Wednesday, June 20, 2012

SUPERSTAR WA MUZIKI..WA UKWELI..CHEKI UTAJIRI WAKE...SIO UNA VITZ UNASEMA WEWE STARHuyu jamaa anafanya Muziki...Sio bongofleva,ni Hip Hop...

Ni CEO wa kampuni ya Muziki inayoitwa Cash Money Records ambayo ina wasanii wakubwa kama Drake,Lil wayne na Nicky Minaj

Amezaliwa miaka 43 iliyopita na wazazi wakampa jina la Bryan Williams

Fans wake dunia nzima wanamfahamu kwa jina la Birdman...Ana watoto wawili Bria,na Brian JR.

Mpaka kufikia Mwezi April mwaka huu, Birdman alikuwa na utajiri unaofikia Dola Milioni 125 ambazo ni zaidi ya Bilioni 200 za madafu..

Mwaka huu alimpa zawadi mwanae wa kufikia,Lil wayne gari aina ya Bentley Mulsanne na yeye akajinunulia 1 la kufanana nae...Hakuishia hapo,akampa na zawadi, Rasi wa Young Money Records, Mack Maine Rolls-Royce mpya...Mack Maine hakuamini macho yake na akakiri hiyo ni ndoto ambayo hakuwahi kuota kama Birdman anamthamini kiasi hicho..

Kwenye Listi ya marapa wenye mkwanja mrefu duniani, Birdman amezidiwa na P.Diddy mwenye utajiri wa dola milioni 550 ambaye amekaa kwenye number 1 slot kwa mwaka wa 2 mfululizo. Listi ya marapa matajiri inafuatiwa na Sean Carter au Jay Z kama anavyofahamika akiwa na utajiri wa Dola milioni 460,halafu Andre Young au Dr Dre mwenye dola Milioni 260 kisha anafuata yeye,na anayefunga Top 5 ya mkwanja ni Curtis Jackson aka 50 Cent mwenye wallet ya Dola Milioni 110.

VITU USIVYOJUA KUHUSU YEYE

Birdman anaishi kwenye nyumba ya Dola Milioni 30 huko New Orleans,Louisiana...CHEKI HOUSE HIYO

Mwaka jana alinunua gari aina ya Bugatti Veyron kwa Dola milioni 2.5 ambazo ni bilioni 3 na ushee za madafu...Wiki iliyofuata akanunua Pete ya thamani ya Bilioni 3.Wiki moja akaspend Bilioni 6...Hapo vipi??Ni moja kati ya magari ya Bei mbaya zaidi duniani na ni wachache sana wameweza kununua akiwemo yeye,Christiano Ronaldo na Kanye West..HILO HAPO CHINI LICHEKI...
BUGATTI KWA NDANI


MUZIKI UNALIPA BWANA..UKIFANYA KWA MOYO,KWA KUJITUMA NA KWA HESHIMA

Ni baba wa kufikia wa Lil Wayne

Wakati Katrina Hurricane ilipopiga nchini Marekani, Birdman alipoteza Nyumba 20 na magari 50 kwenye Kimbunga hicho...Hakumind,akanunua mapyaaaa!

Ofisi ya Label yake ilibidi ihamishwe kwenda Miami baada ya Katrina kupiga almost kila kitu

Birdman ni Fan mkubwa wa Justin Bieber na amekiri hilo mara kadhaa

Hununua magari 100 kila baada ya Miezi 6..Na yale ya Zamani anagawa kama Zawadi


Mwaka huu,2012,amenunua gari kwa Special Order,aina yaLamborghini Aventador lenye thamani ya Dola 800,000 ambazo ni Bilioni 1.3 kwa madafu..HILO HAPO CHINI....Kama haitoshi Birdman alikaririwa akisema ameweka Oda ya gari litakalotoka December mwaka huu aina ya Maybach Exelerro lenye thamani ya Dola Milioni 8 ambazo ni Bilioni 15 za madafu na ni lazima awe nalo ....LAZIMA UCHOKE...HILO HAPO CHINI
Halafu wewe ununue VITZ useme wewe Star???Hebu mtupishe
3 comments:

  1. Hao ndio masuperstar sio hawa wetu kujiona sana tu, kazi kuchukua vitoto vya disco kila siku

    ReplyDelete
  2. mhh jamani sasa wamfumbia nani hapo?na vitz yake?lol

    ReplyDelete