Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo.
Dokta Ulimboka aliokotwa katika msitu wa Mabwepande na msamaria mwema aliweza kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum  kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara,  kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote  watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na  sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo 
WAANDISHI WA HABARI WAKIMSIKILIZA KAMANDA KOVA
KAMANDA KOVA AKIONGEA NA WAANDISHI MCHANA HUU
Hii ndio hali ya dokta Ulimboka alipofikishwa Muhimbili Hospital.Inatisha aisee kama Tanzania tumefikia hali hii,amani iko wapi!
HAPA AKIWA NA WAZIRI MKUU PINDA..NA MIKONO WAKASHIKANA





No comments:
Post a Comment