Monday, May 14, 2012

ACHA KUGUNDUA STEP MPYA YA KWAITO WAKATI MUZIKI UMESHAISHA...UKIPENDWA PENDEKA

Acha kugundua Step mpya ya kwaito wakati Muziki ushaisha,muda wa Blues we ndo unapiga viduku...
Ulipopendwa kwa dhati ulijiona we malkia sana,ukadengua mwenyewe....Ulipopendwa ukajiona wewe kidumeeee,super handsome kama Ommy Dimpozz,mapozi mengi,hujali aka Mr dont Care,ukaona umemshika masikio,haendi kokote,ukajua mtaani hakuna wenye mapenzi na mbinu kukuzidi wewe...
Sasa kapata mtu mpya,AMEHAMIA ...AIRTEL,Basi lina nafasi tele,anajinafasi,na kujimwayamwaya,unaanza kuleta Drama,ooh I need you back..Hakuna cha I need you back wala I need you front,ndo umeshahamwa hivyo,mapenzi yako yako bondeni na kuna mafuriko,mwenzio kaogopa kuzama kahamia Magwepande.
 
Tafuta tu kibito kingine ujishikize ujifunze kuthamini penzi...

Ukipendwa pendeka,kuna watu wana mahaba huku nje wanamtolea macho huyo bishosti na huyo kidume wako,utatemwa uanze search upyaaa na huku mtaani network busy,utazeeka

No comments:

Post a Comment