Friday, June 15, 2012

CMB PREZZO AAMUA KUJITOA BIG BROTHER AFRICA

Vijimambo vinaendelea kurindima kwenye jumba la Big Brother huko Afrika Kusini!

Baada ya washiriki kutoka Tanzania kutia fora baada ya kutimuliwa mapema,na baadae mshiriki DKB kutolewa baada ya kumdunda mshiriki mwenzie makofi akimaindi kuchunguliwa bafuni,sasa imekuwa zamu ya msanii nguli wa kenya, CMB PREZZO!

Prezzo ameamua kujitoa kwenye jumba hilo baada ya sheria ya Mitungi kutoruhusiwa kwenye jumba na amesema yeye sio mfungwa hivyo ana uhuru wa kutoka muda wowote anaotaka!Msanii prezzo ambaye anapewa nafasi kubwa kuondoka na kitita cha dola 300,000 mwaka huu amemshangaza kila mtu pale alipomwambia mshiriki mwenzake Keitta kwamba ni heri afunguliwe mlango aondoke zake kwenda home kuliko kukaa kwenye Mjumba usio na Pombe kama Mfungwa.

Sijui kama Big Brother atamruhusu kusepa,ingawa kama itatokea itakuwa ni pigo kubwa kwa waafrika wengi ambao wanaonekana kumpa sapoti kubwa sana tangu aingie kwenye Jumba hilo kutokana na kuchangamsha sana kwenye mchezo huo!

No comments:

Post a Comment