Tuesday, June 26, 2012

ABIRIA ALAZIMISHWA KUKAA NA MAITI KWENYE KENYA AIRWAYS


Africa kuna mambo sana aisee.hii imetokea juzi tu hapa,Mwanamke mmoja raia wa Sweden alikuwa akisafiri kuja Tanzania kwenye Likizo yake kwa ndege ya KENYA AIRWAYS



Akielezea tukio hilo,mwanamke huyo anasema jamaa huyo aliyekaa nae alipandia ndege kwenye uwanja wa ndege wa Amsterdam.

Mshkaji alikuwa anaumwa na alionekana akitokwa na jasho jingi sana na kuchechemea,lakini alilazimisha kusafiri.

Muda mfupi tu baada ya Safari kuanza yule abiria alionekana kuzidiwa zaidi na wahudumu walijitahidi kuwa karibu nae muda wote lakini Izraili alionyesha Umafia wake wa ku-operate hadi angani,yule jamaa aliaga dunia wakiwa katikati ya Safari.

Mwanamke yule kuona vile ikabidi aombe kubadilishiwa Siti lakini kwa Mshangao akajibiwa kuwa ndege imejaa na hakuna popote wanaweza kumpeleka zaidi ya yeye kukaa palepale na ile maiti.

Masaa karibu 10 yule mwanamke alisafiri akiwa amepoze na ile maiti just next seat.

Mawanamke huyo,Lena Petterson,alipofika Dar es Salaam aliuandikia uongozi wa kenya Airways kulalamikia ishu hiyo na ndipo Uongozi ulipoamua kumrudishia Nusu ya Nauli yake kama part ya kumpoza moyo Mwanamama huyo.

Nauli aliyolipa Mwanamama Lena Petterson ilikuwa Dola 1400 na alirudishiwa Dola 700 kama Compensation kwa yeye kukalisha siti moja na Maiti na Mwanamama huyo alikubali Fidia hiyo na kuwa mpole.

Sasa kama hiyo ni Kenya Airways,ambao wako very smart kwenye operation zao,Usishangae Air Tanzania ukiambiwa ukae na Magunia ya Viazi uyapakate tena kwenye Siti,sitashangaa!

2 comments:

  1. U have make my day, Air Tanzania hawashindwi kukuambia ukae na gunia la viazi ha ha ha h ah ha ha ahh ah ah ah ah ha.
    Mdau

    ReplyDelete
  2. sky team inainclude Kenya airways but mbongo ni mbongo tu Kenya airways wanababaisha tu kama sisi, so sishangai wao kuweka maiti na abiria mzima, OMG siku nyingine unaweza ukafaulishwa toka KLM kwenda KA utashangaa hiyo difference.

    ReplyDelete