Monday, January 14, 2013

WAKATI MWINGINE SECOND CHANCE HAINA MAANA KWA BAADHI YA WATU,WANAITUMIA VIBAYA

Yes ,Lovers!Once again,naleta mzigo mwingine muuthaminishe wenyewe...

Wote tuna mioyo na hisia,wote tunafall in love kila siku maana tuko tunatafuta Penzi la kweli...Penzi la kweli sometimes ni ngumu sana kulipata,ni safari yenye milima na mabonde..the journey is hard...

Katika pitapita yako,bahati nzuri ukaokota kijamaa au kidada,ukakipa moyo wako mwenyewe,una-expect kitautendea haki...kitakupa mahaba..Kitakupa mambo adimu,sio kama wale wengine ealioudundisha kama Kitenesi...
.....Kiupe mdomo wako smile na sio mnuno kama ufudu...
....Kiupe moyo wako sababu ya kupump damu kwa raha na sio kuuchezesha kiduku..
....Lakini wapi...Kinafanya tofauti na ulivyotegemea...

Inafikia kipindi unaamua,bwana basi! Enough is enough wanasema Waingereza!Unanyosha mikono juu hata kama unaamini wewe ni shujaa wa Mahaba..

Umejaribu kila mbinu kufanya Love Life yako ikupe furaha imeshindikana....
....Umejaribu kujifanya mjinga imeshindikana...
....Umejaribu kujitoa,kumfanyia mpenzi mambo mazito ambayo hata mzazi wako humfanyii maskini,Ili tu,Penzi lako liende vizuri....

LAKINI,Mtu unayemfanyia hayo yote,Je,Yeye anachukulia mambo kwa uzito sawa na wewe???Au umejitwisha Injini ya Scania peke yako???
Mara nyingi watu tunaowapenda na kuwabeba mioyoni mwetu kwa uaminifu na Mapenzi na Huba,hawajali lolote...Wanakuona Kichaa tu,na pengine wanashangaa,kwanini huyu Mwanamke anahangaika hivi???Kwanini hili Lijanaume linanipenda hivi,halina kazi???

TATIZO LINAPOKUJA,Pale unapoamua its over,utashangaa!!

Mtu huyuhuyu aliyeonekana hajali lolote pamoja na Mapenzi yote uliyompa,anakuja kwa nguvu,Atapiga magoti,ataomba marafiki msaada wamuombee msamaha...
Anaweza kuita hata Matrafiki wamsaidie kukwamua gari lake limenasa...Unajiuliza,alikuwa wapi hadi amesubiri haya yote yatokee ndio aonyeshe umuhimu wako kwake kwa misamaha yenye ahadi kama nyingi kama Ilani ya CCM??

ANAOMBA UMSAMEHE,UMPE NAFASI TENA...

Unaona sio ishu,maadam kaomba unampa...Anajitahidi wiki ya kwanza,fresh...Ya pili poa....ANASAHAU...

Mnarudi kulekule,vichozi vyako vilivyojikusanya kwa Wiki 2 za Mapenzi ya Ampicillin vinamwagika tena mwaaaaaaaaaaaaa.....
Na aliyevimwaga ni MTU YULEYULE??

Swali ni Je,NINI UMUHIMU WA SECOND CHANCE kwa mtu asiyeweza kuitumia Second Chance kujirekebisha????

Upuuzi uleule.
...Makosa yaleyale..
...Ujinga Uleule.
...Mateso yaleyale,na maskini ya Mungu Moyo ni huohuo,unauongezea tu Ufa....Matundu....Vidonda.....

JIHURUMIE WEWE KABLA HUJAMHURUMIA YEYE....

Kama kuumia unaumia wewe...Kama yeye alivyo na Moyo,na wewe unao pia,tena wa nyama....

Hata ukimpa SECOND CHANCES ELFU 8,kama habadiliki HAKUFAI...

Maana halisi ya Second Chance huonekana pale MPEWA anapogundua Makosa na Udhaifu na Kuitumia Second Chance kuonyesha kwamba Mapungufu yale ilikuwa ni Bahati Mbaya tu na Kujisahau.....

Kumis-Use Second Chance kwa Kurudia yaleyale ni TUSI kwako kwamba ''Wewe ni Mjinga kwa kunipa Nafasi ya Kukuumiza kwa Mara nyingine tena''...

Think twice kabla hujampa Mtu Second Chance,ANAMAANISHA au Anaiomba kwa sababu ipo kwenye Kamusi????

TAFAKARI

2 comments:

  1. Nakubaliana na wewe asilimia miamoja kaka, ila kama ndo upo kwenye relationship ukiona hizo dalili unakimbia kama huna akili nzuri what if mshaoana tena ndoa ya kikristo? kwa hawa wenye ndoa unawasaidiaje?

    ReplyDelete
  2. NDOA INAONGOZWA NA SHERIA ZA KIMUNGU,HESHIMU KIAPO CHAKO KWA SHIDA NA RAHA...ULIAPA.NDIO MAANA UNAPEWA MUDA MREEEFUUU KUCHAGUA,ILA ONCE UKISEMA I DO,HAINA TENA MJADALA,KUFA NAE KWA SHIDA NA RAHA

    ReplyDelete