Thursday, May 24, 2012

FALL FOR YOUR TYPE...MLINZI YAKE BAISKELI,MLINZI HAMILIKI VOGUE,ATAPATA WAPI WESE??

Kuna wanaume mnajitafutiaga matatizo wenyewe...Mnadate mademu wasio size yenu...Huwezi kuwa na Kitambi ukavaa Skin Jeans..Utachekesha...

Mlinzi wa KK security hawezi kumiliki Vogue,atapata wapi mafuta??Tanunua tu Baiskeli...

Chagua Level yako...Kama una life la Kuungaunga tafuta tu demu uswahilini,hawaombi hela zaidi ya elfu 20...sanasana vocha ya mia 5...

Ukichagua demu Mwanafunzi jiandae na Mizinga....Jiandae kusupport BOOM likichelewa...Utaombwa hela ya Disco...Babe twende Movie..

Ukichagua demu Corporate uwe umetulia haswaa...Akiumwa haendi Zahanati,Bebi nipeleke Burhani,au kwa Specialist wangu..utakoma....hakawii kusema BAbe naomba hata japo Toyota Vitz jamani huoni nateseka Usafiri..utatoa macho kama Mende kawashiwa taa ya Stoo...

Yaani anaomba Vitz kama anaomba hela ya Modem....Kazi kwako!

No comments:

Post a Comment