Tuesday, May 15, 2012

MAHUSIANO NI KAMA BATTERY,INATEGEMEA UNATUNZA ENERGY KIASI GANI KUFIKA MWISHO WA SAFARI

Kuanzisha uhusiano na mtu sio big deal wala,ni rahisi tuu,unakusanya vihisia weeeee kwa muda mreefuuuu vikifika GB 8 tu mnaingiza Modem mnaanza kubrowse Mapenzi Explorer....

Kufahamiana tabia baada ya Browsing Session kuanza ndo mtihani wa kwanza,Windows zingine ziko Slow sana hadi zinaboa unaweza kuzima Laptop..
Kusolve matatizo ya uhusiano wenu ni tatizo,lazima mjue fundi gani wa kumtumia ili ku...hakikisha Laptop yenu ya Mapenzi inarudi kwenye ubora wake...

Kuendelea kupendana kama Mwanzo,kusikilizana,na kusonga mbele kwenye mapenzi bila kujali mawimbi ya hapo katikati ni Mtihani wa Taifa...kufaulu kwa kutegemea kupiga chabo kwa wenzako wameandika nini ni sumu kubwa,lazima ujiamini kwa kumsoma mwenzio ili uweze kujibu mtihani na kufaulu...
La sivyo,kabla hujamaliza mtihani kengele ya Low Battery italia,Its now safe to Shut down the Computer...

Uhusiano wenu mliouanzisha kwa mbwembwe nyingi kama mtoto mdogo kaonyeshwa ice cream UTASHUT DOWN..Kabla ya kuanzisha penzi lenu hakikisha mna battery ya kutosha ku-run PC muda mrefu

No comments:

Post a Comment