Tuesday, October 30, 2012

WHY DO MEN LIE???

Hahahahaaaa!!!!

Mniruhusu nicheke kwanza....Girls, you wanna know????

Sababu chache kwanini Wanaume ni waongo hizi hapa:

1. WANAJUA

Uongo wa Mwanaume ni kama muvi...Kabla hajadanganya anapanga angle zote na majibu,ana-anticipate ataongea nn,utamjibuje,utamuuliza nn,na atakujibu nini...Wanawake hamuwezi,huwa mnapanic,na siku zote ukipanic umefeli

2. HATA TUKISEMA KWELI MNADHANI TUNADANGANYA

Hii ndo ilivyo,na inaudhi...Kwa sababu tunadanganya sana,hata pale tunaposema kweli basi nyie mnatuona wezi...So hakuna maana kusema kweli,bora tuendelee na PHD ya uongo tu-graduate

3.  WANAWAKE WANAPENDA UONGO

Japo hawasemi lakini hili tumeliprove,Wanawake ukimwambia uongo ndo anapenda...whether kwa kujua au kwa kutokujua...Ukimwambia ukweli anakuona hamnazo...Ukimwambia Mwanamke kweli utajuta....Itakuwa ndo wimbo bora wa mwaka...Masimago na Rewind button...Mwaka mzima,ukikosea tu wanarewind ulichokiri..

Waulize Wanaume waliowahi kukiri kucheat wakusimulie,wanajuta kwanini walikuwa na mahaba kuliko Bwana yesu...

4. UONGO KWENYE MAPENZI  NI NDIMU KWENYE SUPU

Mapenzi ni sanaa na sayansi....Mapenzi sio engineering!

Kama ndimu kwa supu ndivyo Uongo kwenye mahaba...kuan vitu unajua umedanganywa lakini unatolewa macho makavu inabidi uwe mpole..inabaki kama drama,na inaleta ladha flani ambayo ni ngumu kuielezea,japo wanawake wanaweza kuielezea how they feel pale ambapo wanajua wamedanganywa lakini hawana proof kwamba ule ni uongo...Mwanaume anashinda kirahisi...inabakia kama assignment flani hivi kwa Mwanamke kwamba next time lazima awe wise kidogo kumkamata...Na hiyo ndo ladha yenyewe na vionjo vya mahaba

SISEMI MDANGANYE,ILA NDIMU KIDOGO TU SUPU IPATE KUKUPA HAMU

WANAWAKE WAKICHEAT,WANA SABABU 4 TU,SI ZAIDI YA HIZO..HIZI HAPA

Ni ukweli usiopingika kwamba CHEATING is now a National Anthem...Kila mtu anaongea...kila mtu analalamika...Mapenzi na relationships yamekuwa magumu kwa sababu watu wanaogopa kuhusu ukweli na uaminifu wa wenza wao waliojitoa kwao kuwa in love...

Watu wengi(ikiwemo mimi), wanaamini kwamba Wanaume ndio wanaongoza kwa kucheat...The reason behind is, Men cant get enough...Every time is tea time using any cup....Lakini pia,Mwanaume akicheat(in most times) hamaanishi kihisia tendo analolishiriki isipokuwa kujisatisfy hamu...Ndio maana,wanaume wanaweza kufanya mapenzi na mwanamke hata hamjui jina na wakaachana hawajuani majina....Thats not the motive..Jina la nini???

Leo sikuja kuongelea hilo.....Today, Lets talk about Reasons which make WOMEN(Ambao wao wanajinasibu kwa kuwa waaminifu kwenye mahusiano), japo ushahidi unaonyesha nao hawavumi lakini wamo.

Achana na Magumegume/Micharuko/Vicheche/Maharage ya Mbeya....Kwa wale wanawake ambao wako kwenye mahusiano na wanaya-value,ikitokea wakacheat,basi wanaongozwa na Reason zifuatazo:

1.MATATIZO YA MWANAUME ALIYENAYE.

Hii huwa ni Lomg-term.Wanawake wameumbwa na software ya ajabu sana,wana uwezo wa hali ya juu ya kuvumilia....Kiu ambacho Wanaume hatuwezi! Wanavumilia mpaka vile visivyovumilika kirahisi....Kama Mwanamke ni mwema na mwaminifu lakini akapata Mwanaume ambae hamridhishi kwa kiwango anachotaka,na akashawishiwa aidha na roho yake,au mashosti,kwamba She can get something better...after a period of time ya uvumilivu,ATACHEPUKA....Ingawa roho itauma maana hajazoea,hakupenda iwe,lakini aliyekabidhiwa jahazi anasinzia,basi atampa mwingine mwenye uwezo wa kusimamia kucha,na akiisimamia vema basi ujue huyo si wako tena

2.REVENGE KWA HISIA KWAMBA UMEMCHEAT

Hii nayo ni Long-term....Ukimcheat Mwanamke na akajua,itamuuma,lakini atasamehe(kama kawaida yao),itaendelea kumhunt ndani kwa ndani....Inawezekana kwa muda flani asipange kufanya lolote,lakini endapo litatokea jambo akabananishwa kwenye kona ambayo uwezekano wa kuchomoka ni mdogo,basi anaweza kutumia justification kwamba 'afterall mbona flani alinicheat',akajikuta anafanya ili kuweka mlinganyo sawa.Hii ni dhahiri....Wanaume,make sure you dont pin your girl in this corner,kwa sababu akianza na ikatokea jamaa amesimamia show vizuri inaweza kuwa mwanzo wa series ya yeye kucheat kwa kutumia justification ileile moja uliyomfanyia,na itakula kwako mazima...Itachukua muda kuanza lakini ikianza haisimami!

3. KAKUCHOKA-NO MORE SPARKS OF LOVE-NO EXCITEMENT

Kwenye mapenzi kuna kuchokana,hilo liko wazi...Kama imefikia hatua ile spark iliyokuwa between you imeanza kufifia na hakuna njia mnayotumia wote waili ku-ignite pendo lenu upya,Mwanamke huyu anaweza kuanza 'kuwaka' na wanaume wengine wa nje,na akajikuta anatumbukia kwa mmoja au wawili ili kuweza kusaka Spark mpya.Wanawake wanapenda content...Sparks na excitement kwao ni kama Pie 22/7...Ndio maana haijalishi Mwanamke umemfanyia Shopping mara ngapi au umemnunulia zawadi mara ngapi,kwake kila Shopping au zawadi ni NEW EXCITEMENT.
Akiikosa kwako,akaipata kwa mwingine,usimlaumu kwa kuchangamkia nje kwa sababu ni wewe uloiyeshindwa kusoma alama za nyakati na kushindwa kumpa sparks anazozihitaji....MEN.,play your part well.

4.KIPATO vs DHARAU NA WOGA

Hii hutokea pia,japo ni 50-50...Si wanawake wote wakipata hela wanabadilika na kuanza kuwadharau wanaume wao,ingawa in reality Mwanamke akikuzidi hela,wewe kama Mwanaume unaanza kufeel weak hata kabla hajasema...Utashindwa kuperform kwa inferiority uliyoijenga mwenyewe,na Mwanamke huyo akiiona inaweza kumchange na kujihisi more superior....
Akianza kupata feeling ya Superiority ataanza kumingle na Superior men ambao watampa new adventure ambayo wewe Mwanaume wake hauna....TROUBLE! Pamoja na hela zake,atajikuta anahudumiwa vitu ambavyo ww huwezi kumpa,atapelekwa trip za dinner Dubai bila wewe kujua na huwezi....Ataliwa hukohuko na hatasema...Slowly, ur love will die...Sio kwa sababu alipenda,ila Inferiority yako ilikumaliza mwenyewe.
MEN,Ikitokea mwanamke uliyenaye amekuzidi kipato,ONGEENI,mlijue hili linaweza kuwa tatizo na mjue how to go about it lisiwaletee shida,ili mwanaume na mwanamke muwe at peace na kila mmoja aheshimu nafasi ya mwenzie kama mlivyokuwa mwanzo