Tuesday, June 5, 2012

SI KILA MPENZI UMPATAYE ATAKUOA..WENGINE NI MITUME TU

Si kila mpenzi ajaye maishani mwako wewe unawaza ndoa tu,na asipokuoa basi unabaki unalia weee na kujihisi una mkosi.
 
Wapenzi wengine hutumwa tu na Mungu kwa kusudi maalum kwa muda maalum,na kusudi likiisha lazima waondoke,hata ufanye nini!
 
Si kila mpenzi atakuwa Mke au mume,Nimejifunza kulielewa hili na ninamshukuru Mungu kwa mengi niliyojifunza in my Past relationships.Nawashukuru ALL my past Girl...friends,kwa changamoto na elimu waliyonipatia kuhusu Love,wale mlioutesa huu moyo na kuubondabonda kama Korosho,wale mlionisulubu kisa mlijua nawapenda,mmenifundisha mengi sana,pokeeni Shukrani zangu!

 Acha kulialia ukiachika,mara ooh nilimpenda tungezaa watoto wazuri wenye vichogo,hilo halikuwa kusudi la Mungu,atakupa mtu sahihi aliyekupangia na utafurahi,yule alikuja kwa kazi maalum tu.
 
Wake up,Learn and Move On...

2 comments:

  1. ni kweli tunakuwa tunajifunza kutokan na maumivu na mapito tunayoyapata

    ReplyDelete
  2. mwingine alikuja just to show yu a certain path baada ya hapo task ikikamilika anatoka

    ReplyDelete