Thursday, June 14, 2012

MUME WA ANGELA CHIBALONZA AOA MKE MPYAAAAA!!

Angela Chibalonza sio jina geni kwenye masikio yetu,amekuja mara kadhaa nchini Tanzania kufanya huduma na anapendwa sana kwa nyimbo zake ambazo miaka na miaka zitaendelea kutamba kwenye chati za Muziki wa injili.Nyimbo zake kama EBENEZER, Ni maarufu si tu Kabnisani,ila kwenye midomo hata ya watu wasio Wakristo.Ama kwa hakika alikuwa muimbaji mahiri sana sana!

ikiwa imepita miaka michache tangu Angela Chibalonza afariki kwa ajali ya Gari akiwa ametoka kwenye huduma huko Kenya, mme wake, Apostle Elisha Muliri ameoa mke mwingine ili kupunguza upweke na ili huduma isonge mbele.

Ni ngumu sana kufanya huduma ukiwa huna mke,vishawishi ni vingi sana na imebidi hata yeye aoe tu ili huduma isonge.

ANGALIA PICHA SIKU AKIFUNGA NDOA(Mwenye Kofia) NA MKEWE MPYA, MAGRETH
Apostle Muliri ni Kiongozi wa huduma ya Shekinah international ambayo mkewe wa Zamani, Angela alikuwa akihudumu pamoja

No comments:

Post a Comment