Monday, June 18, 2012

TETESI:WOLPER ANYANG'ANYWA GARI ALILOSEMA NI LAKE AINA YA BMW X6

GARI ALIYOPEWA WOLPER,AINA YA BMW X6







Mwigizaji wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa gari lake la kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Bongo.

Habari zenye ukweli 100% ambazo Blog hii imezipata kutoka Mtandao namba 1 wa burudani Tanzania,Teentz.com, zinasema kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya  Milioni 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.



Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.



Aidha chanzo hicho, kimeieleza Teentz.com kuwa hivi sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa aliyokuwa anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake wa karibu washitukie mchongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana Teentz.com iliamua kumsaka na baada ya kupatikana Wolper aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.




Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tene kwa siku tatu Wolper alisema hivi: “Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaa



NGOJA TUSUBIRI TUONE UTETEZI WAKE MUDA SI MREFU MTASIKIA

No comments:

Post a Comment