Thursday, June 14, 2012

SABABU 7 KWANINI HUTAKIWI KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA JAPO NAJUA UNA MIHAMU GUNIA ZIMA NA UNAHISI HUWEZI KUACHA UTAMU HUO

Najua hii topic ni msala mtupu! Hilo nalitambua lakini inabidi tu hata hili lisemwe,usiponielewa leo utanielewa tu siku za usoni lakini usiseme sikukwambia


Mimi na wewe wote ni wahanga wa Pre-mature Sex...Kwa wale mliooa(nna uhakika wengi wenu kama sio wote) Mligonga kitu kabla ya muda,au sio?


Sasa mzigo ndo huu hapa...Kuna sababu 7 kwanini tunashauriwa tusifanye Mapenzi kabla ya ndoa....Vitabu vya Dini vimeandika hili na Kukataza lakini amri inavunjwa kama kawa utadhani Kitabu cha Kutoka 20:14 kimefutika kwenye Biblia....Kile kilichokatazwa ndo kinapendwaaaaa,kitamuuuuu,na watu hawataki kukubali kwamba inabidi kiachwe!


Ubishi huu kuhusu kula tunda ndio uliotucost Binadamu kufika hapa tulipo leo...Kosa lileeee la Adamu kupewa Tunda na Eva,baada ya Ibilisi kumdanganya Eva kwamba Tunda lina Mzuka ile mbaya na hata Mungu anajua ndo maana kawabania...uongo ulikuwa mtamu Eva akajaa kimiani..Matokeo yake ndo haya...Adam kafukuzwa Edeni,tumerithi Dhambi na kero chungu nzima...kifo hakikuwa kwenye Plan ya Mungu ila ni adhabu ya uleee uongo wa mwanzo,lakini HATUKOMI wazeee tuko bize kufanya REMIX ya mambo yaleyale aliyofanya ADAM na EVA kule EDENI halafu tunatetea eti haiwezekani,Mungu anajua alichoumba usimfundishe kazi!


SABABU YA 1:IMEKATAZWA NA MUNGU


Sababu ya Kwanza kwanini hatutakiwi kufanya Mapenzi kabla ya ndoa ni kwa sababu MUNGU HAPENDI....Amekataa...Na amekataa sio kwamba hajui Sex ni Tamu,....Anajua utamu woteee unaousikia ukifanya mapenzi...anajua raha unayopata ukiwa unacheza kile kiduku pale bed kwa mbwembwe...Anajua zile hisia unazofeel na nini kinatokea ukifanya,ANAJUA...yeye ndo ameziumba zile hisia,USIMFUNDISHE MUNGU KAZI YA KUUMBA! Alikuumba akijua una Hormone ambazo zitakusumbua lakini vilevile amekupa uwezo wa kuzishinda...Mungu hawezi kuweka jaribu ambalo halina Mlango,kama alisema usifanye basi anajua uwezo wa kutofanya upo!
Tutabisha weeee,ooh haiwezekani,kuna watu hawafanyi na wapo,wanapumua kama wewe,wanamtii Mungu na wanaishi..hawafi,na wanakuja wanaoa na mambo wanakula kama kawa...Zile stori usipofanya sijui ufutio unapotea,mara hivi,ni Plan za shetani tu kama alivyomdanganya Eva akajaa kimiani,anakujaza na wewe uamini ili upotee.USIKUBALI


SABABU YA 2:UTAMU WA HONEYMOON KWISHNEY


Utakapooa, utaenda Honeymoon...Nia ya honeymoon ni wewe kupewa fursa ya kutoa gundi kwa mara ya kwanza...Kumbe gundi umeacha Machimachi Guest House miaka mia8 nyuma


UNAENDA HONEYMOON KUFANYA NINI??KUMDANGANYA NANI??


Hizo hela za Kamati ya Maandalizi watu wanakuandalia kwenda Honeymoon wakati Ramani nzima ya huyo mkeo na mmeo USED unaijua hata ukifumba macho.KATAA HIYO!


SABABU YA 3: UTAKUWA NA AFYA KIROHO


Tunaishi kwa ajili ya Mungu...tuko hai kwa sababu Mungu ametuacha na kutupa nafasi ya kurekebisha maisha...Ukifa leo utakwenda wapi?Umewahi kujiuliza??
Hauko hai kwa sababu wewe ni mwema sana mbele za Mungu...As long as uko hai inabidi uishi vile ambavyo Mungu anataka uishi...MAISHA SAFI MBELE ZAKE!
Na ni ukweli usiopingika kwamba dhambi hii ya NGONO/UTAMU/UZINZI ndio namba 1 katika kuharibu maisha ya kiroho ya Watu...Hii dhambi ndo Weapon namba 1 ambayo Ibilisi anaitumia kumaliza watu.Laiti hii isingekuwa dhambi basi watu wengi sana wangeingia Mbinguni,Wengi sana...Lakini hali ni mbaya sana...
Naweza kuthubutu kusema Afya yako ya Kiroho inategemeana na ushiriki wako kwenye Ngono au La.ukishinda hii,siamini kuna dhambi itakuwa ngumu kwako kushinda,Jaribu uone!
Unaikosa Mbingu hivihivi kisa pale katikati....WAZA UPYA!Tangu uanze kuifanya hiyo kiu imeisha???Mbona unafanya na unafanya na kufanya haiishi,uskiacha utakufa??Its not late to start over,na uzuri wa Mungu ukitubu,anafuta zoteeee za nyuma unakuwa mpya.You can start afresh LEO!


SABABU YA 4:NI NZURI KWA AFYA YA KIMWILI


Hapa napo imekuwa mgogoro.mwanzoni watu walisema aaaah ntakaaje na Sweetie wangu bila kufanya,wakahalalisha...wamefanya weeeee wamechokana...wakaanza kuiba nje,na wapenzi wengine,na kwa sababu umekuwa sugu huoni tabu kuongeza listi...Ishu inakuja Je, hiyo listi yako iko salama???


Watu wengi wamepata pancha hapo katikati,wamefikia muda wanataka kutulia na kufunga ndoa kuanzisha familia...LOH!AFYA MGOGORO!Siku hizi magonjwa ni mengi sana,acha tu Ngoma inayozingua kila kona,kuna magonjwa ya Zinaa ambayo unaweza ukaletewa na bila kuyatibu vizuri ukaharibu vizazi ile mbaya.....Kuna ishu za mimba,maana mechi siku hizi pekupeku tu...ETI MNAAMINIANA,peku pekua mara kitu kimejaa...wote ndo mnagundua hamko tayari kwa mtoto!Upuuzi mwingine huo...Mko tayari kukata kiuno ila result za kiuno hutaki...Utafanyaje mtihani halafu useme hutaki majibu??utajuaje umefaulu au kufeli??Mapenzi bwana!Mwanamke wa watu analazimika kutoa mimba maskini,mwisho wa siku mkibahatika kuoana hampati mtoto,HALFU UTASEMA WHY ME LORD???KWELI???Au mtoto wa kike anaolewa na mtu mwingine,tayari ushamsababishia kimeo kwenye ndoa yake,na haya yako kila kona wala sio mapya.WAZA UPYA!


SABABU YA 5:LINDA HISIA ZAKO


Unampenda mtu unafanya nae Mapenzi...mnaachana,unapanga misururu watu wengi kama msururu wa wateja wa NMB kwenye ATM...Wote hawa unatumia moyo huohuo,hisia hiyohiyo,wote umewaonja,wamekupa different tastes,kama mia7 hivi....wote wamekutenda,Hisia zako zinakuwa na rangi kibaooooo,hata hukumbuki moja kati ya hizo ipi sahihi....
Nakutana na watu wanasema hawawezi kupenda tena,kia wametendwa....Sio hivyo...Sehemu ya hisia ishatiwa shoti,kila mtu kaja na bisibisi yake anachomeka tu,size 17 twendeeee size 44 twendeeee,haueleweki hisia zako zimefikia size ngapi,maana kuna waliozi-under size,na wengine wameku-oversize...Umeshakuwa emotionally unhealthy....


Kwanini usitulie uje utumie hisia zako kiusahihi na mtu sahihi???kwanza hawa unaosex nao wengi hata wazo la kuao hamna,wanakutumia tu bureee bureeee,ukimwambia tu twende home nikutambulishe anajitetea  na maneno lukuki kama konda wa Mazese-Mburahati,ndo utajua utatumiwa tu kama condom,kisha kitanda chako jalalani!


SABABU YA 6: UVUMILIVU NI TESTI NZURI YA UPENDO WA KWELI


Hapa hata sina haja ya maelezo mengi...Mtu mvumilivu huonyesha nia ya dhati na upendo wa kweli..Ila mtu anayekurupuka tu huyooo ndani ya Shuka,utajua tu penzi lake ni la ki-shuka shuka zaidi.


SABABU YA 7: BARAKA ZA MUNGU MLIYEMTII NA UTULIVU WA NDOA


Ukimtii Mungu huwa anatoa baraka zake...Na kinyume chake ni dhahiri...


Wle wanaomuamini Mungu na kufanikiwa kufikia hapa,maisha yao yanakuwaga tofauti kabisa na wale walioishi maisha ya kibiriti-Ngoma Style.


Watu mmetoka tangu urafiki mnaibatua amri ya 6 bila huruma....Sasa mnafika kwenye ndoa mmechokana,Ladha yote imakwisha,,Mke hana jipya la kukupa...Hakuna machejo ya Mme usiyoyajua....NO EXCITEMENT.


Sishangai kuona Mwanaume ameoa anacheat...Hamna jipya,Mke anabakia tu kuwa Kiwanda cha kufyatua Watoto lakini INTIMACY YA NDOA HAKUNA. Anaamua kujaribu ladha zingine!


Na effect za Mwanaume asiye na Intimacy na mkewe zitaonekana hata kwa Mkewe in due time...Hatampa haki yake kadri inavyopaswa,na mwishowe mkewe atachoka kulishwa Makombo,anayoyajua kwa Nusu Karne huko nyuma...


Kifuatacho hapo ni wote kugeuka CHEATERS...Mke anapiga show za nje kwa wizi...Mme nae anakamua mechi za Mchangani nje kwa kujiiba...Wote hawa wanajaribu kupasha misuli nje maana ndani Gym imeishiwa vifaa...Wanajifanya wanapasha moto Kiporo kilichochacha...Kamwe hiyo ndoa itakuwa ngumu sana kusimama tests of Time!
ARGUMENTS
Wengi wata-argue kwamba Maadili yanachangia.NAKUBALI,Siku hizi ni ngumu sana kumuamini Mpenzi kwamba atavumilia,ndio maana Wanawake wameamua kujitoa Sadaka kutoa tunda kama njia ya kuwin penzi la wanaume...UONGO!Penzi la Mwanaume halishikwi kwa kumpa Tunda...Kama anakupenda WEWE atakaa,kama alipenda TUNDA atakwenda...Simple Rule....Mwanaume anapaswa akupende WEWE kwanza na Sio ulichonacho Wewe...Afterall kama ana ana nia na hicho kitu,si atakimilikisha kuwa chake Milele na milele??sasa anakiwahi cha nini??kuku wa Kwako ya nini Manati??


Na wanaume pia,wanalalamika wanawake hawaaminiki,wana roho ndogo...Wewe unamtunza hupigi show unadhani kwamba anakutunzia unashangaa anakuja bwege flani anakula mali yako kiulaini,Roho inauma,so bora upige show ili hata ukiporwa,ah fresh mlinganyo umekaa poa.


Maadili yanachangia lakini na Ibilisi kwa kulitambua hilo,ameinvest hapohapo kwenye LOST FAITH ya Maadili,na anawachapa watu bila huruma.


Mimi nimemaliza hapa..Ukiamua kunisikiliza na kuamini Mungu na akubariki,ila nikiwa kama Jogoo anawahi kuamka lakini hafungui mlango haya..


             NATUMAINI MJUMBE SITAUAWA!


3 comments:

  1. big up!! sema wasikie wasisike we umetua mzigo hope so!!1

    ReplyDelete
  2. Thanx very much n be blessed...ofcourse wadada wengi inatukumba ili kutunza penzi...bt we hav to change coz wanaume wapo tu...kubal kuumia saiz kwa kuacha penz la maana ili ufurahie maisha...n God z truthfull n faithful...

    ReplyDelete
  3. Thanx very much n be blessed...ofcourse wadada wengi inatukumba ili kutunza penzi...bt we hav to change coz wanaume wapo tu...kubal kuumia saiz kwa kuacha penz la maana ili ufurahie maisha...n God z truthfull n faithful...

    ReplyDelete