Friday, May 18, 2012

UFAGIO WA ZAMANI NDIO UNAOJUA KONA ZOTE ZA VUMBI

Watu wengi hupenda kudharau ufagio wa zamani,na kupendelea ufagio mpya..kwa sababu zilizo wazi,unakuwa umejaa,chelewa zote zipo kamili,na pengine unanukia upya..

Unafeel vizuri kutumia ule mpya na kuuona ule wa zamani si mali kitu

Ila kwa upande mwingine, Ufagio wa Zamani,ule unaoonekana umechoka,uko hoi,na mkuu-kuu,ndio umekuwa uking'arisha nyumba kwa miaka nenda rudi...Unajua kona zote za nyumba yako,wapi vumbi linajificha,umepenya na kuhakikisha nyumba yako imekuwa safi na inang'ara....

Kumuacha mpenzi wako uliyekaa nae kwa muda mrefu kwa sababu tu amekuwa mkuu-kuu,na kum-replace na yule mpya ukitegemea ataziba hizi defect ndogo ambazo ulizitumia kumtimua huyu old inaweza isiwe suluhisho la matatizo yako..

The old partner knows all corners of you...Mpaka huyu mfagiaji mpya aje azigundue kona hizi zote,ndo aanze na kuziba matundu ya fagio la zamani,Sio leo...

Je,ukazane na fagio la zamani?Au ununue jipya? Its always a challenge to make decision when it comes to Love...all in all,make decision wisely....Old might be gold but leave you cold....And new can also disappoint you....Mapenzi sio rahisi,play your cards well

No comments:

Post a Comment