Monday, May 14, 2012

UNAKULA BATA TU WAKATI HOME KWA WAZAZI HALI MBAYA...TUBADILIKE

Vijana wa siku hizi ndo maana tunakufa mapema..Hatuwajali wazazi tunaendekeza sana starehe...
Mungu amekubariki umepata kazi nzuri angalau,mkumbuke mama yako japo umbadilishie Kitenge chake kilichochakaa..Mkumbuke Babako japo na kiatu,kila akikivaa ajisikie kweli ana mtoto...Kumbuka wadogo zako japo na Uniform mpya uwapunguzie mzigo wazazi kwa vitu vidogo vidogo..

Sasa wewe ni Bar tu,Bata tu,kila mahali unajifanya we ndo wewe wakati wazazi wamekusomesha kwa shida,walijinyima ili uwe na maisha mazuri,umewasahau..

Unajidai wa kishua sana mtaani wakati nyumba yenu imeezekwa na bati la msaada limeandikwa KORIE mafuta bora ya kupikia na kenchi za miti...Kumbukeni mlikotoka,kidogo ulichonacho jaribu ku-improve maisha ya nyumbani kwenu.

Wazazi wakikubariki hata mambo yako yatakunyookea.,Tunakosa baraka hivi hivi kwa kujifanya wajuaji..Ushauri tu wa Bure...Love your parents

1 comment:

  1. hili nalo ni tatizo wapo wapumbavu wachache kama hawa wengi tu

    ReplyDelete