Thursday, May 24, 2012

MOYO WA MWANAMKE NI KAMA KIPANDE CHA DHAHABU

Moyo wa Mwanamke ni Kama Dhahabu...Ukipata bahati ya kuupata ukawa mali yako usiuache tu popote kama Mlevi anavyoacha Simu akienda kujisaidia...Utunze kama unavyoheshimu Subscription yako Ya bLackberry ikiisha unawahi Fasta kuongeza...

Moyo wa Mwanamke sio kama Funguo ya gari unairusharusha tu hata ikianguka ikitapakaa mchanga unapuliza tu...

Mwanamke akikupa Moyo wako ushikilie kwa nguvu,ukave na kila aina ya Vumbi,usiuchezee karibu na Matope maana ukiangukia humo hautatakata tena,utabakia na mabaki ya Matope...

No comments:

Post a Comment