifi wakoje,wanamchukuliaje...Maana mawifi wana visa,unaweza kumficha halafu mawifi siku unaoa haziwaki na mkeo,na unajua mawifi wakinuna na ndoa yaweza kununa mwanzo mwisho...Atajisikia vizuri kuona anakubalika kwenu...Its a point

6. Epuka ugomvi unnecessarily...Wanawake ni watu wa kumind vitu vidogo na sometime unaweza ukashangaa,hata hiki amemind???Yes,ndo walivyo.Wachukulie hivyo,ndio udhaifu wao,unaweza kuchelewa kujibu SMS ikawa bonge la ishu...Hujapokea simu...Bonge la Ishu....Amekupigia usiku amekuta Call waiting...Bonge la issue,lakini kumbe hukudhamiria.Huna haja ya kumuwakia,kujaribu kumuelewesha kitu ambacho tayari akili yake imegoma kuelewa.AM SORRY ni uchawi unaofaa hapa...Mwambie Sorry babe,najua umemind lakini sikudhamiria hili litokee,nisamehe,tuongee mambo mengine.Am sure hatanuna,ila ukijifanya una point na unataka uwe Mshindi,jua itakula kwako.Utahisi umewin hiyo battle lakini in actual sense umejipunguzia point sana.Hao ndo wanawake,wameumbwa ili wabembelezwe kama Wanasesere!

7.Mpe hela asipotegemea.Wanawake wana needs nyingi,especially wale ambao bado wako shuleni ama chuoni,si kila kitu wazazi wake wataprovide.Sisemi ujiunge na Bili,lakini kwa kuelewa kwamba kuna hiki na kile atahitaji mfurahishe...Jipinde mara mojamoja,mpe pocket money kidogo,atanunua kitu alichhotamani sana kununua na hakuwa na hela,na atakushukuru a million times...Thats how you win.Usihisi umekuwa buzi,and afterall hela ya kupanga mwenyewe bila kuomba haiumi kiivyo coz utaitoa from your heart.

8.Mbusu mahali asipotegemea....Tembea nae kwa uhuru na umpe uhuru wa kukushika...Nenda nae outings sehemu romantic,for a dinner or lunch....Kuna mahali ha-expect wewe utambusu,mbusu hapo!Atashangaa,,,anaweza kusikia aibu,but the kiss will stick to her memory,that he actually did that! Wengine hampendi kushikwa eti aibu,aibu kwa mpenzi wako nani kasema??Mpe uhuru,anapenda,mwache ajivinjari maana anaamini yeye ni mali yako,maadamu hakukumbatii kanisani au mbele za wazazi wako,ila mtaani,kwa raha zake mwache ajiachie.

Hii ni kwa wale mlio serious,kama we ni mtu wa vimeo,huna direction na huyo mtoto wa watu wala hata usijisumbue kusoma maana haya yote utaona utumwa tu,ila kama una mtu serious,na una mpango wa kuwa nae in future as ur baby mama,Follow this and you will tell me!