Tuesday, February 14, 2012

Mapenzi na Ujinga ni Bestfriends-Huwezi kuinjoi penzi la kweli kama wewe sio mjinga,huwezi kudumu kwenye relationship kama wewe sio mjinga

Mapenzi na Ujinga ni Bestfriends wanaopendana sana,huwezi kuwatenganisha,wanaenda kulala wote,wanaenda shopping pamoja,wanashara hadi mswaki..Huwezi kuinjoi penzi la kweli kama wewe sio mjinga,huwezi kudumu kwenye relationship kama wewe sio mjinga,wakati mwingine wapenzi wanafanya makosa makubwa ila unasamehe ili penzi liendelee japo usingependa kusamehe hilo kosa,ujinga umefanya kazi yake...Bila kuwa mjinga ndugu zangu mapenzi hayaendi,usipoletewa zawadi Valentine,usipotafutwa na mpenzi,kuwa tu mjinga yatapita,ikifika tarehe 15 penzi lako linarejea...Habari zenu wajinga wenzangu,hope mnaendelea vema leo,endeleeni hivyohivyo,msipokuwa wajinga kila siku mtakuwa Single asikwambie mtu kuwa single inataka uwe na moyo wa bati la south Africa.

No comments:

Post a Comment