Wednesday, May 16, 2012

KUPENDA USIPOPENDWA NI SAWA NA KUSUBIRI BAJAJ ZA SALASALA AIRPORT,HAPO ZINATUA NDEGE TU

Kumpenda mtu asiyekupenda ni kama mwanafunzi wa HGL kufaulu mtihani wa Hesabu,inabidi uwe na moyo mgumu kama bati la Alluminium..

Kwakweli inabidi kabla hujafall mzima mzima kama furushi la nguo chafu upime angalau kuna lita ngapi za Love kwenye tenki la huyo mtu,unaweza ukaanzisha safari ya Sumbwanaga kumbe gari ina nusu lita,ngoma itabuma hapo kimara Korogwe...

Unajitahidi we kujishaua,kumuonyesh...a unampenda,unarudi home na zawadi, unamletea Ma-Apple anakwambia ye anapenda Parachichi,Ukileta Sausage anasema anataka mayai,mwishowe utamletea mayai atakwambia anapenda mayai viza,ilimradi tu vululu vululu...Najua kuna wengi tu mnateseka kupenda msikopendwa maskini,mnajitahidi kushow Love weee mnakumbana na Steringi wa Vampire Diaries,somo halieleweki,unabaki na hope tu Labda...Labda One day atakupenda.
Ni kama vile mko Airport mnasubiria Bajaj za kwenda Salasala,utakesha hapo,zinatua Ndege tu

No comments:

Post a Comment