NDEGE YA DANA AIRLINES ILIYOANGUKA NA KUUA WATU 153 JUMAPILI
Ile ndege ya Dana Air MC Donnell Douglas MD 83, iliyoanguka juzi maeneo ya Iju-Ishaga, Lagos Jumapili inajulikana kuwa na historia ya Ubovu hata kabla haijanunuliwa kutoka kampuni ya Alaska Airlines,ya Marekani na Dana
Airlines ya Nigeria mnamo February 17, 2009.
Ndege hii ilinunuliwa na Alaska Airline mnamo November 13, 1990.
Miaka 12 baadae mnamo November 4, 2002,Ndege hii ilipata hitilafu na ikabidi igeuze njia kwa dharura baada ya kutokea moshi kwenye cabin area.
Ndege hii ilinunuliwa na Alaska Airline mnamo November 13, 1990.
Miaka 12 baadae mnamo November 4, 2002,Ndege hii ilipata hitilafu na ikabidi igeuze njia kwa dharura baada ya kutokea moshi kwenye cabin area.
August 20, 2006, Ilibidi abiria waondolewe kwa dharura tena baada ya kutua uwanja wa Long Beach, California, baada ya kuonekana Moshhi tena kwenye cabin area,ila watu wakauchuna tu. Baada ya matatizo haya mfululizo Alaska Airlines mnamo August 21, waliipaki ndege hiyo hadi September 11 2008 na wakaipeleka kwa matengenezo. Miezi 5 baadae baada ya matengenezo kumalizika, ndipo walipoiuza ndege hiyo mnamo February 2009, kwa to Dana Airlines ya Nigeria.
Unaweza kuona jinsi gani nchi za Africa zinakuwa Dampo la bidhaa chakavu na Mbovu.Hatujui hili tatizo linatufundisha nini sisi kama Watanzania,maana Usafiri wetu wa Anga nao uko dhoofuli hali,hatuna uhakika hata hizi ndege wanazopaka rangi na kusema wamenunua ziko kwenye hali nzuri kiasi gani kwa Usalama wetu.Mungu tu anatuokoa kwakweli!
RAISI WA NIGERIA,GOODLUCK JONATHAN AKILIA MACHOZI BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO
Tukio la karibuni,wiki chache tu nyuma,mnamo May 23,Abiria walilazimika kuchelewa kuondoka kutoka uwanja wa Ndege wa Lagos baada ya ndege hii kupata hitilafu tena kwenye mfumo wake wa Hydraullic.
Ila yote hii haikutosha kutoa WARNING kwa Mamlaka ya hali ya hewa kuzuia ndege hii kuendelea kutoa huduma za ndege bila matengenezo madhubuti hadi ilipoanguka juzi na kuua Roho za watu 153 waliokuwa kwenye ndege hiyo. Inasikitisha kuona picha za waliokufa,wengine wakiwa ni watu wa familia moja,wakiteketea kwa uzembe huu.Hili liwe fundisho hata kwetu hapa Tanzania,Usalama wa Ndege uchekiwe kabla hayajatokea maafa makubwa!
Historia inaonyesha ndege hii ilitengenezwa mwaka 1983 na ilirushwa kwa mara ya kwanza December 17, 1984
MABAKI YA NDEGE YA DANA BAADA YA KUANGUKA KWENYE KIJIJI
Habari kwa hisani ya my friend, Linda from Lagos
Aisee bad news kweli kweli, cjui usafiri upi utakuwa bora jaman, mungu tunusuru na haya maajari, pole Nigeria na walopoteza ndugu zao, Inalillah Wainaillah Rajiruun.
ReplyDelete