Muhammad Hosni Said Mubarak: MAISHA YAKE HADI KIFO CHAKE
Wakati akihukumiwa kifungo cha Maisha wiki 3 zilizopita,niliwaambia rafiki zangu fulani tukiwa pale mlimani city kwamba huyu jamaa hatamaliza Mwaka....kumbe hata Mwaka it was too much...Hajamaliza hata Mwezi tu....Alizoea maisha ya Starehe mno,ya kitajiri mno,kuishi jela ni zaidi ya kitu alichotegemea in his life...Alitegemea kuishi kifahari maana ana kila kitu Binadamu anataka humu duniani...
Hosni Mubarak alizaliwa kama mtoto wa wakulima katika kijiji cha Kafr-El-Meselha kwenye mkoa wa Monufia uliopo Misri ya kaskazini. Baada ya shule alijiunga na jeshi la anga la Misri akawa rubani akasomeshwa kwenye vyuo vya kijeshi huko Umoja wa Kisovieti Baada ya vita ya siku 6 akawa mkuu wa jeshi la anga la Misri.
Mwaka 1975 aliteuliwa na rais wa Misri Anwar Al Saadat kuwa Makamu wa rais. Sadat aliuwa mwaka 1981 na Waislamu wakali hivyo Mubarak akawa rais mpya. Kuanzia 14 Oktoba 1981 alishika vyeo vya rais wa taifa hadi mwaka 2011. Kuanzia 25 Januari 2011 wananchi wa Misri alianza kuandamana dhidi ya utawala wake na tarehe 11 Februari Mubarak alijiuzulu na kumkabidhi makamu wake madaraka yote.
Mubaraka na familia yake walikaa kwenye rasi ya Sinai lakini tar 24 Mei 2011 serikali ilimshtaki Mubarak pamoja na wanawe Gamal na Alaa na aliyekuwa mkuu wa polisi ya kisiri Hussein Kamal al-Din Ibrahim Salem kuwa waliwajibika kwenye mauaji ya waandamaji 800 wakati wa maandamano wa 2011, pia ufisadi na wizi wa mali ya dola. Kesi ilifunguliwa tar 3 Agosti na Mubaral alipelekwa kotini katika kitanda ya hospitali.
KUONDOKA MADARAKANI
Mubarak alikuwa mmoja wa watawala wenye mamlaka na nguvu zaidi kwenye eneo la Mashariki ya kati. Alifuata siasa ya rais mtangulizi Sadat aliyepatana amani na Israel. Utawala wake ulikuwa wa kidikteta.
Wananchi wake walipomchoka waliingia mtaani na kulazimisha aondoke,baada ya kuiendesha misri kwa Miaka 30.Alikiwa mmoja kati ya Maraisi walioongoza kwa muda mrefu zaidi duniani ukiacha Mugabe na Omari Bongo wa Gabon.
Hatimaye nguvu ya Umma ilipozidi akaamua kuachia madaraka na machafuko hayo yalisababisha afunguliwe mashtaka ambayo yamempeleka gerezani Wiki 3 zilizopita baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha na Mahakama ya Kijeshi nchini Misri.
HAPA AKIWA JELA KAMA ALIVYOPIGWA PICHA JANA ASUBUHI KABLA HAJAFA
UTAJIRI WAKE
Mnamo mwaka jana, ilikadiriwa kuwa Raisi Hosni Mubarak alikuwa mmoja ya Watu wenye hela nyingi sana na pengine mtu tajiri aliye hai kwenye bara la Afrika.
HAPA AKIWA NA MKEWE,WATOTO NA MKWE WAKE
Utajiri wake ambao alitajwa kuumiliki kwenye Benki za Kigeni ulikadiriwa kufika Dola Bilioni 70 ambazo ni zaidi ya Trilioni 120! USIPIME!
Utajiri huu ni zaidi ya bajeti ya Tanzania kwa Miaka 20 mfululizo...Mtu anamiliki yeye mwenyewe na Familia yake....Ila Mungu atabakia mungu tu,hela zote hizi na amekufa ameziacha,tena kwa aibu,akiwa gerezani anatumikia kifungo cha Maisha alichohukumiwa Wiki 3 tu zilizopita
FUNDISHO
Hela sio kila kitu...He was a president....He was powerful....He is stinky rich....Lakini amekufa akiwa gerezani.....Learn and be wise!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment