Wednesday, June 6, 2012

DAWA YA MBU ALIYEKUAMBUKIZA MALARIA SIO KUMPIGA BUNDUKI,NI EXPEL TU..HASIRA HASARA

Idadi ya chuki na hasira unazobeba moyoni mwako kutokana na vile wapenzi wako wa zamani walivyokufanyia vitu ambavyo unadhani hukustahili kufanyiwa,aidha kwa kupigwa kibuti bila kutegemea,au mpenzi kuchukua kipusa kipya na kukutosa kwa kashfa,au kuwa cheated pale ulipopenda sana,kutakufanya uwe kilema wa kupenda siku za usoni.
 
Kamwe usipende kuingia mahusiano mapya bila kusamehe kile kilichotokea ...kwenye past relationship,ukifanya hivyo,utakuwa kama mtu aliyegongwa na nyoka,hata akiona mkanda mweusi anashtuka.

 Utajikuta unaishi kwa dalili,ukiona wingu kidogo unahisi kuna el nino inakuja kumbe ni watu tu wamechoma takataka nyumba ya Jirani....

 Jifunze kusamehe waliokutekenya moyo na kuuacha unacheka wenyewe,lasivyo utajikuta unalalamika kwamba huwezi kupenda tena kumbe kosa ni la kwako umeshindwa kuachilia visasi vya Past.Dawa ya mbu aliyekusababishia Malaria kamwe sio kumpiga na bunduki kwa hasira,nunua Expel tu kwa Mangi unampulizia kidogo tu

2 comments:

  1. BUT SOMETIME TUNATAKIWA KUWA FUTA MBALI WALIOTUUMIZA KAMA HIYO ITASAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU YETU.. HAKUNA ATAKAE PENDA KUENDELEA KUUMWA MOYO WAKE KILA AJARIBUPO KUSAMEHE HARAFU MKOSAJI HAELEWI .SOO PLAN B NI KUFUTILIA MBALI NA KUANZA MBELE.I THINK SASA ITAKUWA FAMIGATION KABISAA NA SI EXPEL

    ReplyDelete
  2. I LOVE HIZI POST ZAKO HASA KUANZIA HII YA DAWA YA MBU KUPANDA JUU..............SO EDUCATIVE NA NDO UKWELI WENYEWE...BT ZAIDI NAPENDA LANGUAGE UNAYOTUMIA...NI FUL UJANA HUMU YANI......BIG UP SETH

    ReplyDelete