Thursday, May 24, 2012

MAPENZI NI KAMA JACKPOT BINGO,YANATAKA BAHATI

Kama wewe umewahi kutendwa huko nyuma,usitangaze kwamba hakuna Mapenzi duniani...

Wewe ni kama mshiriki wa Lotto/Bahati Nasibu ya Jackpot Bingo....

Umenunua tiketi elfu 2,kila wiki unacheza holaaa...Mwenzio amenunua tiketi 2 tu ameshinda na ametangazwa kwenye TV anapokea kitita chake...

Huwezi kusema Jackpot bingo ni Uongo....Huwezi kusema hakuna Mapenzi duniani...

Umecheza bahati nasibu ukashindwa,kuna mwenzio mwenye bahati ameshinda...

Umejaribu kupenda ukatendwa,lakini kuna Mwenzio amejaribu amepata perfect relationship na anaelea kwenye dimbwi la mahaba wakati wewe unalia,eti hakuna mapenzi duniani...atakushangaa unaongea nini..

Muombe Mungu,Kushinda Bahati nasibu si wingi wa Tiketi unazonunua,ni Bahati...

kupata mtu anayekupenda sio uzuri wa Sura au hela ulizonazo,ni bahati...Unaweza ukawa na kila kitu na ukawa unalia kila siku

No comments:

Post a Comment