Monday, June 11, 2012

UKIGUNDUA MPENZI WAKO ANACHEAT FANYA HIVI

Nimepata kushuhudia Mahusiano mengi yakivunjika baada ya mdudu huyu anaitwa Cheating kuingia hapo katikati..

Cheating ziko za aina 2...Kuna cheating ya kuhisi kutokana na Mazingira,na Cheating ya kukamata nyama mkononi mwa Fisi...

Cheating nyingi ni hizi Type 1..Wivu na mazingira fulani yanayomfanya mtu ahisi kwamba Mpenzi wake ana kidumu au vidumu vingine zaidi yake..Mtu anaamua kususa kutokana na Hisia tu..au wivu tu..

Hii type 2 ndo ile unakuta ushahidi usiopingika...pengine ni SMS kwenye simu yake(ingawa huruhusiwi kusoma maana simu sio yako) au kumkuta laivu bila chenga na kuprove

Kuna mambo nataka tujifunze kwenye huyu mdudu anaitwa Cheating...Mazingira tunayoishi kwenye zama hizi yanapelekea vitu vingi sana na mahusiano mengi kubinuka chali...Kuna Simu...Kuna Emails...Kuna Facebook....Kuna Twitter,na mitandao mingi sana ambayo inasababisha balaa..

TUANZE NA TYPE 1: WIVU NA HISIA CHEATING

Mathalani,umepekenyua simu ya mupenzi na unakuta meseji kutoka kwa mtu usiyemjua,amemuandikia kitu ambacho wewe kwa definition yako unahisi yule ni mpenzi....Kwa mfano neno "MPENZI NAKUMISS KWELI",halafu wewe unakurupuka unaiba namba yake kwa siri unampigia,"we nani,kwann unamtumia mpenzi wangu meseji koma kabisa tafuta wako"...Khaa!Halafu uanrudi kwa Mpenzi wako unamnbwatukia,Lione kwanza kazi kutangatanga tu na nimeona meseji za huyo hawara wajo ntamng'oa masikio....Unashangaa mtu anakaa kimya anakushangaa....Kuna aina nyingi sana za kuwasiliana na watu mbalimbali,si kila anayemuita Mpenzi huyo mupenzi basi ni Romantic lover...Utapotea bure,utabwatukia mtu kumbe anamuita hivyo Cousin wake au Rafiki wa kawaida waliyezoeana kuitana hivyo kitambo,tena wengine tangu hata kabla yako wewe kujuana naye,utaonekana boya....

Rule number 1...Epuka kupekua simu ya Mpenzi wako...inakusaidia nini kugeuka FBI wa Mapenzi??unalipwa???Hakuna utakachokumbana nacho zaidi ya Stress tupu!Kuna vitu utasoma,ni vya kawaida kwake ila kwako vinaleta ladha tofauti,yenye ukakasi,utaibua wivu na moto mwingineNi sawa na kujaribu kufungua bomu bila kujua waya gani wa kukata,litakulipukia tu..ACHA!Kama unatamani upolisi nenda CCP Moshi ukasomee,sio kuwa Polisi wa Mapenzi,itakucost!

Mambo ya kufanya
1.Muulize huyu mwenye hii style ya uandikaji kwako ni nani?Na approve ni nani,kama sio kimeo chake,tena kwa upole bila jazba na kwa timing nzuri..bedtime huwa ni wasaa mzuri wa kuuliza hili,when ur both at ease
2.Muulize kama anaweza kubadili style ya kuitana na huyo mtu majina ambayo anakuita wewe ili kuepusha rabsha siku za usoni(kwa upole na sio kumcommand),maana wivu hauishi leo wala kesho,isije leo akajitetea ni Couzn halafu siku nyingine akatuma mtu kumbe ni kimeo halisi na sio Couzn ukajipa moyo ikala kwako
3.Jaribu kumueleza madhara ya aina hiyo ya Communication na athari zake katika situation kama hiyo

Epuka kulipuka kama Oryx bila kujua ni nani na kukimbilia kuhukumu bila hatia...Mapenzi ni Sanaa na Sayansi kwa pamoja,usitumie Sayansi ukasahau Sanaa,utapotea...

TYPE 2:RED HANDED CHEATING
Lakini,kama umeprove kwamba ni kweli mpenzi amecheat,Solution sio kukurupuka na ugomvi...Tena unaitwa Ugomvi wa bei rahisi..Unampigia huyo mtu unatukana,unamuuliza maswali kama Questionnaire ya Angaza...
1.Anakuona wewe looser,maana amekuibia,na bado umepanic...TULIA...Usireact on the spot,kaa chini fikiria kwanza...
2.Hata huyo mpenzi wako atakuona wewe kanyaboya,huna hekima na hujiamini...Kama unajiamini yeye ni wako huwezi kutumia mbinu kama za kimada kusolve ugomvi wa mme/mke kwa situation kama hiyo,whether ni moja 2 au mara elfu...Cheating haina alama

Maswali ma3 makuu ya kujiuliza kwenye Situation kama hii

Nini sababu ya yeye kucheat???Anayecheat nae yukoje???Amekosa nini kwako hadi aende kule??Kosa ni langu,lake,au letu??Wengine hucheat kwa sababu mpenzi wake yuko aina hii,au kwa sababu Communication between nyie wawili haimpi nafasi yeye kukuelewa na kuelewana,anajikuta anapata aina hiyo ya communication kwa mtu mwingine,hapo kosa linakuwa lenu...

Haya ni maswali ma4 makuu ya kujiuliza...Na sio kupiga simu kumtukana...au kumlipukia mpenzi wako na vitisho vya Its Over....Ameshasikia ITS over Milioni 8 na Laki 7 tangu azaliwe,yako wala haitamtisha,utaenda na huko na utatendwa vilevile,utakimbia Cheating Ngapi??Kwa watu wangapi??THINK...

Ni ngumu kufanya hivi lakini some cheating reasons huwa zinachangiwa kwa asilimia 30 na WEWE...Jua wapi ulikosea,jua wapi amekosea,then tafuteni WAY FORWARD...

Kuvunjika kwa Koleo sio Mwisho wa Uhunzi....Cheating sio mwisho wa Maisha,it can happen at anytime...inaweza kuwa kosa lako,au kosa lake,au kosa lenu...Cheating is not justified in anyway lakini ni jaribu ambalo kama kweli mna nia ya dhati ya kufika kule mnataka kufika,sio sababu ya kuachana wala kutukanana....Its hard to see your partner sleeping with someone else lakini ndio hivyo,Hakuna Mapenzi rahisi duniani...Usione watu wameoana ukadhani ni rahisi rahisi tu,au they are all perfect...kuna watu wamegundua,aidha wake zao wamecheat na wana ushahidi lakini wamestick to them,mpaka hao wanawake wakabadilika na kuwa vile wanavyotaka....na wanaume hali kadhalika.

Inaaminika wanaume wanacheat zaidi kuliko wanawake ingawa sidhani kama ni kweli au kama ni kweli ni kwa asilimia ngapi...mimi naamini anyone can cheat at anytime given that ana sababu ya kumfanya acheat,so, whether ni Mwanaume au Mwanamke,wote ni sawa tu!

Kamwe Cheating haiwezi kuwa solved na decison ya hasira inaitwa ITS OVER...ukiona daladala limeandikwa ITS OVER usipande!


No comments:

Post a Comment