Friday, July 6, 2012

AUNT EZEKIEL AFUNGA NDOA KIMYAKIMYA DUBAI

Msanii Maarufu wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel ameripotiwa kufunga ndoa na Mchumba wake ajulikanaye kama Sunday Dimonte nchini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE)Ndoa hii inaripotiwa kufungwa June 17, wiki 2 tu zilizopita.

Habari zinadai kuwa, Aunt alifikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kumwambia hawezi kuvumilia umbali uliopo kati ya Tanzania na Dubai hali ambayo Aunt alihofia kupigwa chini.

Waandishi walimsaka Aunt kwa njia ya simu ya kiganjani akiwa Dubai, alipopatikana na kuulizwa kama kweli amepigwa pingu za maisha, alifunguka:
“Ni kweli nimefunga ndoa huku Dubai lakini nimesikiasikia kuna watu wanasema nilifanya siri. Siyo siri, ila huku ni mbali na huko nyumbani Tanzani, isingekuwa rahisi kuita watu wangu wa karibu.”
Paparazi: Kwa hiyo ndiyo imetoka hiyo?
Aunt: Hapana, nitakaporudi nyumbani nitafanya sherehe, nitaalika watu, hata wewe, tena itabidi unichangie jamani.

Ngoja tuone akirudi itakuwaje.Kama ni kweli, Aunt Ezekiel atakuwa amejiunga na wasanii wengine wa Bongo movie waliowahi kufunga ndoa kama Irene Uwoya na Wastara.


Tunaomba iwe hivyo!

HABARI KWA HISANI YA RAFIKI YANGU JOHN KIANDIKA

No comments:

Post a Comment