Tuesday, May 15, 2012

UKITAKA WIFE MATERIAL BE A HUSBAND MATERIAL KWANZA

Wewe unajijua sio Husband Material,lakini kutwa kucha umekazana kutafuta Wife Material,,oh Mademu wa siku hizi feki kabisa sio Wife Material,utawapata wapi wakati we mwenyewe una Harakati za dokta Pimbi??Chuma hufua chuma,Mgogo na Mchaga wataweza wapi kuelewana kama kila mmoja anaongea kilugha cha kwao?
Sumaku inavuta chuma na jamii ya Chuma,hainasi kwenye Sahani ya Udongo hata siku moja.Kama wewe sio Husband material jiandae kukumbana na mcharuko,usitegemee muujiza.Badilika wewe kwanza na Wife Material atapatikana kirahisi mbele ya macho yako,lasivyo kushnehi...Utasubiri sana,utazeeka hadi macho yataota vigimbi,hata siku moja Kipofu hawezi kwenda jela kwa kesi ya kukonyeza

1 comment: