Tuesday, June 5, 2012

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU ATUMA UJUMBE WA KUAGA FACEBOOK KISHA AJINYONGA!DAAH

Ama kweli Facebook imeleta mambo duniani! Yaani mtu unataka kujiua unakumbuka kwamba kuna Facebook,unaingia,una-Log in,unatuma Post then Una-Log out,unaenda unajiua!Hii ni kali ya Mwaka!

Mwanafunzi huyu,mpaka sasa haieleweki nini hasa ni chanzo kilichosababisha exactly ajiue lakini kuna element kwamba kuna shida flani aliipata akiwa chuoni na kuna maneno yalisemwa dhid yake na hakuyapenda,akaamua kufikia uamuzi wa kuukatisha uhai wake kwa Kamba kwenye mti wa Mwembe kijijini kwao,Ipaja mjini Lagos!

Jina lake kamili ni Ayodeji Balogun,Mwanafunzi wa Chuo Kikuu kinachoitwa National Open University mjini Lagos ambacho ni equivalent na Open University of Tanzania (OUT),kwa hapa kwetu.

HUYU NDO JAMAA MWENYEWE ALIYESUSIA UHAI WAKE KISA AMESEMWA CHUONI..MKUBWA KWELI ILA DAH


Kinachonishangaza mimi sio uamuzi wake wa kujiua...Watu wengi wanajiua kwa sababu mbalimbali,ILA,style yake ya kujiua...

Yaani kweli unajiua unakumbuka Kupost Status,Facebook...Whats on your Mind??/Unaandika Goodbye to you all mi najiua,duh,kweli Izraili mtoa roho nae ameanza kupenda teknolojia.

CHEKI STATUS ALIYOPOST JIONI YA JANA KABLA HAJAJITOA ROHO KWENYE MTI WA MWEMBE! MSOMI KABISAAA WA CHUO KIKUU!

2 comments:

  1. inatsikitisha ..mhh sijui wamemfanya nn uyu

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha kweli.
    Ila kuna ishu ya kisaikolojia inaweza ingia hapo, mfano: wanaume wengi katika ukuaji wetu sana sana wakati wa kubalehe huwa tunakosa mwanaume wa kutuandaa nasi kuwa wanaume. Maana mwanaume inabidi aandaliwa toka uvulana, lazima ukuzwe na kufundwa nini maana ya uanaume na wajibu unaokupasa kwenye jamii. Tamaduni za zamani zilikuwa zinalitambua hilo na kuhakikisha linafanywa kwenye ngazi ya kila familia. Sasa hio kiakili inamuandaa mtu na kuelewa kinachompasa ni nini.

    Sasa siku hizi, hata mababa zetu wengine hawafahamu maana ya kuwa mwanaume ni nini na wengi ni matokeo ya kukosa hio elimu au hayo maandalizi. Unakuta baba mzima anaweza kuwa analewa muda wote na kusahau majukumu yake, au pamoja na kuwa na familia lakini pia haijali inavyotakiwa n.k.
    Sasa hata kama baba upo nae ila katika kipindi cha kubalehe hakuwahi kukuandaa kuwa mwanaume au mawasiliano kati ya baba na mtoto hayakuwa mazuri, watoto wengi huweza kupata matatizo ya kisaikolojia.

    Kama huyu jamaa aliejiua, ukiangalia status zake nyingi ni za kujipa moyo, ni kama mtu ambae alikuwa anaumia moyoni lakini alikuwa haioneshi na kutokana na hilo kuna wakati jamii inaweza ikafanya jambo la utani kwake, ila yeye akalichukulia kiukweli moyoni na kuzidi kumfanya awe na hisia mbaya juu yake. Mara nyingi watu kama hawa hupenda sana sanaa ya aina fulani aidha kupiga ala, au kuchora au uandishi, sababu hio inakuwa ni kama njia ya kuionesha jamii yale yanayomkuna moyoni mwake.

    Na ukiangalia vizuri jamaa atakua aidha baba yake alifariki au kupotea akiwa mdogo, au kama alikuwepo basi baba alikuwa hampi nafasi ya yeye kuji-express yeye kama yeye!

    ReplyDelete