Wednesday, June 13, 2012

RAISI BEN ALI WA TUNISIA AFUNGWA MVUA 20

Lile wimbi la Maraisi wa Zamani waliotumia vibaya madaraka kufungwa limeonekana kuendelea baada ya jana,Mahakama ya Kijeshi nchini Tunisia kuamuru Raisi wa Zamani wa nchi hiyo,ZINE EL ABIDINE BEN ALI kuamriwa kwenda jela kutumikia miaka 20 baada ya kukutwa na Makosa ya uhalifu wa kivita uliosababisha machafuko nchini Tunisia ambayo yalimlazimisha kukimbia nchi na kusalimu amri.

Kwa sasa Raisi Ben Ali anaishi uhamishoni nchini Saudi Arabia na itabidi arudishwe kuja kutumikia kifungo hicho. Raisi huyo aliamuru waandamanaji waliokuwa wakimpinga kupigwa risasi katikati ya January, 2011 kwenye mji wa Ouardanine nchini tunisia,lakini vurugu hizo hazikuweza kuzimwa na Polisi na hatimaye ikabidi akimbie nchi.Wasaidizi wake kadhaa nao pia wamehukumiwa kifungo cha kati ya miaka mi5 hadi 10 kila mmoja

Huu ni mwendelezo wa kichapo kwa Maraisi wa Africa waliotumia madaraka yao na kujiona wako Above Law,baada ya Charles Taylor kuhukumiwa miaka 5o wiki 2 zilizopita na Mahakama ya Uhalifu ya The Hague,akifuatiwa na Raisi wa Misri, Hosni Mubarak aliyehukumiwa kifungo cha Maisha jela japo yuko hoi hata Mwaka sijui kama atamaliza.

Hili ni fundisho kwa viongozi wa Africa kwamba Madaraka sio dhamana ya kutesa wengine, What Goes Around comes Around like a Hoola Hoo..

RAISI BEN ALI

No comments:

Post a Comment