Tuesday, May 15, 2012

MUZIKI NA MAPENZI NI KAMA KAKA NA DADA

Muziki na Mapenzi ni kama Kaka na Dada,wanafanana sana kitabia,ukimuudhi mmoja basi wote wananuna na matokeo yake hutawapenda wote wawili..
Muziki ni mpangilio wa sauti zilizopimwa kwa urari na mirindimo iliyopangika ili kutoa tune yenye kupendeza na kuburudisha wasikiao mdundo...
Sauti zikipangwa vibaya unatoka wimbo mbovu na tune itakuwa Flati,haipendezi hata kusikiliza na utazima redio.
..Mapenzi... yanahitaji mpangilio kama Muziki,mpangilio wa jinsi mnavyoishi,mapenzi yanayolingana na sio mmoja juu mwingine chini hana habari,maelewano,kusameheana,na sio kununa kama fenesi lililopigwa na jua,hapo mtatengeneza Flati..

Ukitaka uhusiano wako uwe na outcome nzuri,hakikisha una Beat nzuri,Shirikiana vizuri na Producer wako aka Mpenzi,fundishaneni vizuri jinsi gani ya kuimba ili wimbo utakaotoka uwe Wimbo mkali mtaani.

Mkipishana tu sauti mjue Album yenu haitauza

No comments:

Post a Comment