Thursday, July 19, 2012

UKITENDWA NA MTU ULIYEMPENDA FANYA HAYA

Karibu kila mmoja wetu ametendwa,kwa namna moja au nyingine..Ni wachache sana ambao waliingia kwenye Mapenzi na wakafanikiwa kuoana na hao wapenzi wao bila kuhama baada ya kuumizwa na First Lover wake...Ila wengi tushahama nyumba kama 8(kadirio la chini) ndo kufikia hapo tulipo sasa

Uhamaji huu ni kwa sababu wale tunaowapenda,aidha hawatupendi in a same way,au wanajikuta wao wanatuhama,na hivyo inabidi tutafute nyumba nyingine ya kutusitiri...This is an on-going process,kila siku ya Mungu ipitayo,kuna Break ups,watu wanalia na kulia,kisha wanarudia tena...Ama kwa hakika Mapenzi ni machungu lakini watu wanayapenda no matter what...We keep on playing the Love Game despite of pains we get in the game...ila tutafanyaje sasa...Homoni ziko bize!

Wengi tulioumizwa na wapenzi wetu,wengine hatujaweza kusahau machungu ya First Men wetu...Thats true...Umempenda,ukamkabidhi bikira yako tukufu,jamaa akalikoroga,ukaachwa mataa ya Buguruni unashangaa..Unaishia kuwachukia wanaume...Haisaidii

Wale wanaume waliojitoa Mhanga,unampenda Mwanamke,unamzimikia(ambacho ni nadra sana Mwanaume kufanya),unamsomesha,unaingia gharama ukijua huyu ndio mkeo mtarajiwa,GHAFLA,linatokea jamaa kwa ulaini kabisa,linamwaga sumu baharini,Samaki wooooteee wanakufa...Huamini,umetumia gharama zote,na mahaba yote uliyompa kwa kujiminya kwelikweli,Sacrifice,hata babako hujawahi kumnunulia Batiki ili Mpenzi wako awe Clasic,jamaa kampitia fasta...Na demu anasepa huku anamwaga shombo kwamba HUJUI MAPENZI!Tusi kubwa sana kumwambia Mwanaume hili,atakuchukia milele,anaweza kukata roho huku anatukana jina lako.Umechukia wanawake,umeamua kuwakomesha,umekuwa Player,unawachezea na kuwaumiza wanawake kwa sababu ya Mwanamke mmoja aliyetibua nyongo,HAISAIDII!Na wala haitamaliza ile hasira,Kiu ya kuumiza itabakia palepale,hata uchezee wanawake 1000,atabakia moyoni tu!

SASA UFANYE NINI PALE UMPENDAYE SANA ANAPOKUUMIZA????

1.SAMEHE

Ngumu!Kila mtu anaguna aaargh,mi siwezi kumsamehe huyu Mwanaume,nimetoa Mimba zake 3 na bado kaniacha hana Shukrani!Hata ukimchukia ameshaenda,na ukimchukia hakutabadili zile mimba 3 ulizotoa ziwe watoto.Kumchukia kwako kunaufanya moyo wako uwe na Kinyongo,na hata ukikutana na Mr Right Man bado utakuwa na particles za woga na hasira,UTASHINDWA KUPENDA kwa moyo,kwa hofu ya kuumia...Dawa ni kumuachilia na kumtoa moyoni kwanza,hii itakufungulia mlango wewe kurudi kwenye Neutral Zone,ili Moyo wako uwe at ease,na love iendelee kuflow,lasivyo,utapishana na Muujiza wako wa Mme kisa una hasira ya jitu ambalo liko huko linakula zake raha,wewe huku unaendelea kuwa mtumwa wa Past.KAMWE,usiwe mtumwa wa Past,its gone,and you should move on!Hilo lilipita ili ujifunze kwamba wapo wa dizaini hiyo!

2.KUWA MAKINI KWENYE SELECTION

Usirudie kosa lile lile.Fanya screening ya kutosha(sio kama ya Questionnaire though),kama nia yako ni kuwa na uhusiano imara,kuna mambo ya kufanya.know the person better,familia yake,jua nia yake thabiti kwenye uhusiano huo,do some little test za kuprove kwamba he/she worthy it...ila isiwe too much...kuna tests huwa zinapiss off,unaweza kumpa mtu test akasepa,japo alikwa na nia...Ifanye kwa busara,usikimbilie tu mahusiano,ila kama unapass time,ize tu...Strong Relationships are built by Strong people...Jua level yake ya wivu,how anasolve matatizo yakitokea,ili ujue how to deal with taht person...Maana matatizo yapo tu,na wivu upo...jua Jealous level,jua Problem Solving mechanism yake...Ili yakitokea uhue fate.Kama ni mtu wa kupiga,au Mnunanji,Je,Uko tayari kuface Mnuno wa mwezi???Kama uko fit poa,go for it.Kama hauko fit usiforce,hata awe handsome au Gorgeous namna gani.Ndoa ni kimeo cha Milele,kuna vitu they look simple but in long run,they are so complicated....Msimamo wake wa Kiimani pia ukoje????Hili watu wanali-overlook sana,ila ni CRITICAL....Wote ni dini moja???Au mmoja Musilamu wewe Mkristo??Can u make it????Msichukulie poa tu,Tofauti za kidini mnaweza msione madhara yake ila ni msala...Watoto wakizaliwa ndo mtaona kazi,Wakwe watakuja juu,aitwe Asha au Neema,ndo utaona kazi..mtoto asali Msikiti wa Bin Jumaa au Lutheran Mbagala???THINK TWICE!

3.FALL IN LOVE
Baada ya choice kufanyika kwa umakini na una uhakika na mtu,Please FALL! Usianze maswali,sijui huyu atakuwa kama yuleeeee???Ah ah...ukianza questions tu,moyo wako hautafunga completely.Maadam umefanya Screening kwa uhakika,na kwa muda wa kutosha,na umesema huyu ndiye,basi FALL!

Ni balaa kushindwa kufall eti kisa uliumizwa nyuma,si nzuri kabisa...utajikuta kosa kidogo unakimbilia Break Up maana BREAK UP kwako ndio SAFETY ZONE.Hii sio njema.Umemchagua mwenyewe,Give Him/Her your all,and allow Him/Her to give asilimia zote za mapenzi kwako

4.TALK ABOUT YOUR RELATIONSHIP SO OFTEN AND CARE FOR MEMORIES

Ni vizuri kuongelea wapi mmetoka na wapi mnakwenda....Mara kwa mara ongeleeni how mmekutana,ilikuwaje...ingekuwaje kama msingekutana pale..Share how you feel for having him/her...Muonyeshe kwamba yeye ni wa thamani na ameleta mabadiliko kwako///

Kumbukeni Anniversary ya uhusiano wenu hata kama hamjaoana....Kama mlikutana April 15 kwa mfano,.Mnaweza kuwa mnakumbushana Kila Tarehe 15 ya mwezi kwamba mmetimiza miezi 6,au miezi 7...It shows kwamba ur happy with the relation...Lakini Pili,it shows kwamba you are going somewhere and you cherish the journey....

Trust me,This works...Hakuna ujanja mwingine wa kuwa na Penzi imara zaidi ya kulipenda penzi lenu kwanza....Epukeni maneno ya watu...Wakiona mnapendana wataanza chokochoko,utasikia maneno kuhusu Mpenzi wako...Mara hivi mara vile....Msiwajali,as long as nyie wenyewe wawili mnajua nini mnafanya na mnaaminiana,TRUST IS EVERYTHING...Kamwe msipoteze TRUST....Mkipoteza tu,amini amini nawaambieni,Mahaba yenu yatazama hapo KISIWA CHA CHUMBE!

Kwa leo inatosha!

2 comments:

  1. ahsante sana mwalimu kwa ushauri wako,mwenye kuelewa na elewe sasa..

    ReplyDelete
  2. Mwalimu hilo la kukumbuka anniversary nitalifanyia kazi.

    ReplyDelete