Tuesday, May 15, 2012

MAPENZI YA KWELI HAYANA MASHARTI KAMA BRELA

Ukisikia Sentensi yoyote inayoanza na hili neno kwenye mapenzi yenu,ujue kifuatacho hapo si salama kwa afya ya penzi lenu:

KAMA KWELI UNANIPENDA..... ninunulie japo Vitz tu mpenzi nimechoka Daladala..
KAMA KWELI UNANIPENDA..twende Bagamoyo kwenye Birthday yangu mpenzi
KAMA KWELI UNANIPENDA...tumlipie mdogo wangu ada anadaiwa
KAMA KWELI UNANIPENDA...Ninunulie na mimi Blackberry Torch,all my Friends... are on BBM baby
KAMA KWELI UNANIPENDA....nipe Password yako ya Facebook
KAMA KWELI UNANIPENDA..sitaki nikuone tena na rafiki yako yule Kataza na Polite,siwapendi kama nini...KAM KWELI UNANIPEND...hamna kwenda Club,TULALE...

Hili neno,popote linapotumika ujue kuna tatizo,linamaanisha you have to prove something kuhusu wewe kumpenda yeye,na kwenye mapenzi inapofikia kila kitu kiwe proved namna hii ujue muda si mrefu Baraza lenu la Mapenzi litapigiwa kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na litahitaji sahihi 70 tu za wabunge ili Penzi lenu life kibudu,ni bora mvunje tu baraza hilo..

No comments:

Post a Comment