Monday, July 2, 2012

TABIA YA MTU NI KAMA SCREENSAVER

Habits are like Screensavers

Tabia ya mtu haijifichi.Atajitahidi kupretend tu kwa muda lakini ipo siku itajulikana tu rangi halisi.

Ni ujinga kuamini kinyonga ana rangi ya Kijani na ukaenda kusimulia watu halafu wamkute ana rangi ya Kijivu,mazingira ndio yanaset rangi yake.

Huwezi kutegemea kondakta wa Mwananyamala anyanyue kwapa lake kudai nauli halafu usubiri kama atanukia Perfume ya Isa Miyake,tegemea kikwapa kilichoenda Shule kitakachokupa Flu ya kukutosha wiki nzima.

 Ukitaka kujua tabia ya mtu,Mpe tu muda,hawezi kudanganya muda.Ni sawa na Msichana wa Kichaga,ataweka mikogo na Swaga zote lakini Mwisho wa siku lazima Tege lake la kufa mtu litaonekana tu,Miguu ya kichaga haiongopi,Mchaga asiye na tege labda amezaliwa Thailand

No comments:

Post a Comment