Thursday, May 24, 2012

KUNA WATU WAMBEA KAMA WAMEMEZA BLOG YA UDAKU...

Kuna watu wana midomo mirefu jamani,kama chuchunge!

Omba wasijue unadate na nani...Watachukua maneno kutoka huku na kupeleka kule...Na kuchukua kule kupeleka pale...wako bize kama Mesenja wa Shirika La Posta anasambaza barua..

Wataongea maneno Booklet nzima kama Hansard ya Bunge....Oh unadate na yuleeee,Mwanaume ananuka Boxer yule...Ohh Mwanamke yule kicheche amewahi kufumaniwa Corner Bar..ohh mwanau me bahili yule...oh Mwanaume alikuwa anampiga demu wake wa Zamani....Oh Mwanaume yule hafai amekimbia Mimba Ileje huko kakimbilia mjini...

MMETUMWA????

Yaani Mpenzi wako mna uhusiano wiki 2 tu lakini kashalazwa Aga Khan mara 6 kwa presha ya kushuka,maana leo anasikia hili kesho lile...KAma mna maneno mengi ya kuongea kuharibia wenzenu si mfunguo Blogu ya Udaku tujue moja???

Tumechoka jamani hatuhemi,Kila siku Mahusiano yetu tafrani kwa ajili yenu...

No comments:

Post a Comment