Tuesday, May 15, 2012

WASICHANA NI KAMA MTI WA MA-APPLE

Wasichana ni kama Ma-Apple yaliyo juu ya mti,yale Ma-Apple mazuri huwa yanakaa juu sana karibu na kilele kabisa,yale mabaya yananing'inia karibu karibu...Wanaume wanaona kupanda hadi juu kule sio ishu,wanachuma haya yanayoning'inia karibu na chini coz hayahitaji hustle ya kukwea mti,ya nini uvunjike kiuno bure kusaka Apple lilio kileleni..

Yale Ma-Apple yaliyo juu yanaanza kupata Maswali,Stress,Lo...neliness,kwanini wao hawatunguliwi?wana matatizo gani?wanakosa raha,kumbe hawana matatizo,matatizo ni ya wanaume wamezoea kutungua vilivyo karibu karibu...
Mwisho wa siku yale Ma-Apple yanaiva weeee huku yana Stress yanaanguka chini maskini,yanakumbana na Mbwa na Mapaka Shume,hayakuwa hata na habari kwamba yamekaa chini ya mu-Apple,yanalamba,yanakula burebure!


Je, wewe ni Apple la juu au la kuning'inia???Wanawake wazuri huangukia wanaume Wabaya na Ma-Player kwa kushindwa kuvumilia,Wanaume wazuri siku zote huchelewa,wana mapozi,hawataki kupopoa mapema hadi uive na jua...Kazi ni kwako

No comments:

Post a Comment