Thursday, June 28, 2012

ILI UPATE MME/MKE MWEMA,KWANZA WEWE UWE MWEMA LASIVYO HUPATI

Kamwe huwezi kuingia kuchat Twitter na Nokia ya Tochi,unahitaji smartphone ili uweze kufanya hivyo...

 Hakuna Mmachame anayezikwa Dar makaburi ya Kinondoni,labda hana ndugu Machame wote wanazikwa Moshi,huo ni utamaduni..Huhitaji kuwa genius kujua hilo.

 Unapokuwa busy kutafuta Husband material na kujishaua unataka kuolewa na kwamba huna bahati,jiulize kwanza unaoleka wewe,are you a wife material???
 
Kabla ya kutafuta mme jiulize kama una sifa za kuwa mke wa mtu,ndoa sio kama vinyweleo kila mtu anavyo.Kama huna sifa ya nunua tu midoli ujikumbatie tu maana hutapata. be that best person that someone will see the best qualities in you first...Huwezi kuwa mfinyanzi halafu unatafuta udongo wa kichanga ujenge

 Unapotafuta wife material na kujishebedua jiulize kwanza una hadhi ya kuwa mme wa mtu wewe,are u a husband material??Unayaweza majukumu au unadhani kuwa na misuli na ndevu ndo una-qualify kuwa mme?
Kama wewe huna sifa za mke/mme bora tafuta kwanza sifa hizo kabla hujatusumbua na kelele kwamba ur looking for hubby/wife material.be the material that you are looking to have na ndoa itakuwa automatic maana tabia zako zitaongea na si maneno na kelele kama debe tupu
 
Tumekuwa na tabia mbaya halafu tunatafuta watu wema tuwaweke ndani,nani anataka uwe kichaka chake cha kuficha uhuni wako??Everyone deserves a better wife and a better husband lasivyo utatesa au kuteseka tu.
 
Huwezi kwenda Mbinguni kwa kupanda basi la Kariakoo...Njia ya kwenda mbinguni ni kuokoka tu,FULL STOP,bila hivyo mbingu utaisikia kwenye hadithi za Sunday school

1 comment:

  1. Utapewa wa kufanana naye tu.kama jangili utapata mwenza jangili,kama muhuni utapata muhuni mwenzio tu!

    ReplyDelete