Tuesday, June 19, 2012

ANAITWA DIAMOND PLATINUMZ...KUTOKA OPA MPAKA LANDCRUISER PRADO....HAKI YAKE TUMPE,HEKO MWANABONGO FLEVA
Sikuwahi kudhani nitakuja kumuandika DIAMOND...Kwakweli ila imebidi...

Wanasema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,nami nampa heko zake...

Baada ya ku-release Hit baada ya Hit...Mbagala...Kamwambie...Nitarejea....Mawazo...Nimpende Nani...Lala Salama...na mpya alioshirikishwa na Diva,Piga simu...Pamoja na nyingine nyingi tu alizoshirikiswa na wasanii wenzie kama Shetta na Ommy Dimpoz....ANASTAHILI MAFANIKIO HAYA NA ANAJITENDEA HAKI

Baada ya ku-expose mjengo wake wa thamani ya Milioni 69 wiki chache tu nyuma,Diamond Platinumz alipata nafasi adhimu na adimu kwenda Bondeni kwa Madiba,South Africa kwenye Jumba la Big Brother kutumbuiza....Wiki chache tu baada ya Headlines hizo,another headline zimesambaa na kuthibitishwa naye mwenyewe kupitia Blog yake ya This is Diamond,baada ya kununua mkoko mpya aina ya Land Cruiser, Prado...
Nyota ya Jaha imemuangukia,na Mungu anabariki kazi za mikono yake baada ya kujituma na kufanya kazi bora kabisa tangu aingie kwenye Tasnia hii ya Bongo Fleva...Mwenzetu kahama kwenye ile Toyota Opa nw he gat the new ride...

1 comment: