Tuesday, May 15, 2012

ZAWADI BORA YA KUMPA MWANAMKE NI TRUE LOVE,VINGINE NI EXTRA TU

Je, unajua zawadi ambayo unaweza kumpa mwanamke yoyote,(asiwe tu gumegume maana gumegume halipendeki),ili akupende na kukupendakwa dhati mpaka kufa??

Siri ya kupendwa na mwanamke haiko kwenye gari zuri la kutembelea unalotaka kumpa,haiko kwenye Handbag za Louis Vuitton ulizomjazia chumbani,haiko kwenye Bikini za Cassandra Lingerie unazomnunulia wala hela unazompa eti ili umlinde..

Zawadi ya thamani unayoweza kumpa mwanamke ikagusa moyo wake ni TRUE LOVE AND CARE kwake,ajihisi anapendwa nawe kwa dhati na sio penzi la mgawanyiko...True Love ni core product kwenye mahusiano,hivi vingine hivi (Augmented/Extra/Auxilliary tu,vinasaidia tu Core product ibakie bora ili iuze sokoni...Usihangaike kutafuta Augmented products wakati Core Product unayouza iko mahututi,penzi litakufa tu...Usipompa true love huyo mdada hata umpe bilions ni kazi bure,ni sawa na kuuza vitabu vya Tenzi za Rohoni kwenye msikiti wa Al Hushoom Kariakoo,utatolewa baruti pekupeku..

1 comment:

  1. Ni ukweli mtupu huu kaka nakuunga mkono

    ReplyDelete