Tuesday, May 15, 2012

HATA KIPOFU KUNA SIKU HUWEZA KUKONYEZA..UKIMPENDA MTU MWAMBIE,USIOGOPE


Wanawake wazuri na wanaume wazuri wako wachache sana kwa sasa....Ukimpenda mtu ni heri umwambie tu ajue...Zile zama za kale za kumpenda mtu halafu unauchuna eti atanionaje,au atanijibuje zimepita,unakufa na kijiba cha roho,ukimuona unahisi roho yote inaungua na gari la Fire liko mbali...
 
Wanawake wazuri na wanaume wazuri ni kama mikeka iliyo sokoni,we unapita unasagulasagula tu,unashika huu unaacha...,unashika ule unaacha,unatamani lakini unakuwa bahili kujitoa mhanga,mwishowe unamwambia muuzaji utarudi baadae...
Wenzio wakija wakiona mikeka sokoni,mizuri,inalipa,wanaulizia bei,hata kwa kushindana kwenye mnada hadi wananunua na kulipa,we ukirudi unakuta tayari kitambo unabaki unasikitika..Sio lazima umropokee usoni kama unaona utaonekana cheap kama ganda la vocha iliyotumika,tafuta mbinu mbadala na ujumbe utafika tu.Usiogope kusema,kuna siku kipofu huwa anaweza kukonyeza

No comments:

Post a Comment