Wednesday, June 13, 2012

HOW TO WIN MOYO WA MWANAMKE-RISASI 8 MUHIMU KWA WANAUME

Mara nyingi nimesikia watu wakisema Wanaume hupenda kwa akili, na Mwanamke hupenda kwa Moyo....Huenda ni kweli,lakini mimi naamini kuna wanaume hupenda kwa moyo pia na kuna wananwake hupenda kwa akili...Hawa ni wale waliochoka kufall in Love na kuumia,wameamua kutumia ubongo kudeal na wanaume,na usiombe ukutane na hiyo type utajuta,...

Leo tuongelee mambo kadhaa jinsi ya kuwin moyo wa Mwanamke,,na Somo hili ni kwa Serious people ambao wanataka kuwa in serious relationships with commitments...

Mwanaume ni kichwa wa familia,theoretically,ila Mwanamke ni kiongozi wa Familia practically...Ukitaka bisha na upasuke, Wanawake ndio wanaoongoza familia kwa asilimia 90..wana vision na familia,wana planning ability...Wana budgeting ability,ya hali ya juu,na Leadership na hata ukuzaji wa watoto unamhitaji MAMA...tafuta mtoto aliyekuzwa na BABA uone kazi...Shughuli pevu

Ukitaka kuwin moyo wa Mwanamke fanya yafuatayo:

1. Tambua mwanamke uliyenaye ana tabia gani,anapenda nini na anachukia nini.Mpe anachopenda na usifanye asichopenda.Ni ngumu,kwa sababu wanaume huwa wanataka kuonekana vidume na hawataki kuishi kwenye amri za mtoto wa kike lakini kama una nia ya dhati ya kuwa na Strong and Solid relationship na Bond iliyotakata na Mwanamke,Make her win in whatever she wants...Ukimpa hili,wala huna haja ya kufanya muujiza mwingine

2. Mpe attention maana wanapenda,na ni wote,ukiona Mwanamke hataki attention yako jua kuna jamb nyuma ya pazia au wewe ni 2nd choice. Attention hii ni mkusanyiko wa vitu vingi...Kumjali hisia zake,kuzielewa wakati yupo down na kujua nini cha kufanya kumrudishia Smile yake,na wakati akiwa happy kujua jinsi ya kushare happiness yake.Haichukui dakika nyingi kumjulia hali asubuhi,Mchana,na Jioni...Ni ngumu kwa Mwanamke kuona wenzie wakijuliwa hali halafu wewe umeuchuna eti uko busy,Busy my Foot!

3.Surprise her! Hakuna Mwanamke hapendi surprise,bado sijaona,na anayejifanya hapendi anazuga tu...Na wala surprise yenyewe wala haitakiwi na sio lazima iwe expensive ndo iwe surprise...Ile feeling kwamba My boy amenikumbuka out of nowhere wins a lot....Ukienda mahali ukakuta kitu kizuri,buy for her...buy her a gown,buy her shoes..buy her earings...buy her a nice watch...wala haicost milioni....Mpelekee...Hakutegemea,ila umemkumbuka....Uchawi mnooo!Wanawake wanapenda vitu vinavyoonekana,ili waringishie...akiambiwa saa yako nzuriiiii...its from my boy...See that! Buy her a good card ya Love...Sio mpaka Valentine ndo unajifanya una mahabaaaaaaaa,be different,be unique.....hata teddybear si mbaya,si unajua wanapenda kuweka room kwao...atakumbatia usiku,na atakuwa anakuwaza wewe,maana ndo umenunua!

4.Be proud of her ukiwa around marafiki zako.Atajisikia vibaya kama humtambulishi,ataanza kuhisi yupo uliyemtambulisha ndo maana yeye unampotezea...Mara moja moja ukiwa unahang na friends,be with her,ili pia kuweka Safety deposits,ukisema uko na Juma awe anamjua na kujua my man is safe...Sio niko na Juma,hamjui,anamsikia tu kama mmakonde anavyomsikia Santa Claus..Imaginations fulu.

5.Mtambulishe kwa ndugu zako,hata kama hujampeleka kwa wazazi...Atafeel vizuri kujiona amekuwa part ya familia yenu...Anaanza kuifeel ile bond ya upande wa pili,ajue mawifi wakoje,wanamchukuliaje...Maana mawifi wana visa,unaweza kumficha halafu mawifi siku unaoa haziwaki na mkeo,na unajua mawifi wakinuna na ndoa yaweza kununa mwanzo mwisho...Atajisikia vizuri kuona anakubalika kwenu...Its a point

6. Epuka ugomvi unnecessarily...Wanawake ni watu wa kumind vitu vidogo na sometime unaweza ukashangaa,hata hiki amemind???Yes,ndo walivyo.Wachukulie hivyo,ndio udhaifu wao,unaweza kuchelewa kujibu SMS ikawa bonge la ishu...Hujapokea simu...Bonge la Ishu....Amekupigia usiku amekuta Call waiting...Bonge la issue,lakini kumbe hukudhamiria.Huna haja ya kumuwakia,kujaribu kumuelewesha kitu ambacho tayari akili yake imegoma kuelewa.AM SORRY ni uchawi unaofaa hapa...Mwambie Sorry babe,najua umemind lakini sikudhamiria hili litokee,nisamehe,tuongee mambo mengine.Am sure hatanuna,ila ukijifanya una point na unataka uwe Mshindi,jua itakula kwako.Utahisi umewin hiyo battle lakini in actual sense umejipunguzia point sana.Hao ndo wanawake,wameumbwa ili wabembelezwe kama Wanasesere!

7.Mpe hela asipotegemea.Wanawake wana needs nyingi,especially wale ambao bado wako shuleni ama chuoni,si kila kitu wazazi wake wataprovide.Sisemi ujiunge na Bili,lakini kwa kuelewa kwamba kuna hiki na kile atahitaji mfurahishe...Jipinde mara mojamoja,mpe pocket money kidogo,atanunua kitu alichhotamani sana kununua na hakuwa na hela,na atakushukuru a million times...Thats how you win.Usihisi umekuwa buzi,and afterall hela ya kupanga mwenyewe bila kuomba haiumi kiivyo coz utaitoa from your heart.

8.Mbusu mahali asipotegemea....Tembea nae kwa uhuru na umpe uhuru wa kukushika...Nenda nae outings sehemu romantic,for a dinner or lunch....Kuna mahali ha-expect wewe utambusu,mbusu hapo!Atashangaa,,,anaweza kusikia aibu,but the kiss will stick to her memory,that he actually did that! Wengine hampendi kushikwa eti aibu,aibu kwa mpenzi wako nani kasema??Mpe uhuru,anapenda,mwache ajivinjari maana anaamini yeye ni mali yako,maadamu hakukumbatii kanisani au mbele za wazazi wako,ila mtaani,kwa raha zake mwache ajiachie.

Hii ni kwa wale mlio serious,kama we ni mtu wa vimeo,huna direction na huyo mtoto wa watu wala hata usijisumbue kusoma maana haya yote utaona utumwa tu,ila kama una mtu serious,na una mpango wa kuwa nae in future as ur baby mama,Follow this and you will tell me!

2 comments:

  1. somo zuri sana yule anayeweza kuelewa na kutambua ni nini cha kufanya atakuwa na maisha yenye furaha....safi sana mwalimu kwa somo..

    ReplyDelete
  2. Aksante sana kwa somo zuri la kuelimisha

    ReplyDelete