Monday, January 21, 2013

WASICHANA...EPUKA TABIA HIZI KAMA UNA MPANGO WA KUWA MKE WA MTU ONE DAY LASIVYO SAHAU

PLEASE I NEED YOUR SUPPORT...PLEASE!

Tuma neno SETH kwenda 15678 SASA HIVI kama bado hujajiunga na Huduma ya Seth Straight to Your Phone.Its next level:Ili kupokea Meseji hizi na zingine nyingi kwenye simu yako ya Mkononi popote ulipo kubadilisha mtazamo wako wa Kimahusiano na Kimapenzi na kufanya maamuzi sahihi ukiwa kwenye Mahusiano..Usisubiri ufunge ndoa ndio ugundue ulifanya makosa kuingia....Kujiunga ni BURE kabisa hutakatwa hela kwa kutuma Meseji hii.Wateja wa Mitandao yote ya simu Tanzania wanaweza kutuma SMS hii na HUTAKATWA hata thumni...

Narudia,Tuma neno SETH kwenda 15678...Please tuma SMS kabla hujascroll kwenda chini kwa somo la leo....NAWAPENDA1
....

.....


......


.....


.......

........

Naulizwa WHY GIRLS...Kwanini nawaandika sana...Jibu ni rahisi sana,Wanawake ndio vichwa vya nyumba kivuli....Baba ni kama Raisi lakini MAMA ni Waziri Mkuu...Mtendaji mkuu wa day to day activities za Home Government...Waziri mkuu feki ni hasara kwa nyumba..Lazima washibe neno haswa ili hiyo nyumba isimame.Baba bila Mama bora hakuna Familia....

I have a lot to share to girls,natamani Familia Bora sana kwenye Kizazi hiki cha Nyoka aisee,na sitoacha mpaka nione Ma-mama bora wakizaliwa huku mitaani....

Leo nna katopic tena kwa ajili yenu,Wanawake...Najua siku hizi mmepata Hobby Mpya....KUPENDA NDOA!

Hii Hobby inawacost sana maana hamu zimezidi uwezo....Mnatamani sana ndoa lakini uwezo na credits za kuipata HAMNA...Sasa miujiza hii ya Maji kugeuka Divai mara ya mwisho alifanya Yesu tu kule Kana ya Galilaya,sijasikia tena maji kugeuka Ndovu Tandale...You must work for it...Very hard...

Na jinsi gani unaweza kuwork...ni discpline tu...Manage ur attitude! Wengi wenu ni kama mshakata tamaa...Mnajiendesha tu kama Guta...Values za Mapenzi hamna tena...Miiko ya Mapenzi mnaivunja bila hofu...Mapenzi yamekuwa Useless,kwahiyo kwenu lolote ni sawa....SI SAWA!

Kuna tabia ambazo,kama wewe ni Mwanamke na unazo,SAHAU kwamba utakuwa mke wa mtu,labda huyo atakayekuoa awe Stevie Wonder...Namaanisha kipofu,poyoyo,hakujui amekurupuka tu..Maana Wanaume hao wapo pia wanadamka tu na kuzama dimbwini kisa Housing....Kaona una shape kajaa kimiani,kumbe angelijua.....Ange...ishakula kwake anajitia kitanzini!

Kati ya Tabia ambazo Wanawake wa Kizazi hiki wanazo,na hawajali,bila kujua zinawaharibia Pozi kinoma,na zinawapa kitu wao wanaita Gundu,kumbe Gundu wamelikumbatia wenyewe,na wanalisababisha wenyewe ni hizi hapa:

1.MWANAMKE SAJENTI WA JWTZ MAKUTUPORA

Tunawafahamu Wanajeshi..lugha yao nzuri na tamu ni AMRI....Lete...Kuja...Kwenda....Rudi...

Sasa Mwanamke tangu lini una Amri kama umekabidhiwa Kombania ya JKT???Mwanamke yake mapozi na politeness...Lugha tamu....Mwanaume hahitaji Amri maana nature yake ni amri tosha...Akumbane na Amri za Bosi wake,na wewe home umletee Amri.Sasa nani BABA??..KINANUKA FASTA!

Utawasikia,

We Papito Casto hivi huoni kwamba sina viatu??

We Kataza,si nimekwambia Sina Vocha???

Lugha nzuri zimejaa teleeee...Baby wangu sina vocha ai weweeeee,nitumie japo buku.Unamrembea mkaka Sauti,HACHOMOKI!....Mwanaume ukishamrembea sauti hivi hata kama hakuwa na mpango atanunua tena Buku 2 atatuma tu....Sasa wewe endekeza Amri uone,utabip weee,utaishia kuomba TIGO NIWEZESHE!

2.MWANAMKE USELESS

Role kuu ya Mwanamke ni USAIDIZI....HELPER....Hii ni Kibiblia kabisa,Mungu akaona si vema Adam awe peke yake,akamtafutia Msaidizi....Sasa wewe Mwanamke husaidii anything,badili tu jinsia yako!

Kama kuna jambo moja tu unaloweza kunyonga Hisia za Mwanaume na akakupenda maisha yake yote ni kama utatimiza hili jukumu vizuri....

Kuna watu mnakaa na Boyfriends wenu/Wachumba/Waume,hamjui anafanya nini...Ana wazo lolote la Kibiashara...Humsaidii kumpa Mawazo mfanye nini kuongeza Kipato....Sasa we wa nini kwenye Maisha yake????USELESS
Akitokea Shankupe anayejua hii Siri anamuiba fasta,utashangaa,Huyu Mwanaume kafuata nini pale kwa yule shosti hata Sura hana,NDIO,Sura hana,Shape Sony Wega ya Inchi 26 kama Mjapenga lakini ROLE KUU kapata 100% kwanini jamaa asikutose????Inakula kwako I guarantee.

Likikugusa badilika...Onyesha kwamba upo..Show ur presence...Mwanaume kila akikaa akihesabu Mafanikio anakuona upo behind this..Behind That..behind that and that one....Sasa kila kitu kafanya mwenyewe,hela hujachangia...Hata wazo???Come on Girls!!!You can do better than that.

3.MWANAMKE DEBIT AND CREDIT NEVER

Hawa ndo Kiboko yao! Hakuna wazo atakalokupa ambalo ni la kuingiza hela..yeye kila wazo lake ni la kupulusa kilichopo bila kujali kitarudije na zikiisha itakuwaje!Wanatumia ile 'Shauri yake Principle'

Baby twende Maisha Club Leo kuna Usiku wa Mabeste anazindua Album jamani,Nampenda kweli Ben Paul atapafomu....

''Baby uko Mlimani City??please nichukulie 'Tuna' Fish hapo njaa inauma kweli mpenzi..hata hujui ana hela au hana,kiruu!

''Baby,nimeona cheni nzuri kweli can i have 60 thou mpenzi wangu,mwaahh...Ulimpa hiyo 60 thou??Ilikuwa kwenye Plan???Is it necessary ununue leo????THINK!

''Honey,kuna Samsung Galaxy nzuriiiii nimeona dukani,kama ile ya BFF wangu Joanita''

''Mpenzi,hivi huwezi hata kuninunulia VITZ,kwakweli nimechoka Daladala''.....Umechoka daladala wakti mamako bado anapanda,tena za Tandika...acheni biashara kichaa,hailipi!

Sisemi usiombe hela au vitu lakini hakuna hata sentensi moja ambayo ni Income Generating inaweza kutoa kinywani mwako hata mara moja kwa mwaka ili huyu MKAKA akumbuke kwamba She did this last year????

Hata kusema mpenzi nimeona tangazo kiwanja kinauzwa can we go see it and buy tujenge when tukioana?? Au Mpenzi kuna this Business nimeona rafiki yangu amefanya inamlipa sana,can you think of doing it???

Wewe ni Debit Debit Mwanzo Mwisho,hakuna Positive hata moja???Halafu unataka huyu jamaa A-propose ndoa???Na unamkomalia kwamba mbona yuko kimya hasemi kitu mwaka wa 3 huu???Apropose kuoa DEBIT????Ah nani kasema,utasubiria Treni hapo Ferry,subiri hapohapo hadi usikie honi..Anakutafutia tu Timing ya kukumwaga,maana ur a Liability to him japo hakwambii!

4.MWANAMKE CHAUPEPO

Hawa kama ni graph basi inaongezeka huku ikiongezeka...Waingereza wanasema Increasing in Increasing Rate!VYAUPEPO!
Jumatatu yuko Samaki Samaki...
Jumanne yuko Club Rouge...
Jumatano yuko New Palm Bar kwenye Baikoko na Friends.....
Alhamisi yuko Ladies Free Billicanas...
Ijumaa yuko Elements....
Jumamosi yuko Runway.....
Jumapili yuko Skylite Band Thai Village.....
Ana Ratiba kama Mbunge wa Msovero!

Unajua kuna mambo Wanaume wanafanya,sawa,ila Wanawake mkiiga wala haifai...mtasema mbona Wanaume wanafanya,lakini ukweli unabakia palepale,Mwanamke Chaupepo wa usiku ana-raise lots of Question Marks...Lots.....

Mama wa nyumba ajaye,anapepea haifai,hata Bendera ya Mwenyekiti wa Kijiji haikufikii,Wiki nzima una mishe,hujali hela ngapi umetumia kama kweli ni za kwako unajitegemea,but it shows that HUNA FOCUS....

Na hili lina-apply hata kwa Wanaume,siku 4 kwa Wiki zote unatoka,hata kama unatumia 20thou kwa siku,still its too much...ukisave hiyo hela unanunua tofali za kutosha tu....Mtalalamika ujenzi shida lakini hela unazokula gambe ili bata ikuzoee ukiichange FOCUS yako kidogo utashangaa kibanda kinainuka taratibu...Siongei Rocket Science,inawezekana,Nimeona na ninazidi kuona....Change ur focus and things around you will change...MEN,HEAR THIS!

5.MWANAMKE ZEZETA/GOIGOI/KILAZA

Mwanamke lazima awe Sharp...Bed...Jikoni...Everywhere! Make your Man proud of YOU!!Ukiwa Sharp hata mmeo atakusifia kwa rafiki zake,hiyo kafanya mama flani bwana....Sasa mmeo hana hata kimoja cha kukusifia....Bed pia uko shallow na you dont bother kujifunza wala,unaona utaaaammmm...Mh mama,wataka ndoa ama ndoano???

Mkisoma Sifa za Mke mwema kwenye Biblia ndo mtajua....Mke sio Sura au Shape,hata Punda ana shape...Mke shurti uwe SHARP.....

Kuna nyumba ukiingia tu unajua Mke KILAZA...liko wazi....Mwanamke Sharp hata ukifika kwake utaona....iko clear na kilaza iko clear...
Kuna watu wanaoa vilaza wanajuta...Mke hajui kupika,kutwa alikuwa anashinda vibanda vya chips na kula burger...Kisa ana shape umeweka ndani,dadeki bonge la pancha,muda wote anatengeneza kucha...Mwanamke kufua hawezi/hataki eti ataharibu kucha....Mwanamke anajua Kuoga na Kuvaa tu....Mwanamke kupika hawezi anamuachia Housegirl kila kitu....mahausigeli siku hizi ukizubaa tu MESSI huyooooo kapita,unapinduliwa Uganda hivihivi na IDD AMIN upo hapohapo!

Mwanamke kitanda akutandikie Housegirl????Halafu unategemea nini???Kama Housegirl anashine in the eyes of your Man kwamba yeye ndo Masterplanner wa House,Mmeo atajuta kwanini alikuoa wewe ni afadhali angem-turn Housegirl into a Wife....

Tafadhali,Think Twice,Ndoa sio kama Vinyweleo kila mtu anavyo...Zile Zama zimepita....Utabakia kutegesha Mimba huolei Ng'o maana huoleki...

Kama una hizi Tabia BADILIKA lasivyo chagua,ama UJIOE au UOLEWE na Same type of Stupid Man as ur maana mtakutana wote level za Ngassa na TEgete...ASANTE!

9 comments:

 1. asante sana, nimefurahi kwa kweli kuna mambo yamenifungua akili yangu

  ReplyDelete
 2. i realy like your blog, but do you practice what you preach?

  ReplyDelete
 3. mpasheni,i will be stupid if i dont do what i write,God forbid

  ReplyDelete
 4. Honestly u have made my day coz Every thing u said It's means a lot! Good Advice!

  ReplyDelete
 5. seth u r soooo damn good, this stuff u write r soo true, am with u 100 percent keep up the good work my broda

  ReplyDelete
 6. najifunza lots of things kwa hii blog,much blessing seth

  ReplyDelete
 7. True, somo zuri limeeleweka. lakini pia wapo wanaume wenye sifa kama hao wanawake MARIO waseme nao.

  ReplyDelete
 8. Its real umemtelekeza mtu na kitambi jaman florah lyimo blog nimeona nimeanza kukuchukia

  ReplyDelete